GENTAMYCINE,
Vyama vikongwe ni adui ya Demokrasia ya kweli.
Huyo wa Malawi awamu yake itakua ni moja tuu. Na wataendelea kuchagua mpaka watampata atakayewaunganusha na hapo watakwenda mbele kwa kasi na nchi yao itadumisha amani.
Waafrika umaskini na Elimu ya mkoloni ndiyo inayowafanya watu kuwaza madaraka tu badala ya kutumia rasilimali na utajiri mkubwa tuliopewa na Mungu Kwa kujitawala na kujiajiri na kuishi kwa Uhuru na amani.
Lakini pia watu wanapenda madaraka kwa sababu magereza zetu bado hazijapata wafungwa waliokuwa wametawala kwa dhulma na wizi na ubadhirifu wa Mali za umma.
Madaraka imekuwa ni sehemu ya kujilimbikizia Mali kwa haraka haraka bila kuulizwa.
Hatuna Sheria Kali za kuwadhibiti viongozi wa umma wanapopora rasilimali zetu. Watawala ni ndio mabeberu wa karne hii kwa sheria za kibeberu. MTU anateuliwa kuwa Waziri ndani ya mwaka mmoja namiliki Mali ambazo mfanyakazi aliyetumikia nchi kwa miaka 40 hana hata 1/10 ya Mali hizo.
Tatizo ni sheria na katiba dhaifu zisizokuwa na maadili ya uongozi
Lakini pia kuwaweka ndugu sio tatizo tatizo ni ,Je, hao ndugu wanatenda Haki?
Sio kuweka ndugu wanaokula bata tu na kunyanyasa watu? Ndugu wanaoteka watu na kuua watu na kutisha watu ili kulinda himaya ya kaka au Dada yao, ndugu wanaoishi kwa propaganda na kuzuia watu kuikosoa serikali . Ndugu wanaominya na kugandamiza Uhuru wa watu wengine hawafai. Lakini hata wasio ndugu wanaweza wakafanya vibaya kama hawafuati sheria.
Nchi inaweza ikatawaliwa na mtu asiyekuwa hata wa asili ya nchi hiyo kama alivyokuwa Obama lakini kwa Afrika ni ngumu kidogo mana Ukabila bado upo hata kwa vyama vikongwe.
Huyo Rais wa Malawi angeweza kuudanganya ulimwengu kwa kukanusha lakini amekua muawazi kutokana na Uhuru wa nchi yake wa kuweka takwimu sawa
Kuna nchi pia ambazo wakati wa Uhuru kura nyingi zilikuwa za dini Fulani iliyowapinga sana wakoloni lakini baada ya kuingia madarakani walioteuliwa wakawa ni wale wale walioungana na kwa sehemu ya wakoloni. Hapo ikawa ndio mwanzo wa kuwa na wazungu weusi tii wanaotawala na kuendekeza mila,desturi ,elimu na sheria za kikoloni.