Kama Kifo ni mpango wa Mungu basi Mungu wenu atakuwa katili sana, mnawezaje kuwa nae?

Kama Kifo ni mpango wa Mungu basi Mungu wenu atakuwa katili sana, mnawezaje kuwa nae?

​


ume-skip swali langu now umeingia kwenye fallacy ya Straw Man Argument

Swali langu ni hili

unakuaje na hakika katika vitu unavyotumainia?

unakuaje na hakika na vitu ambavyo hujavifikiri?
Nimekujibu. Maelezo yangu yamejikita kwenye tofauti ya faith na critical thinking na maswali niliyokuuliza yanatilia mkazo. Ukijibu hayo maswali utapata majibu yako.
 
Nimekwambia kifo hakihusiani na aina ya ulimwengu,sasa sijui unakwama wapi kung'ang'ania kuhusisha ulimwengu na kifo.
Mimi nakuuliza baba yako alishindwa kujenga nyumba ambayo haiwezi kupata ufa?

Unanijibu nyufa hazihusiani na aina ya nyumba.

Totally off point.

Whether nyufa zinahusina na aina ya nyumba au hazihusiani na aina ya nyumba, swali liko pale pale.

Baba yako alishindwa kujenga nyumba ambayo haiwezi kupata ufa?

Usikimbie swali kwa objections zilizo off point.

Mungu wako alishindwa kuumba ulimwengu ambao kifo hakiwezekani kuwepo wala kufikirika?

Hujajibu swali hili.
 
MUNGU si wakala wa Vifo Kifo ni matokeo ya uchaguzi kama vile Uzima ulivyo ni Matokeo ya Uchaguzi.Matokeo ya Uchaguzi kwa nani?Kifo ni matokeo ya Uchaguzi wa Uasi kwa Kile alichosema Mungu.Uzima ni Matokeo ya Utii wa Kile alichoagiza Mungu.Shetani ndiye Muasisi wa Kifo kama matokeo ya uongo aliowalisha wazazi wa kwanza Adam na Hawa Katika Bustani ya Eden Sura ya kwanza na ya pili ya Kitabu Cha Mwanzo inaeleza Asili na Chimbuko la kifo cha wote wenye mwili.Ukipata muda soma hizo sura.Kifo ni matokeo Ya uasi wa sheria na maagizo ya mwenyezi Mungu.Mungu hajakusudia kuona watu wakifa na anazo nguvu juu ya Mauti na Kaburi Na hivyo ameahidi urejeshwaji wa Uzima wa mwili na Maisha ya milele kwa wote wale Watakaokubali na kumwamini Yeye Aliyetumwa na Yeye basi japo atakufa lakini siku ya Kiyama atamfufua na kumvisha mwili usioharibika na Asione kifo tena.
Mungu wako alishindwa kuumba ulimwengu ambao kifo hakiwezekani kuwepo wala kufikirika?

Hujajibu swali hili.
 
Hivi Mungu angetaka dikteta kiasi hicho unafikiri leo hii ungekuepo?...yeye hakutaka kumpangia mtu maamuzi yake aliwaachia wawe huru kuamua jema lipi na baya lipi. Ila badae atakapofanya maamuzi ya kuondoa waovu msije sema ooh mi sikujua...ooh mi sikuambiwa

Usirudie habari ambazo tumezijadili hapa kwa lengo la kukwepa maswali

habari za mungu kua dikteta tumezipita, Mungu asingekua dikteta asinge angamiza watoto wa kwanza wasio na hatia kwenye familia za wa misri kwa lengo la kumkomoa farao

hujajibu swali

kwa hiyo upeo wa mungu uliishia kumuona shetani akiwa malaika tu haukuweza kumuonesha extra miles kua atakuja ku change?
 
Thibitisha kwamba hayupo.
Kisichopo unakithibitishaje kwamba hakipo outside of abstract logic?

Unaweza kuthibitisha Shokolokokangoshee Masalakulangwa, mtu mwenye macho matatu na miguu nane, si rais halisi wa Tanzania, aliyejificha Ikulu, na Magufuli ni msukule wake tu?

Mungu wa Biblia na Quran, na Mungu yeyote mwenye sifa za kujua yote, kuweza yote na kuwa na upendo wote, hayupo, kwa sababu ulimwengu uliopo unam contradict.

The problem of evil contradicts the existence of that God.

Do you understand that?
 
Mungu angekuwa na maamuzi ya haraka bila huruma hata ww unavokufuru hapa angeshakutoa tayari, lakini anakuacha akijua ipo siku utarudiwa na fahamu na kutubu
Sa si bora hata angekua anamaamuzi ya haraka ambayo yangefanyika kwa weledi bila errors kuliko ukurupukaji ambao hata yeye kuna muda unafika anajilaumu na kujutia
 
Mtu mbaya haexist katika dunia ya Mungu huondolewa mara moja achana na dunia hii gombania goli ya shetani..ko unauhuru wa kufanya unachotaka ndiyo ila mahali ndo utakosa maan kwa Mungu hakuna ubaya.
kwenye uhuru wa kweli hakuna neno "isipokua"

kwa maana hiyo mtu mbaya hana uhuru wa kuchagua kuendelea kubaki?
 
