Hujajibu nilichouliza. Unarukaruka tu.
Mungu Anajua kila kitu na habanwi na muda. Hata wakati anamuumba huyo malaika aliyekwenda kinyume alijua kila kitu. Kwamba huyo malaika atakuja kuasi na kuwa shetani atakayetusumbua na kutuletea dhambi. Kwa nini Alimuumba pamoja na kujua kuwa huyo kiumbe atakuja kutuletea, dhambi, kifo na hata moto wa milele?
Unaielewa dhana ya pre-determinism? Kwamba Mungu Anajua kama utakwenda motoni au mbinguni hata kabla hujazaliwa. Kwamba Alikufahamu hata kabla hujaumbwa tumboni mwa mama yako. Kwamba kuna watu ufalme wa Mungu umeandaliwa kwa ajili yao hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.
Mimi naamini Mungu yupo na ndiye Aliyeumba kila kitu kwa sababu haiwezekani universe hii iwe hivi ilivyo fine-tuned kwa bahati tu ila maswali hayo juu huwa yananitatiza sana. Hata wewe kama huna majibu jikalie kimya tu kuliko kuendelea kubwabwaja yale yale huku ukiukwepa mhimili wa hoja yenyewe. Na haya ni masuala ya muda mrefu hayajaanza leo!