Ulipaswa kumsikiliza kwa umakini, kila neno na sentesi kabla ya hitimisho lako hilo.
Mwanasayansi yeyote, makini na aliyebobea kwenye taaluma yake, kama Rais Magufuli, tofauti na wa sayansi ya jamii, tafiti zao hufanywa kutokana na nadharia (hypothesis) na si maswali "research questions". Ili kupata jibu sahihi la " hypothesis" inabidi mtafiti atayarishe mazingira ya kisayansi kukusanya takwimu, kuzichambua kabla ya kuhitimisha matokeo (hypothesis, data collection, data analysis, conclusion, recommendations).
Alichokisema Rais Magufuli ni nadharia kuhusu jinsi ya kupima na aina ya vipimo vya COVID-19 kama vinakidhi matakwa ya kisayansi (Generalisation + Replication). Nadharia yake hiyo aliifanyia majaribio uliyoyataja akahitimisha kwa nadharia mpya kama ulivyozianisha. Nadharia mpya ameagiza taasisi na vyombo husika kuzifanyia kazi kupata majibu sahihi.
Madai yako kwamba Hiyo hotuba itaibua mengi sana, na inaweza ikajadiliwa mpaka Ulaya, maana leo hii tunaambiwa na kuona watu wanakufa kona zote za dunia..., ametoa jibu. Baadhi ya watu wanakufa kwa sababu ya hofu, "stress", tiba isiyo sahihi, nk. Na wala hajasema COVID-19 siyo ugonjwa hatari.
Nakudhauri uisikilize vizuri kwani imeibua maswali mengi. Hakika Rais Magufuli atakuja kukumbukwa kwa mambo mengi Tanzania na dunia nzima.