Kama ingetokea watu wakamuamini Nuhu au nusu yao tu je safina ingetosha kuwabeba watu wote Dunia nzima?

Kama ingetokea watu wakamuamini Nuhu au nusu yao tu je safina ingetosha kuwabeba watu wote Dunia nzima?

"The size of the ark was such that it could have accommodated thousands more people.

Even using the larger estimate of 32,000 animals onboard, researcher John Woodmorappe postulated that there remained 6,000 tons of unused cargo space on board the ark;1 this means that 1/3 of the tonnage of the ark was unused.

Put another way, there could have been an additional 32,000 people and their necessary living space, food, and water for a year on board the ark.

Using the Ark Encounter’s estimates of ~7,000 total animals on the ark, even more space would have been available for any repentant pre-flood peoples, possibly enough space for 100,000 additional people."

ChatGPT:

"Ukubwa wa safina ulikuwa mkubwa kiasi kwamba ingeweza kuchukua maelfu zaidi ya watu.

Hata kwa kutumia makadirio ya juu ya kuwa na wanyama 32,000 ndani ya safina, mtafiti John Woodmorappe alipendekeza kuwa kulikuwa na tani 6,000 za nafasi ya mizigo ambayo haikutumika ndani ya safina; jambo hili linamaanisha kuwa 1/3 ya uzito wa mizigo wa safina haukutumika.

Kwa maneno mengine, kulikuwa na nafasi ya ziada ya kuwachukua watu 32,000 pamoja na mahitaji yao ya kuishi kama chakula na maji kwa mwaka mzima ndani ya safina.

Kwa kutumia makadirio ya Ark Encounter kuwa kulikuwa na jumla ya ~7,000 ya wanyama ndani ya safina, basi nafasi zaidi ingepatikana kwa ajili ya watu waliotubu kabla ya gharika, labda hata nafasi ya kuwachukua watu 100,000 zaidi."
 
Ungetuwekea hivyo vipimo ndugu yangu ili tuchambue kisayansi otherwise jambo lako ni la kufikirika pia.
 
Wangekubali wote, kusingekuwa na haja ya gharika.

Lakini hayo maji hayakuwa dunia nzima (biblia yenyewe inasema NCHI IKAJAA MAJI.)

Kama mahubiri yaliwalenga watu wote ulimwenguni, hakuna mahali Nuhu alisafiri hadi Australia kisha aje Afrika, Aende Ulaya yote.
Kama hayakuwa dunia nzima, kwa nini alibeba wanyama wawili wawili!? Je, wanyama hao si wangekuwepo sehemu nyingine ambako gharika haingedhuru!?
 
Mambo ya Imani ni magumu Sana, ndo maana huwezi kutumia sayansi kuyaprove, wewe amini tu kama zuzu, hivi kutoka Misri mpaka Israel ni kilomita 600 lakini wa Israel walitumia miaka arobaini kufika huko, Mimi naamini Mungu yupo Lakini vitabu vyetu walioandika wamtia chumvi au wamejipendelea sana
Inawezekana Mungu aliwapa changamoto mbalimbali ili wachelewe. Mfano kupotea njia.
 
Mambo ya Imani ni magumu Sana, ndo maana huwezi kutumia sayansi kuyaprove, wewe amini tu kama zuzu, hivi kutoka Misri mpaka Israel ni kilomita 600 lakini wa Israel walitumia miaka arobaini kufika huko,
Kizazi cha wasraeli waliotoka Misri walilaaniwa wasiingie kwenye nchi ya ahadi kwasababu ya kukosa imani kwao. Mungu aliwazungusha hapo muda wote huo ili waishe wasiingie nchi ya ahadi, watoto wao ndo wangeingia.

Simulizi lenyewe:

" Alipowatuma kwenda kuipeleleza nchi ya Kanaani, Mose aliwaambia: “Nendeni juu kule Negebu, hadi kwenye nchi ya milima,

mkaipeleleze nchi ilivyo. Chunguzeni pia kama watu wanaoishi humo ni wenye nguvu au dhaifu, wengi au wachache.

