Kama huna elimu ya juu mafanikio utayasikia tu kwenye tv

Diamond platnumz wapo wangapi Tz?
 
Hao watu aina ya Diamond wako wangapi ? Acheni mzaha jamani, elimu itakuwa juu siku zote
Wako wengi mno hiyo ni mifano michache tu,elimu ni maarifa/njia ya kuyafikia mafanikio,kujitambua na uondoe ujinga ila sio kwamba kua na elimu ndio kufanikiwa

Watu wengi wenye mafanikio huku mtaani sio wasomi NIMEKUAMBIA NIPE MSOMI MWANAHABARI AU MTANGAZAJI AMBAE ANA MAFANIKIO ZAIDI YA diamond plutnumz UMESHINDWA huo ni mfano mdogo sana
 
Sijasoma elimu ya ngazi za juu ila nimeajiri waliosoma. Vice versa...
 
We uliyefika mpaka chuo una nn?
sio kufika chuo tu,nimefika hadi DUNIANI.

cv yangu kwa ufupi;-

1. ninamiliki kiwanda cha matofali,wapo vijana si chini ya 12 wanajipatia ridhiki yaan nimewaajili.

2. nina heka nyingi tu nimelima nyanya huko dakawa,mzigo unatema si kidogo .

3. ninamiliki depot mbili na nimeajili vijana 24.

huu ni mwaka wa 16 shughuli zote hzo zinajiendesha vzr.

hakuna mahala ninalipia pango zaidi ya kulipia ushuru wa serikali yaan TRA pamoja na halmashauri

miladi yote hiyo pasi kuwa na ELIMU hautoboi.

haya tuje upande wako wewe ambaye hujafika CHUO,

officen kwako hapo,hilo frem tangu umeanza,je ni la kwako au umekodi??

kwanini unaongopea wateja wako kama kweli unafurahia kutokufika kwako CHUO??
 
Wewe itakuwa unaishi vijijini hujui kinachoendelea mijini,, Asilimia kubwa ambao hawajaenda shule ndio matajiri na ndio wamewaajiri hao wasomi. Wa diploma kaajiriwa na wa darasa la 7/form 4.
Mkuu mnajidanganya,Kati ya watu kumi wanaoishi vizuri nchi hii 8 ni waliosoma,wanaotabika wakiwa na elimu ni wachache sana ukilinganisha na mamilioni ya wasio end shule wanaotabika.Ndo maana hata wewe mwanao umempeleka shule tena si ajabu kwa gharama kubwa otherwise ungemuacha akawa Kama wewe
 
Nina ofisi za ushonaji sehemu 3 nmefungua.nimeajiri vijana 30

Frem ni zangu sijakodi
Nina nyumba za kupanga room kama 10 nimekodisha

Nina bar kama 2 nasimamia mwenyew

Nanimeishia darasa la saba.una lipi lingine la kusema
 
mnaweza kunambia elimu ya bill gates na bakhresa
Mkuu Dunia hii Ina matajiri wawili tu? Mbona unawatafuta kwa tochi.Elimu ni ufunguo wa maisha ndugu acha ubishi mpeleke mtoto shule
 
Acha kuaminisha watu uwongo..wenye elimu ndo hao wanasota mtaan

Me na ufundi cherehan wangu nina mafanikio kuliko hao waliosoma
Ambao hawakusoma na wanatabika mtaani ni wengi zaidi kuliko walio Soma.Over 90%ya masikini wa Tanzania ni watu ambao hawaja soma
 
Mkuu Kati ya kumi yupo mmoja wa aina hiyo.tisa ni choka mbaya
 

Ingia mijini uone wakina nani wanachangia kodi serikalini,,,wenye maduka, mini market, supermarket na mamall, ukija kwenye matrucks ya mizigo, meli n.k asilimia kubwa ambao hawajaenda shule. Walioenda shule wanahangaika na vilaki mbili kwa mwezi hapo unategemea ataowa ai atajenga!


Kama nilivyosema hapo mwanzo, Mungu humpa amtakae, atakupa elimu kubwa na akakunyima utajiri,,,au hujaenda shule na ukatajirika/ukafanikiwa.
 
Nina ofisi za ushonaji sehemu 3 nmefungua.nimeajiri vijana 30

Frem ni zangu sijakodi
Nina nyumba za kupanga room kama 10 nimekodisha

Nina bar kama 2 nasimamia mwenyew

Nanimeishia darasa la saba.una lipi lingine la kusema
yaan unachotaka kumaanisha nikwamba umenifunga mdomo??
 
Elimu ya darasani kwa maana ya masomo siyo sababu ya mafanikio.

Tuna uchambuzi mwingi sana juu ya neno mafanikio na tuna ushahidi wa mafanikio hayo bila elimu
 
si kweli na kuna mchizi hata kuandika vizuri hajui lakini ni billionea ana nyumba ghorofa tano na magari nane
 
Hahaha Bilionea Laizer hata certificate of secondary education sizani kama anacho lkn tazama mwenzio mafanikio ni kujituma ila kutia NIA ndio kidogo kaelimu katahusika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…