kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Kwa wale wa CHADEMA iliyokataliwa na Watanzania nawashauri wafuatilie kinachoendelea Ethiopia. Sera za majimbo alizokua anazipigia chapuo Lissu ndio hizo huko Ethiopia zimesababisha serikali ya Taifa Addis Ababa kuingia vitani na Serikali ya jimbo lake la Tigray. Jimbo lina Rais lina Bunge lina jeshi lake hayo ndio Lissu anataka kutuletea.
Wakati Ethiopia wanatamani wangekua na umoja kama sisi Lissu anatamani tuwe sio kitu kimoja kama Ethiopia. Ethiopia wana majimbo kutokana na kuendekeza tofauti zao za kikabila sio kwa mapenzi ya utaifa wao.
Umajimbo ni rahisi kusambaratishwa Taifa na maadui kuliko kuwa Serikali moja imara yenye mikoa na wilaya zilizo na uwakilishi imara kwenye Serikali kuu. Hakuna kitu hatari kwa umoja wa kitaifa kama kuwa na majeshi ya kivita yanayomilikiwa na mamlaka tofauti kwenye nchi moja.