Pelelezeni kama nchi hiyo ni nzuri au mbaya, na kama miji wanamoishi ni kambi au ni nyumba zilizozungukwa na ngome.

Chunguzeni pia kama nchi yenyewe ni tajiri au maskini, ina miti au haina. Muwe na mioyo ya ujasiri na mnaporudi chukueni baadhi ya matunda ya nchi hiyo.” Hayo yalikuwa majira ya zabibu zianzapo kuiva.

Basi, watu hao wakaenda na kuipeleleza nchi toka jangwa la Sini hadi Rehobu, karibu na njia ya kuingilia Hamathi.

Walikwenda hadi Negebu wakapita mpaka mji wa Hebroni. Humo waliwakuta Waahimani, Washeshai na Watalmai, wazawa wa Anaki. (Mji wa Hebroni ulikuwa umejengwa miaka saba kabla ya mji wa Soani ulioko nchini Misri).

Walipofika katika Bonde la Eshkoli, watu hao walikata shada la mzabibu lililokuwa na matunda mengi nalo lilibebwa na watu wawili juu ya mti. Walichukua pia makomamanga kadhaa na tini.

Mahali hapo paliitwa Bonde la Eshkoli kwa sababu ya shada ambalo watu hao wa Israeli walikata kutoka mahali hapo.

Baada ya kuipeleleza nchi kwa muda wa siku arubaini, watu hao walirudi.

Waliwaendea Mose, Aroni na jumuiya ya Waisraeli huko Kadeshi, katika jangwa la Parani, wakatoa taarifa ya mambo waliyoyaona na kuwaonesha matunda ya nchi.

Walimwambia Mose, “Tuliifikia nchi uliyotutuma tuipeleleze; hiyo ni nchi inayotiririka maziwa na asali, na hili ni tunda lake.

Lakini wenyeji wake ni wenye nguvu sana, na miji yao ni imara na mikubwa sana. Zaidi ya hayo, huko tuliona wazawa wa Anaki.

Waamaleki wanakaa katika eneo la Negebu; Wahiti, Wayebusi na Waamori wanakaa katika eneo la milima, na Wakanaani wanakaa karibu na bahari ya Mediteranea na karibu na kingo za mto Yordani.”

Lakini Kalebu aliwanyamazisha watu mbele ya Mose, akasema, “Twende mara moja tukaimiliki nchi hiyo. Kwa kuwa tunao uwezo sana wa kushinda.”

Lakini watu walioandamana naye kuipeleleza nchi wakasema, “Hatutaweza kupigana na watu hao; wao wana nguvu kuliko sisi.”

Kwa hiyo wakaeneza mambo ya uongo kati ya wana wa Israeli kuhusu nchi waliyoipeleleza, wakisema, “Nchi hiyo inawaua watu wake. Pia watu wote tuliowaona huko ni wakubwa sana.

Tuliona majitu huko, wazawa wa Anaki. Sisi tulijiona kuwa kama panzi mbele yao, na ndivyo walivyotuona sisi.”
Hesabu.13.17-33.BHN

"Mwenyezi-Mungu akajibu, “Nimewasamehe kama ulivyoomba.

Lakini kwa kweli, kama niishivyo na kadiri dunia itakavyojaa utukufu wangu,

hakuna hata mmoja wao ambaye amewahi kuuona utukufu wangu na miujiza yangu niliyoifanya Misri na jangwani kisha akazidi kunijaribu mara hizi zote bila ya kutii sauti yangu,

ataiona nchi ile niliyoapa kuwapatia babu zao; kadhalika hata wale wanaonidharau pia hawataiona
.

Bali kwa sababu mtumishi wangu Kalebu ni tofauti, na amenitii kikamilifu, nitamfikisha kwenye nchi hiyo aliyoingia na wazawa wake wataimiliki.

