Kama Kifo ni mpango wa Mungu basi Mungu wenu atakuwa katili sana, mnawezaje kuwa nae?

Mungu mwenye kuweza kila kitu anashindwaje kutufanya tuweze kuuona ukuu wake na kumtukuza bila ya kupitia uwepo wa shetani?
Hivi ni kwanini kila nchi ina sheria? Kwani hatuwezi kuishi hivi hivi bila sheria?
 
Usifananishe ukuu wa Mungu na nchi.Mungu anaweza kila kitu ila nchi haiwezi kila kitu.Mungu ana uwezo wa kufanya watu watii sheria bila shuruti lakini nchi haina uwezo wa kufanya watu watii sheria bila shuruti.Unafananisha vitu viwili ambavyo ni tofauti kabisa!
 
Adam alikua na umri gani wakati wanahasi?
Adam kwa Mungu ni mtoto mdogo kwa sababu hana uwezo kama Mungu.Hata vitabu vitakatifu vinasema wazi kabisa kuwa sisi ni watoto wa Mungu.Sisi kwa Mungu ni watoto kwa sababu hatuna uwezo wote kama Mungu.Sisi kwa Mungu ni sawa tu na watoto wadogo waliovaa pampasi!
 
we unasomaga vitabu vya dini kweli hujui chanzo cha dhambi ? sisi wenyewe ndo tulio tengeneza dhambi katika bustani ya eden kwa kula tunda ambalo alisema mungu tusilile adam na hawa /eva sasa unaniulizaje hilo swali mkuu weka hoja yenye mashiko boss
Mungu mwenye upendo sana,huruma sana na mwenye uwezo wa kufanya kila kitu alishindwa vipi kumzuia binadamu asile hilo tunda?Upendo wake uko wapi?Huruma yake iko wapi?Uwezo wake uliotukuka uko wapi?
 
huo n mtazamo wako na c wa fulani pengine mwingine angewaza nje na hilo ulilo uliza .
jibu n ivi chanzo cha dhambi ndo kulileta hayo mabayo yote ambayo huyapendi coz binadam hatujaumbwa kwa bahati mbaya tungekuwa wasafi tungefutiwa zote mabaya na kuishi pasina maswali na hofu ama shaka mioyoni mwetu
Mungu tunaehubiriwa kuwa ana upendo sana,ana huruma sana na anaweza kila kitu alishindwa vipi kumuumba binadamu ambae ni msafi?Alishindwa vipi kuzuia vyanzo vya dhambi?Huo upendo wake uko wapi sasa?Hiyo huruma yake iko wapi sasa?Hizo nguvu zake za kuweza kufanya kila kitu ziko wapi sasa?
 
Acha kumkufulu Mungu!!!.
Kwahiyo wewe ulitaka kwamba unapochafuka akuoshe wakati huo umepewa Uwezo Wa kufanya jambo/mambo
Lakini pia Mungu wetu anaDeal na Moyo wako
 
Hujajibu nilichouliza. Unarukaruka tu.

Mungu Anajua kila kitu na habanwi na muda. Hata wakati anamuumba huyo malaika aliyekwenda kinyume alijua kila kitu. Kwamba huyo malaika atakuja kuasi na kuwa shetani atakayetusumbua na kutuletea dhambi. Kwa nini Alimuumba pamoja na kujua kuwa huyo kiumbe atakuja kutuletea, dhambi, kifo na hata moto wa milele?

Unaielewa dhana ya pre-determinism? Kwamba Mungu Anajua kama utakwenda motoni au mbinguni hata kabla hujazaliwa. Kwamba Alikufahamu hata kabla hujaumbwa tumboni mwa mama yako. Kwamba kuna watu ufalme wa Mungu umeandaliwa kwa ajili yao hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.

Mimi naamini Mungu yupo na ndiye Aliyeumba kila kitu kwa sababu haiwezekani universe hii iwe hivi ilivyo fine-tuned kwa bahati tu ila maswali hayo juu huwa yananitatiza sana. Hata wewe kama huna majibu jikalie kimya tu kuliko kuendelea kubwabwaja yale yale huku ukiukwepa mhimili wa hoja yenyewe. Na haya ni masuala ya muda mrefu hayajaanza leo!
Boss Mungu sio dikteta,amewapa uhuru viumbe wote wenye akili na dhamiri,hampangii mtu jinsi ya kuishi wala hataki kukibana kiumbe chochote kuwa ni lazma wamuabudu au kufuata sheria yake. Uhuru ambao viumbe wamepewa ndio wameutumia vibaya na kujifanya wajuaji ndio maana unaona matatizo haya. Lakini ipo siku ataondoa uovu wote na kuacha watu safi wenye adili
 
Kuhasi kwa shetani halikua lengo lake, kusudi lake ni kuumba,matokea baada ya kuumba angejua jinsi ya kupambana nayo
Ina maana alipokuwa anamuumba huyo malaika hakujua kuwa atakuja kuasi na kuwa shetani atakayetuingiza dhambini, kifo na hatimaye kututenga naye Baba yetu muumba? Alijua hakujua? Jibu hili swali kwa ndiyo/hapana mengine yote puuzia !!!
 