Hivi Mungu angetaka dikteta kiasi hicho unafikiri leo hii ungekuepo?...yeye hakutaka kumpangia mtu maamuzi yake aliwaachia wawe huru kuamua jema lipi na baya lipi. Ila badae atakapofanya maamuzi ya kuondoa waovu msije sema ooh mi sikujua...ooh mi sikuambiwa
Unakataa kuwa Mungu sio dikteta. Je unao uthibitisho ama ushahidi wa kuwa Mungu alikupa nafasi ya kuchagua kati ya kukuleta duniani ama kutokuuleta duniani (kuumbwa ama kutokuumbwa?
 
Mungu hakupangii braza usikariri mafundisho ya kitaa Mungu anapanga kila ki2..Ubaya ni wewe unaechagua ila yeye anakujua kuwa umechagua ubaya na anakupa nafasi ujione ulivoamua kuchagua mabaya ili ukipata adhabu usilaumu..hakuna mtu anapelekwa kwenye dhambi na Mungu. Leo hii mtu unaishi sio jambazi hauui watu. Je, jambazi anapaswa kulalamika kuwa kaonewa kupelekwa kwenye ujambazi? Mungu angekuwa anamfundisha m2 ubaya kusingekuwa na haja ya kuleta maandiko matakatifu. Kitu unachotakiwa kujua ni kuwa dunia inaexist sio Mungu aprove point kwako wewe nd prove point kwake..Ndo maan bible inasema mtu mbaya anapewa mafanikio sometimes aendelee na ubaya wake...hyo statement inatuonesh nn? kwamba binadam anachagua ubaya na Mungu anaeza muachia mazingira ya ubaya wake.
kwa hiyo ephesians ni mafundisho ya kitaa?

Ephesians 1:11​

All things are done according to God's plan and decision; and God chose us to be his own people in union with Christ because of his own purpose, based on what he had decided from the very beginning.
 
Mungu sio wa uhuru tu pia ni wa haki ukimtenda ndugu yako jambo baya. Je, wafanya haki?
kwa maana hiyo mungu hawezi ku manage uhuru bila mipaka?

Na mungu akimtendea ndugu yako jambo baya atakua amefanya haki?
 
Ambacho hujaelewa hapo ni kipi? Uliezaje kumsikiliza shetani kuliko mtu anaekulisha na kukuvisha unadhani una tofauti nae Mpaka unataka asingeumbwa ila wewe na ukaidi wako ndo ungeumbwa..Kma unataka shetani muhasi asiwepo nawewe usingekuwepo vile vile. Mnachotofautiana wewe na shetani ni Muda wa neema ya Mungu 2. yeye yakwake ilishaisha.. Ndo maan mtu atakaefanya dhambi mpaka siku ya mwisho atachomwa pamoja nae. N.B naposema wewe simaanishi wewe kama wewe kuwa nakuhukumu nakuterm wewe kama binadamu kama nilivo mimi ili upate picha halisi tu.
unaweza kunionesha wapi nimesema nataka shetani asiwepo?
 
Thibitisha kwamba hayupo.
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote hayupo.

Angekuwepo, asingeumba ulimwengu ambao unaruhusu vifo, magonjwa, matetemeko ya ardhi, ma tsunami, vita, magonjwa na mabaya mengi kama hayo.

Kuwepo kwa mabaya hayo kunaonesha Mungu huyo hayupo.

Mungu huyo kuwepo na ulimwengu kuwa na mabaya hayo, ni contradiction.

Umeelewa?

Wewe unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
 
Are you sure hawakuwa na hatia? Mungu nnae mwamini ni Mungu wa haki hivo hawezi ua mtu asie na hatia hata siku moja. Au we unadhan aliposem watoto wa farao alimaanisha watoto wachanga? Farao alikuwa mtu mzima maan yeye ndo aliemlea Mussa..Mbona kuna watoto wa watumish wengine wengi 2 walilaaniwa kwasbabu ayubu alikuwa mtu wa Mungu ko wote ndugu zake walikuwa watu wa Mungu. Lakini hayo yote yalikuja kutoweka baada ya haki ya kweli kuja kuishi duniani nae ni YESU kristo maan alitufia kwa dhambi zetu sahivi hakuna kifo cha dhambi cha duniani anacholeta Mungu ila kifo kitakuwa mbinguni.
kwa hiyo mimi nikiua mtu mwenye hatia sio dhambi?