Kwa kuwa Waamaleki na Wakanaani wanakaa katika mabonde ya nchi hiyo, kesho geukeni nyuma mwende jangwani kuelekea bahari ya Shamu.”

Mtakufa na miili yenu itatupwa humuhumu jangwani, kwa sababu mmenungunika dhidi yangu, hakuna hata mmoja wenu mwenye umri wa kuanzia miaka ishirini na zaidi,

atakayeingia katika nchi hiyo ambayo niliapa kuwapa iwe yenu, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni.

Nyinyi mlisema kuwa watoto wenu watatekwa nyara, lakini mimi nitawafikisha watoto wenu kwenye nchi mliyoidharau, ili waijue na iwe makao yao.

Lakini nyinyi, mtafia humuhumu jangwani.

Watoto wenu watatangatanga na kutaabika humu jangwani kwa muda wa miaka arubaini kwa ajili ya ukosefu wenu wa imani mpaka mtu wenu wa mwisho atakapofia jangwani.

Kutokana na makosa yenu, mtataabika kwa muda wa miaka arubaini, sawa na zile siku arubaini mlizopeleleza ile nchi, mwaka mmoja kwa kila siku moja; mtatambua kwamba mimi nimechukizwa.

Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema: Hakika nitawatenda hivyo nyinyi nyote mliokusanyika hapa kunipinga. Wote wataishia humuhumu jangwani na ni humu watakamofia.”

Hesabu.14.20-35.BHN
 
Kama hayakuwa dunia nzima, kwa nini alibeba wanyama wawili wawili!? Je, wanyama hao si wangekuwepo sehemu nyingine ambako gharika haingedhuru!?
Inahitaji tafakari ya kina zaidi kuamini kwamba samaki, chura, kasa na viumbe na mimea ya baharini nayoilikumbwa na kadhia hii. Akabeba kunguni na mbu wa kazi gani sasa
 
Maswali yatazidi kuwa mengi sana kuhusiana na story ya SAFINA YA NUHU.

Unaposoma Kitabu cha mwanzo sura ya 6,7 na 8 utaona Mungu mapema kabisa anatoa maelekezo namna gani safina itengenezwe akatoa na vipimo vile viantakiwa viwe!!

Kwa maana hiyo Mungu alikuwa anajua idadi halisi ya wanyama watakao ingia pamoja na binadamu, mbegu zote za miti na nafaka.

kifupi Mungu alijua safina itakuwa na uzito fln ndio maana alitoa vipimo

Nuhu aliingia yeye na familia yake si zaidi ya watu 10 vipi kama wangeingia watu 200 tu vipimo vingeongezwa?

Imagine dunia yote ingekubaliana na mahubiri ya Nuhu na wote wakatii na kuamini alichokuwa anakisema Nuhu je hiyo safina ingelitosha kubeba watu wote duniani pamoja na wanyama,mbegu za nafaka miti na ndege?

Pia kwa wale mnaodai wanefili ulikuwa uzao wa malaika na wanadamu (chotara) na lengo la Mungu lilikuwa kuwaangamiza wanefili wote ili kibaki kizazi og cha binadamu halisi ambaye ni Nuhu kama mnavyodai.

Je kulikuwa na ulazima gani wa Nuhu kuwahubiri na vipi kama wangemtii Nuhu na kuingia nao kwenye safina Mungu asingeiangamiza dunia kwa maji?

Kama Mungu target yake ilikuwa watu wahubiriwe kama wangeamini mahubiri hayo safina iliyotengenezwa kwa miaka 120 ingeli vunjwa?

Happy Sunday 😊

View attachment 3429246View attachment 3429248
Safina imgezama kwa kubeba chakula Cha siku Moja Cha wanyama waliostahili kibebwa....
Safina haikuwa na uwezo wa kubeba asilimia kumi ya wanyama wLiostahili kubebwa.
Mpaka sasa hakuna uwezekano wa kuwa na chombo Cha mbao Cha ukubwa wa safina.
 