Mungu mwenye upendo sana,huruma sana na mwenye uwezo wa kufanya kila kitu alishindwa vipi kumzuia binadamu asile hilo tunda?Upendo wake uko wapi?Huruma yake iko wapi?Uwezo wake uliotukuka uko wapi?
Udogo wako kwa Mungu hujajua baya na zuri?
 
Kwa nini Mungu ninaehubiriwa kuwa ana upendo na huruma sana anitege na kunipa mitihani ya kuchagua baya na zuri wakati ana uwezo wa kunifanya nitende mema tu?
Yeye sio dikteta mzee,angekubana au kukupangia usingekuwepo leo hii. Yan hauko chini ya sheria ndio mana una uhuru wa kufanya dhambi na ukaendelea na maisha
 
Yaani Mungu mwenye huruma sana,upendo sana na muweza wa yote anipe uhuru wa kutenda dhambi ambacho ni kitu kibaya sana?!Hii inamake sense?
 
Mungu mwenye upendo sana,huruma sana na mwenye uwezo wa kufanya kila kitu alishindwa vipi kumzuia binadamu asile hilo tunda?Upendo wake uko wapi?Huruma yake iko wapi?Uwezo wake uliotukuka uko wapi?

Sikia mkuu.
Mungu alipomuumba Adam na Hawa kusudi lilikua wamtii na Kumtumikia yeye tu, pamoja na yote aliyowapatia wafurahie lakini walikua bado hawajafunuliwa jema na Baya kwa wakati wote walikua wanajua yaliyo mema tu.
Ila Baada ya Ibilisi kuona na yeye anaweza kua na uwezo kuliko Mungu ndipo alipoasi sasa na kutupwa duniani, na ibilisi huyo alikua malaika huko Mbinguni lakini pia huyo ibilisi hakuwahi kufunuliwa uwepo wa Kristo ambae ni Mwana wa Mungu, yeye alimuona Mungu kama Mungu Pekee yake soma Mwanzo vizuri utaijua Biblia
Sasa baada ya kuja kuwadanganya Adam na Hawa na kulila tunda la ujuzi wa mema na mabaya ndipo walipofunuliwa ufahamu na kujua lipi jema na lipi baya na ndo maana wakati Mungu anakuja watembelea walikua wamejificha ni sababu ya kua walijua tayar mema na mabaya.
Na hakika baada sasa na wao kudanganywa na kuasi ndio Mungu akaanza kutoa hukumu alianza na ibilisi, Akaja kwa Mwanamke, akabaki Adam na Mungu alihitaji Adamu atubu aombe radhi hakika naamini wangesamehewa lakini hakuna sehemu yeyote Adamu alijutia au kutubu au kuomba samahani na ndipo Mungu akasema mwisho hakika Mtakufa. Hivyo tulideserve.
Lakini sababu ya Mungu kua mwingi wa huruma na rehema pamoja na Adamu kushindwa kutubu / kujutia bado alituhurumia akasema hivi sitaleta gharika wala maafa yeyote tena kwa kizazi cha wanadamu ilaaaa nitamtuma Mwanangu ili aje kuukomboa ulimwengu huu na dhambi zake, na ndio Maana yesu ama Kristo mwana wa Mungu alipokuja na kukamilisha kazi yake tulikombolewa kwa njia ya Imani na si Sheria tena na ndio maana sasa una uhuru wa kuchagua kumtumikia Mungu aliye Juu au Ibilisi ungali hai. Uchaguzi ni wako. Ili baada ya kufa mwili huu basi roho yako iwe mahali sawasawa na njisi ulivyoenenda na kumchagua wa kumtumia wakati ukiwa Duniani.
Mungu anasema Mautini Hakuna kumtumikia yeye wala kujua lolote bali ungalipo hai ndipo uwezapo kumtumikia.
Mwisho kupanga ni kuchagua na kila Mtu yupo anaemtumikia either ni Mungu au Shetani. Mungu yupo na Shetani yupo na mwisho kuna maisha mazuri zaidi ya haya baadae
Huna haja ya kuogopa kufa mwili huu ila tuogope kufa kwa roho zetu.
 
Unaamini kuwa Mungu hashindwi chochote?Kama jibu ni ndiyo,kwa nini alishindwa kumzuia ibilisi asihasi?
 
Back
Top Bottom