exodus 12
And it came to pass, that at midnight the LORD smote all the firstborn in the land of Egypt, from the firstborn of Pharaoh that sat on his throne unto the firstborn of the captive that was in the dungeon; and all the firstborn of cattle.
At midnight, God killed all the firstborn children (and cattle [4]) in Egypt.
30 And Pharaoh rose up in the night, he, and all his servants, and all the Egyptians; and there was a great cry in Egypt; for there was not a house where there was not one dead.

mungu hakuua watoto wa farao tu bali ilikua watoto wote wa uzao wa kwanza nchi nzima walikufa, kwa hiyo kama kulikua na familia ambayo ilikua imetoka kupata mtoto wa kwanza miezi miwili iliyopita basi mtoto huyo alipatwa na mauti

Na hapo ukiangalia ilikua sio watu tu hata wanyama ambao kimsingi ni ngumu kumtetea mungu kwamba wanyama walifanya dhambi hivyo hukumu ya kifo walistahili
 
Ok pole Mkuu nilikuwa sijaelewa Mentality yako wakati nakujibu hapo juu; Nia yangu si kubishana, nilikuwa nakujibu kitu ambacho ulisema Mungu anaua; Ndio nikakwambia Kwamba usomaji Mbaya ndio unapelekea shida za Kum-attribute Mungu; Sasa naona kama wewe unataka Kubishana; Niwie radhi kama nimekukwaza.

Lakini tu kitu ninachokwambia ni kwamba, Bible iliandikwa na watu, na Ukisoma Bible in Comprenhensive way hutaona Mikanganyo ya Tabia za Mungu.
kwamba mtu asiyebishana ni yule anayekubali kila kitu?

mimi nimeweka hoja tena kwa reference kabisa we kama una hoja defensively ya ku disprove unashindwa nini hapa kuiweka watu wote wakajifunza?

au unafikiria huu ni mjadala ambao unasomwa na wachangiaji tu? umesahau kuna wasomaji wengi wanapita kujifunza wengine hawana uanachama na hii site wanatembelea tu kujifunza

Nani asiyejua kwamba Dhana ya kusema "usomaji mbaya" pale ambapo dosari imejionesha ni weapon inayotumika kuficha weakness ya vitabu vya dini?

basi naomba unitafsirie hii Exodus 12:29-30 kwa namna ya usomaji mzuri tuone kama kweli nilichokisoma mimi ni tofauti na kilichoandikwa na kumaanisha
 
Nimekujibu. Maelezo yangu yamejikita kwenye tofauti ya faith na critical thinking na maswali niliyokuuliza yanatilia mkazo. Ukijibu hayo maswali utapata majibu yako.
hapana hujajibu

ulipotoa maana ya imani ulisema imani ni kuwa na hakika na vitu uvitumainiavyo

mpaka hapo tayari ni contradiction, kwamba ukiwa na uhakika maana uko katika hitimisho ambalo lishakua verified na linathibitishika.

Na vitu vitumainiwavyo ni vitu ambavyo havithibitishiki wala kuhakikiwa, ni vitu ambavyo vinategemewa/vinatarajiwa/kufanyika/kutokea katika siku za mbele, kwa maana hiyo kuna uwezekano mkubwa vitu hivi vikaenda vice versa na ulivyotarajia

sasa uliposema kua na imani ni kuwa na hakika na vitu uvitumainiavyo umeniacha njia panda, inawezekana vipi ukawa na hakika katika kitu ambacho hujakithibitisha wala kukihakiki wala huna ushahidi nacho?
 
hapana hujajibu

ulipotoa maana ya imani ulisema imani ni kuwa na hakika na vitu uvitumainiavyo

mpaka hapo tayari ni contradiction, kwamba ukiwa na uhakika maana uko katika hitimisho ambalo lishakua verified na linathibitishika.

Na vitu vitumainiwavyo ni vitu ambavyo havithibitishiki wala kuhakikiwa, ni vitu ambavyo vinategemewa/vinatarajiwa/kufanyika/kutokea katika siku za mbele, kwa maana hiyo kuna uwezekano mkubwa vitu hivi vikaenda vice versa na ulivyotarajia

sasa uliposema kua na imani ni kuwa na hakika na vitu uvitumainiavyo umeniacha njia panda, inawezekana vipi ukawa na hakika katika kitu ambacho hujakithibitisha wala kukihakiki wala huna ushahidi nacho?
Imani haina uthibitisho. Unaweza kuamini na isiwe kama ulivyoamini. Ukishakithibitisha, ukakihakiki na ukawa na ushahidi sio imani tena ni uhalisia.
 
Imani haina uthibitisho. Unaweza kuamini na isiwe kama ulivyoamini. Ukishakithibitisha, ukakihakiki na ukawa na ushahidi sio imani tena ni uhalisia.
Sasa unakuaje na uhakika katika vitu ambavyo hujavithibitisha?
 
Back
Top Bottom