Kama huelewi ubaya wa Majimbo ya Lissu, angalia kinachoendelea Ethiopia

Kama huelewi ubaya wa Majimbo ya Lissu, angalia kinachoendelea Ethiopia

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,892
Reaction score
7,780
Kwa wale wa CHADEMA iliyokataliwa na Watanzania nawashauri wafuatilie kinachoendelea Ethiopia. Sera za majimbo alizokua anazipigia chapuo Lissu ndio hizo huko Ethiopia zimesababisha serikali ya Taifa Addis Ababa kuingia vitani na Serikali ya jimbo lake la Tigray. Jimbo lina Rais lina Bunge lina jeshi lake hayo ndio Lissu anataka kutuletea.

Wakati Ethiopia wanatamani wangekua na umoja kama sisi Lissu anatamani tuwe sio kitu kimoja kama Ethiopia. Ethiopia wana majimbo kutokana na kuendekeza tofauti zao za kikabila sio kwa mapenzi ya utaifa wao.

Umajimbo ni rahisi kusambaratishwa Taifa na maadui kuliko kuwa Serikali moja imara yenye mikoa na wilaya zilizo na uwakilishi imara kwenye Serikali kuu. Hakuna kitu hatari kwa umoja wa kitaifa kama kuwa na majeshi ya kivita yanayomilikiwa na mamlaka tofauti kwenye nchi moja.
 
s
Wewe Fisi mbona unatapatapa sana wewe nenda katafute mzoga huko lumumba
Sio anatapatapa, anasema ukweli CHADEMA ilifika hatua wakawa wana usemi wao eti Lissu ana akili sana. Kumuelewa Lissu unatakiwa uwe na akili kubwa sana haha dah. Sasa yuko wapi? Nyie mnao muelewa haya tuambieni mbona kawasaliti sasa hivi kaenda kula raha tu huko nje.
 
Mbona kwa Akina Nkurunziza hakuna majimbo na vita vya wa hutu na wa tutsi kila siku?
Namibia. Botswana. South Africa. Kenya etc kuna serikali za majimbo lakini hakuna shida?
HUU uzi wapelekee Darasa la saba Ndio watakuelewa
Provinces of Burundi
  • Bubanza.
  • Bujumbura Mairie.
  • Bujumbura Rural.
  • Bururi.
  • Cankuzo.
  • Cibitoke.
  • Gitega.
  • Karuzi.
===========.====
Burundi majimbo yapo lakini chanzo cha migogoro yao hakihusiani na majimbo isipokuwa ukabila (hakuna jimbo lililosimama kupigana na jimbo lingine ila mtu kupigana na mtu mwingine).
 
Ethiopia wana matatizo toka kitambo sababu za koo zao siyo majimbo - kama majimbo yangekuwa tatizo basi nchi ya Kenya, Rwanda, South Africa, Mazambique, Lesotho, na Angola kungekuwa na vita

Shida yako ni uelewa
Nchi ulizotaja hapo ni Africa ya kusini tu ndio kidogo haina shida, hii ni kwasababu wazungu wameweka mizizi pale.
Ila zilizobaki zote zina matatizo.kwa lesotho idadi ya watu.wenyewe hawafiki hata milion4.wakigombana si wajinga!!

Kenya wana Mikoa minane.
Lakini mikoa mitatu tu ndio wanaishi kwa raha.
Lakini kulikobakia kote kunashida sio ya kawaida.
Gavana wao wa pwani msafara na ulinzi wake hata Rais akasome.

Wakati huo Tanzania yetu ina mikoa karibu 30.
Lakini inategemea mikoa mitano tu katika chakula na yote imebalance kwa upatikanaji wa chakula na bei.
Hata kwenye ulinzi wa nchi na mipaka yake mifumo ya majimbo ni shida.
Uganda ingekua na mifumo hii Josef Koni angeshamuondoa Museveni angali kijana sana.

Mfumo wa Majimbo kwa Watanzania bado. Waelimishwe kwanza hata kwa miaka 30 ijayo, halafu wapige kura wenyewe.
 
