Kama Kazi ya Uenezi imemshinda Paul Christian Makonda nani ataiweza?

Kama Kazi ya Uenezi imemshinda Paul Christian Makonda nani ataiweza?

Bush Dokta

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2023
Posts
24,831
Reaction score
45,154
Wazungu wanasema the Bone that Failed the Heyna, who can?

Kazi ya Uenezi ndani ya ccm aliyeiweza kwa ufasaha alikuwa Abdulrahman Kinana miaka ya 2010.

Tangu hapo Chama cha Mapinzudi hakijawahi kupata mtu sahihi, hata walipojaribu kuteua watu wenye dosali ktk jamii bado napo imekuwa ngumu kufikia mafanikio wayatakayo.

Inaskitisha kuwa ndani ya miaka mitano tu tayari nafasi hiyo imeshikwa na Viongozi zaidi ya wa nne.

Hii maana yake ni nini? Kutapa tapa?

Alianza Hamphrey Polepole, Shaka Abdul Shaka na baadae Mjema kabla ya Paul Makonda.

Kama hawa wote hawakideliver Results je nani anaweza ktk mazingira ya namna hii.

Pole sana Ndugu Mwenezi Mpya, nakupa pole kwa sababu una kazi ngumu sana ya Kuperform zaidi ya Paul Makonda.

Kazi ambayo sioni kama utatoboa, Expectation za Chama chako ni kubwa kuliko uhalisia.

Changa vizuri karata zako lakini ujiandae kwa lolote.

Mfupa uliomshinda Fisi nani atauweza?
 
20240209_095750.jpg

Kwa matumizi haya mabovu ya pesa bora Bashite alivyopigwa chini
 
Ukiwapima kikazi kati ya makonda vs makalla, utagundua makalla ni mwepesi sana, makonda jitu la kazi wengine wote hamna kitu. Akishindwa paul siamini kama kuna mwengine ataiwezea hiyo shughuli
 
ukiwapima kikazi kati ya makonda vs makalla, utagundua makalla ni mwepesi sana, makonda jitu la kazi wengine wote hamna kitu. Akishindwa paul siamini kama kuna mwengine ataiwezea hiyo shughuli
Kwani Mh Unadhani Paul amefeli wapi?
 
Mmh? Mkakati upi? Gambo si alikuwepo? Nini kimeshindikana?
kuna wakati ccm huwa sielewi mkuu, ila Paul mimi mwenyewe niliweka imani kubwa sana...inawezekana uongozini kuna makundi...watu (baadhi ya viongozi kichama)hawapendi kuona Paul anapewa sifa binafsi na wananchi na makundi mengine mbalimbali...wana wivu wanaamua kumfanyia figisu. Ila naamini Paul ana kibali mbele za Mungu na mbele za watu... ni ngumu sana kumshusha mtu huyu
 
Makonda alifeli pakubwa. Makalla asifanye mbwembwe za kitoto kama za Makonda ambaye alikuwa anaendeshwa na hulka za kishamba kama ilivyo kawaida kwa watu wa kanda ile.
 
kuna wakati ccm huwa sielewi mkuu, ila Paul mimi mwenyewe niliweka imani kubwa sana...inawezekana uongozini kuna makundi...watu (baadhi ya viongozi kichama)hawapendi kuona Paul anapewa sifa binafsi na wananchi na makundi mengine mbalimbali...wana wivu wanaamua kumfanyia figisu. Ila naamini Paul ana kibali mbele za Mungu na mbele za watu... ni ngumu sana kumshusha mtu huyu
Paul ana dosari nyingi sana. Ni rahisi kutiliwa mashaka
 
Back
Top Bottom