Kama jibu hili la kipuuzi alilolitoa Rais Chakwera wa Malawi ndizo akili za Wapinzani wengi Barani Afrika, ni bora Vyama Vikongwe vitutawale milele

Kwani kule jimboni kwa Mbunge mstaafu maarufu kama bwege walijibiwa nn juzi na mtu ambaye anasisitizaga maendeleo hayana chama.
Hakuna utofauti na alichojibu Chakwera

Kwahiyo Kwako Wewe Kosa 'linahalalishwa' kwa Kosa Mkuu?
 
Hii mada imekaa kishabiki!Sioni mantiki ya kuhukumu vyama pinzani africa nzima kwa makosa ya Rais wa Malawi!
 
Yote ni makosa,lakini la kutoteua waziri kutoka sehem ambayo hukupata kura linavumilika wala sio ishu, lakini kutopeleka maendeleo wakat kodi zao unachukua kwa Hoja kwamba hawakukuchagua sio haki.
Umeongea jambo kubwa sana kwa maneno machache,kama mleta mada yuko open minded ataelewa!
 
GENTAMYCINE,

Changes muhimu mkuu no matter what.

Akiboronga next election wananchi wamuweke pembeni. Namna hiyo. Hakuna mwema. Hata hivo vyama vilivotawala years and years nini wanafanya. Zero kabisa. So bora mazuzu yapokezane maisha yaendelee.
 
Changes muhimu mkuu no matter what.
Akiboronga next election wananchi wamuweke pembeni. Namna hiyo. Hakuna mwema. Hata hivo vyama vilivotawala years and years nini wanafanya. Zero kabisa. So bora mazuzu yapokezane maisha yaendelee.
Kwa hiyo awamu ya 5 hawajafanya chochote?
 
GENTAMYCINE,

Na kwa wako kupuuzia kuwa Chikwera huyohuyo amependekeza kuwa madaraka ya rais yapunguzwe, nasema ni heri mtazamo wako pia ukapuuzwa.

 
GENTAMYCINE,

..chama cha Raisi Chakwera siyo miongoni mwa vyama vya "upinzani."

..MCP, chama cha Raisi Chakwera, ni chama KIKONGWE cha Malawi ambacho kimerejea madarakani.

..itapendeza kama utarekebisha post yako ili iendane vizuri na ukweli kwamba MCP ni moja ya vyama VIKONGWE barani Afrika.
 
GENTAMYCINE,

Kuna kosa gani kwa jirani mpya kumwiga jirani yake mkongwe? Nje ya Afrika ya Mashariki nchi aliyotembelea Rais wetu mpendwa mapema ni Malawi ikiongozwa na Rais mtangulizi wa huyu aliyopo madarakani sasa. Rais wetu mpendwa yuko madarakani miaka 5 na kabla ya hapo alikuwa Waziri miaka 20 uzoefu wa kuigwa na mtu yeyote mpya mwenye akili timamu.

Mpendwa wetu nafasi nyeti zote za kazi za uteuzi wamepewa ndugu, au rafiki, au wapenzi, au Wasukuma, au wa Kanda ile nk na nchi imepata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na madege yamenunuliwa, MW 2115 umeme wa Stiegler's Gorge, treni za umeme 100 mph, Chato International Airport, Burigi National Park, maflyover lukuki nk nk. Rais wetu ni Mwenyekiti wa CCM Chama tawala na unamkubali na Chama chenu pia ungependa kiongoze milele lakini unakerwa na Rais wa Malawi kuiga uteuzi labda na kutengua. Hueleweki, lazima uwe mjinga wa kutupwa!
 
Waafrika tuko hivyo, huyu hana tofauti na yule mh aliyefika bukoba wakamueleza suala la stendi akawajibu "mlichagua vibaya". Pia kauli hii haitofautiani sana na ile ya iliyotolewa juu ya wananchi wa mh Bwege...endeleeni na bwege wenu.....siasa hizi jamani.
 