Unamaanisha safina haikuwepo?
 
Maswali yatazidi kuwa mengi sana kuhusiana na story ya SAFINA YA NUHU.

Unaposoma Kitabu cha mwanzo sura ya 6,7 na 8 utaona Mungu mapema kabisa anatoa maelekezo namna gani safina itengenezwe akatoa na vipimo vile viantakiwa viwe!!

Kwa maana hiyo Mungu alikuwa anajua idadi halisi ya wanyama watakao ingia pamoja na binadamu, mbegu zote za miti na nafaka.

kifupi Mungu alijua safina itakuwa na uzito fln ndio maana alitoa vipimo

Nuhu aliingia yeye na familia yake si zaidi ya watu 10 vipi kama wangeingia watu 200 tu vipimo vingeongezwa?

Imagine dunia yote ingekubaliana na mahubiri ya Nuhu na wote wakatii na kuamini alichokuwa anakisema Nuhu je hiyo safina ingelitosha kubeba watu wote duniani pamoja na wanyama,mbegu za nafaka miti na ndege?

Pia kwa wale mnaodai wanefili ulikuwa uzao wa malaika na wanadamu (chotara) na lengo la Mungu lilikuwa kuwaangamiza wanefili wote ili kibaki kizazi og cha binadamu halisi ambaye ni Nuhu kama mnavyodai.

Je kulikuwa na ulazima gani wa Nuhu kuwahubiri na vipi kama wangemtii Nuhu na kuingia nao kwenye safina Mungu asingeiangamiza dunia kwa maji?

Kama Mungu target yake ilikuwa watu wahubiriwe kama wangeamini mahubiri hayo safina iliyotengenezwa kwa miaka 120 ingeli vunjwa?

Happy Sunday 😊

View attachment 3429246View attachment 3429248

Mungu alimuona mwenye haki mmoja Amwokoe na gharika lakini kama wangelimsikila Nuhu na kuokoka kama waninawi,Mungu angeweza kughairi gharika
 
Swali:
Kama ingetokea watu wote au nusu yao tu wangemsadiki Nuhu na kutubu, je safina ingeweza kuwabeba watu wote wa dunia ya wakati huo?

Jibu 1:

Mungu asingekuwa na sababu ya kuihukumu dunia kwa gharika kama watu wote wangetubu. Hukumu ya gharika ilitokana na uovu uliokuwa umeenea duniani kote:

"BWANA akaona ya kuwa uovu wa mwanadamu ulikuwa mwingi duniani, na kwamba kila kusudi la mawazo ya moyo wake ni baya tu siku zote."
Mwanzo 6:5 (SUV)

Ikiwa watu wengi wangesikia na kuamini ujumbe wa Nuhu, Mungu asingehitaji tena kuiangamiza dunia kwa gharika, kwa sababu lengo la adhabu lilikuwa kuondoa uovu na kuokoa haki. Nuhu aliokoka kwa kuwa alikuwa mwenye haki mbele za Mungu:

"Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu kati ya watu wa zamani zake; Nuhu alikwenda pamoja na Mungu."
Mwanzo 6:9 (SUV)

Kama watu wote wangegeuka na kuwa wenye haki kama Nuhu, basi Mungu asingeharibu dunia bali angewasamehe kama alivyofanya kwa watu wa Ninawi (Yona 3:10).

Jibu 2:
Kama hata baadhi ya watu wangetubu (nusu au wachache), bado kulikuwa na uwezekano wa kufanya marekebisho ya vipimo vya Safina au maandalizi mengine ili kuwahifadhi wote waliotubu.