Provinces of Burundi
  • Bubanza.
  • Bujumbura Mairie.
  • Bujumbura Rural.
  • Bururi.
  • Cankuzo.
  • Cibitoke.
  • Gitega.
  • Karuzi.
===========.====
Burundi majimbo yapo lkn chanzo cha migogoro yao hakihusiani na majimbo isipokuwa ukabila (hakuna jimbo lililosimama kupigana na jimbo lingine ila mtu kupigana na mtu mwingine).
Mkuu hayo ni Majimbo au Mikoa!
Mbona Burundi ni ndogo kuliko Mkoa wa Morogoro halafu Majimbo nane
Sasa kila Jimbo Lina Mikoa mingapi?
 
Kwa sisi wenye akili huwa tunatazama USA na kwingineko kwenye serikali za majimbo kujua wamepataje mafanikio. Wewe mtumwa endelea kutazama Ethiopia moja
 
Mataifa yote yanayoendesha serikali zao kwa mfumo was majimbo ndiyo yanaongoza kwa maendekeo. Kanusha nikupe facts!
Mkuu unapoandika uwe unajaribu kidogo kutulia na kushusha pressure.
Yanini utake facts angali ulichoandika hakieleweki?
#"Was"!
#"Maendekeo"!
 
Kwa sisi wenye akili huwa tunatizama USA na kwengineko wenye serikali za majimbo kujua wamepataje mafanikio. Wewe mtumwa enedelea kutizama Ethiopia moja
Marekani ilipata uhuru mwaka 1776.
Wewe ulipata uhuru mwaka gani?

Marekani ina Rais wa 45 sasa. Wewe una Rais.wangapi tangu upate uhuru?

Akili za waafrika bado zina usokwe ndani yake.
Ndiomaana unaona mtu akipata wadhifa fulani anaona wale wa chini yake wote wajinga na hawana hakili kama yeye.

Sasa subiri mtu wa aina hiyo akabidhiwe jimbo hususani la kama Kilimanjaro halafu uone kitakachotokea.

Wewe usiangalie hizo nchi kubwa, zimefanya nn. Soma kwa makini mfumo wa mjimbo ulivyo, halafu rudisha akili kwa Watanzania uone kama wana akili ya kuongoza kwa mfumo huo.

Kisha fuatulia nchi za Afrika zenye Malighafi muhimu hasa zinazotakiwa Duniani uone kama zina Amani.
 
Mbona kwa Akina Nkurunziza hakuna majimbo na vita vya wa hutu na wa tutsi kila siku?

Namibia. Botswana. South Africa. Kenya etc kuna serikali za majimbo lakini hakuna shida?

HUU uzi wapelekee Darasa la saba Ndio watakuelewa
Hii misukule sijui huwa inaandika ikijua wasomaji ni wajinga kama wao?Umemaliza na thread ilitakiwa ifungwe baada ya hii post!
 
Mbona kwa Akina Nkurunziza hakuna majimbo na vita vya wa hutu na wa tutsi kila siku?
Namibia. Botswana. South Africa. Kenya etc kuna serikali za majimbo lakini hakuna shida?
HUU uzi wapelekee Darasa la saba Ndio watakuelewa
Huyu jamaa anafanya 'fallacy of generalisation'.

Anachukua sehemu moja kuhukumia kote kwa ubaya wake ila kunakofanya vema hapachukui kuhukumia kote kuwa ni pema.

Na huko ambapo hamna serikali ya majimbo ila kuna vita sijui atasema nini? Ni ajabu hatosema sababu ni kutokuwa na majimbo.
 
Marekani ilipata uhuru mwaka 1776.
Wewe ulipata uhuru mwaka gani?

Marekani ina rais.sasa wa 45 wew una rais.wangapi tangu upate uhuru?

Hakili za waafrika bado zina zina usokwe ndani yake.
Ndiomaana unaona mtu akipata wazifa fulani anaona wale wachini yake ote wajinga na kawana hakili kama yeye.

Sasa subili mtu wa aina hiyo akabidhiwe jimbo hususani la kama kilimanjaro halafu uone kitakachotokea.

WEWE USIANGALIE NCHI HIZO KUBWA ZIMEFANYA NINI.SOMA KWA MAKINI MFUMO WA MAJIMBO ILIVYO HALA LUDISHA AKILI ZAKO KWA WATANZANIA UONE WANAZO AKILI ZA KUIONGOZA?
KISHA FUATILIA NCHI ZA AFRIKA ZENYE MALIGAFI MUHIMU HASA ZINAZOTAKIWA DUNIANI UONE KAMA ZINAAMANI.
Kwa uandishi huo kama umesogea sana ni form 4!
 
Back
Top Bottom