Umesahau kwa Magufuli, Kimara walivunjiwa nyumba kwa vile hawakumpigia kura za ushindi! Ni lini ulisikia Magufuli anateua kutoka mikoa ya Kaskazini?
 
Huyo ni Magufuli wa Malawi, maana hata chama chake ni kikongwe sana.
 
GENTAMYCINE,

Vyama vikongwe ni adui ya Demokrasia ya kweli.

Huyo wa Malawi awamu yake itakua ni moja tuu. Na wataendelea kuchagua mpaka watampata atakayewaunganusha na hapo watakwenda mbele kwa kasi na nchi yao itadumisha amani.

Waafrika umaskini na Elimu ya mkoloni ndiyo inayowafanya watu kuwaza madaraka tu badala ya kutumia rasilimali na utajiri mkubwa tuliopewa na Mungu Kwa kujitawala na kujiajiri na kuishi kwa Uhuru na amani.

Lakini pia watu wanapenda madaraka kwa sababu magereza zetu bado hazijapata wafungwa waliokuwa wametawala kwa dhulma na wizi na ubadhirifu wa Mali za umma.

Madaraka imekuwa ni sehemu ya kujilimbikizia Mali kwa haraka haraka bila kuulizwa.

Hatuna Sheria Kali za kuwadhibiti viongozi wa umma wanapopora rasilimali zetu. Watawala ni ndio mabeberu wa karne hii kwa sheria za kibeberu. MTU anateuliwa kuwa Waziri ndani ya mwaka mmoja namiliki Mali ambazo mfanyakazi aliyetumikia nchi kwa miaka 40 hana hata 1/10 ya Mali hizo.

Tatizo ni sheria na katiba dhaifu zisizokuwa na maadili ya uongozi

Lakini pia kuwaweka ndugu sio tatizo tatizo ni ,Je, hao ndugu wanatenda Haki?

Sio kuweka ndugu wanaokula bata tu na kunyanyasa watu? Ndugu wanaoteka watu na kuua watu na kutisha watu ili kulinda himaya ya kaka au Dada yao, ndugu wanaoishi kwa propaganda na kuzuia watu kuikosoa serikali . Ndugu wanaominya na kugandamiza Uhuru wa watu wengine hawafai. Lakini hata wasio ndugu wanaweza wakafanya vibaya kama hawafuati sheria.

Nchi inaweza ikatawaliwa na mtu asiyekuwa hata wa asili ya nchi hiyo kama alivyokuwa Obama lakini kwa Afrika ni ngumu kidogo mana Ukabila bado upo hata kwa vyama vikongwe.

Huyo Rais wa Malawi angeweza kuudanganya ulimwengu kwa kukanusha lakini amekua muawazi kutokana na Uhuru wa nchi yake wa kuweka takwimu sawa

Kuna nchi pia ambazo wakati wa Uhuru kura nyingi zilikuwa za dini Fulani iliyowapinga sana wakoloni lakini baada ya kuingia madarakani walioteuliwa wakawa ni wale wale walioungana na kwa sehemu ya wakoloni. Hapo ikawa ndio mwanzo wa kuwa na wazungu weusi tii wanaotawala na kuendekeza mila,desturi ,elimu na sheria za kikoloni.

Your browser is not able to display this video.
 
Hii hawawezi kuiongelea katu, wote ni walewale.
Kama ni kwel huyo rais wa Malawi ana tofauti gani na Jpm eg rejea kauli aliyotoa kwa wananchi wa kilwa akirudi kutoka mtwara kuhusu bwege
 
We jamaa Haya mambo huyajui for your information chama Tawala malawi kwa sasa ndio chama kikongwe malawi huwezi kufananisha na CDM au NCCR kwani hivi havijawahi kuwa madarakani.
 
Umesahau kwa Magufuli, Kimara walivunjiwa nyumba kwa vile hawakumpigia kura za ushindi! Ni lini ulisikia Magufuli anateua kutoka mikoa ya Kaskazini?
Nilidhani wewe utakuwa na majibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…