Mungu alimpa Nuhu maagizo ya kina ya namna ya kujenga safina (Mwanzo 6:14-16), na kwa kuwa Nuhu alikuwa na muda wa miaka mingi kuijenga (inaaminika kuwa karibu miaka 100 kulingana na Mwanzo 5:32 na 7:6), kulikuwa na nafasi ya mabadiliko iwapo watu wangeamini. Mungu huwa hajifungi na mpango mmoja; hujibu toba:

"Lakini ikiwa mtu mwovu atatubu dhambi zake zote alizozitenda, na kuzishika amri zangu zote, na kutenda haki na haki tu, hakika ataishi, hatakufa."
Ezekieli 18:21 (SUV)

Hivyo, ingekuwa watu wengi wamesikia na kuitikia, Mungu angeweza kuagiza kupanua safina au kutoa njia nyingine ya wokovu. Hakika Mungu hapendezwi na kifo cha mtu mwovu:

"Je! Mimi napendezwa kabisa na kufa kwake mtu mwovu? asema Bwana MUNGU; sivyo, napendezwa na haya, ya kwamba amwache njia yake, akaishi?"
Ezekieli 18:23 (SUV)

Jibu 3:
Mpango wa Mungu ulikuwa ni wokovu, si maangamizi – lakini watu walikataa onyo la Nuhu.

Nuhu aliwahubiria watu kwa miaka mingi kama "mhubiri wa haki":
"... Nuhu wa haki mwenye haki, mhubiri wa haki..." - 2 Petro 2:5 (SUV)

Hii inaonyesha kuwa mpango wa Mungu ulikuwa kutoa nafasi ya toba kwa watu wote. Lakini watu walidharau onyo lake na wakaendelea na maisha yao ya kawaida hadi siku ya gharika:

"Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Kwa maana kama vile walivyokuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, wasitambue hata gharika ikaja, ikawachukua wote..."
Mathayo 24:37-39 (SUV)

Hili linathibitisha kuwa Mungu hakuwa amewakata watu; waliamua wao wenyewe kupuuza wito wa wokovu.

Jibu 4 :
Kama watu wengi wangeitikia, safina ingekuwa ishara ya neema kwa wote waliotii – si janga la maangamizi.

Safina haikuwa tu chombo cha kuokolea familia ya Nuhu, bali mfano wa wokovu kwa wote watakaotii:

"Kwa hiyo alingoja kwa uvumilivu katika siku za Nuhu, wakati safina ikitengenezwa, ambayo ndani yake wachache tu, yaani watu wanane, waliokolewa kwa maji."
1 Petro 3:20 (SUV)

Ikiwa wengine wangeingia pamoja naye, wangeokoka pia. Mungu angeweza kuokoa hata miji kama Sodoma na Gomora kwa watu wachache waliokuwa waadilifu (Mwanzo 18:23-32). Hii inaonyesha kwamba wokovu unapatikana kwa yeyote atakayeitika, si kwa chaguo la Mungu la kibaguzi.

Hitimisho:
Kama watu wote au nusu yao wangesadiki ujumbe wa Nuhu, Mungu asingeharibu dunia ile kwa gharika. Kama ni wachache tu wangetubu, bado Mungu angeweza kuruhusu upanuzi au maandalizi mengine ya safina kuokoa wote waliotii.

Hukumu ya gharika ilikuwa ni jibu kwa uovu uliokithiri na si shambulio la ghafla; Mungu alitoa nafasi ya toba kupitia mhubiri wa haki – Nuhu.

Hii inatufundisha kuwa Mungu daima huweka mbele toba kabla ya hukumu, na wokovu upo kwa wote watakaoamini.
 
Mungu alimuona mwenye haki mmoja Amwokoe na gharika lakini kama wangelimsikila Nuhu na kuokoka kama waninawi,Mungu angeweza kughairi gharika
Nini kilifanya wasimsikilize?
 
Maswali ya ufahamu na akili ni yapi Pope Leo XIV?

Nimetumia Neno kijinga kumaanisha kutokuwa na elimu ya Biblia. Nitawajibu jinsi ya kusoma Biblia na Kuielewa. Ukielewa jinsi ya kuusoma Biblia na kuitafsiri maswali mengi ya kijinga yatakwisha.
 
Back
Top Bottom