Kama Kazi ya Uenezi imemshinda Paul Christian Makonda nani ataiweza?

Sio kama kazi ilimshinda, ila amewekwa mahali pa utawala zaidi, muwakilishi wa mama.
 
Maza Aliambiwa Makonda atakuja kugombea Urais ,Maza anaogopa utadhani atatawala milele
 
Usinishangae mimi maana mimi naamini Makonda alikuwa sahihi lakini Haikukubalika kwa wazito na haiwezi kukubalika ile style kwa sababu itaonekana wanamfuata yule Jamaa na style zake zilivyokuwa za Uongozi !
 
CCM NI SIKIO LA KUFA.Ndio maana inatapatapa kila kukicha.wala hawajui cha kufanya.
 
kabla ya march 2025 atachaguliwa tena mwingine,ndani ya ccm uenezi sasa hivi ni mwaka mojamoja, kila mtu apitie kuongeza cv,kama wamemkosa mtu sahihi waache tu wazi hiyo nafasi ukizingatia takriban miaka 48 ya utawala wao watakuwa na lipi jipya la kueneza
 
Siku hizi hawafanyi uenezi, itikadi wala mafunzo; bali ni kusikiliza kero na kudhalilisha watumishi wa umma!
 
Nani anajua nafasi hiyo ya uenezi katika chama malipo yake yapoje
 
kabla ya march 2025 atachaguliwa tena mwingine
Nani anajua nafasi hiyo ya uenezi katika chama malipo yake yapoje
kitengo cha propaganda kina ulaji tu mzuri,ujue kutengeneza fitina
 
Kigezo kikubwa katika nafasi hii ni laizma mtu uwe na mvuto mkubwa wa kisiasa makonda alifaa
 
Wewe huna kibali machoni pa Mungu!! Mafanikio mnayoyataja ya Makonda ni kuita watu kusikiliza kero zao na kuwaambia wasijaribu mahakamani,huko ni kwa ya wenye pesa tu!! Ccm imeunda serikali yenyewe pamoja na mahakama na jeshi la polisi. Vyombo hivi ndivyo vinalalamikiwa sana, na ukiangalia unagundua ccm ndiyo chanzo cha ufanisi mdogo wa vyombo hivyo na hasa kwa kuviingiza kwenye siasa.
Huyu mwenezi nadhani kitu cha maana ilikuwa ni kukishauri chama chake kuona kinaboreshaje hizo taasisi zake zifanye kazi kwa weredi,wewe unashauri wananchi wasipeleke matatizo yao huko.
Labda kwa vile naye alikuwa mmoja wa waharibifu alipovamia clouds na hao hao na bado akawa salama. Ninapata shaka kuwepo kwa kundi kubwa la wajinga nchi hii ndio kinamuona Makonda ni malaika wao. Mnaambiwa kila siku jengeni taasisi imara, hamsikii. Huko Marekani wangekuwa na taasisi dhaifu watu kama kina Trump wangeguswa!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…