Kama kweli Mungu yupo, basi hana nguvu

Itakua unamuomba aliyekaimishwa madaraka ya Mungu
 
Duh nimecheka sana leo.....Mzee Mungu Anatisha asikwambie mtu.......inategemeana unamuombaje ! Kaeni na watu wenye kutafakari ikiwa Kuna mambo yanawachanganya(wazee)
 
 
Nilipokuwa deep kwenye dini maisha yangu yalikuwa magumu kama chuma Cha pua nimetoka uko uko ila waya ni mkali sana unaweza ukadata na kupagawa Kuna mida huelewi maisha yanataka nn? Kmmk
Hekima ya Mungu siyo ya mwanadamu. Unapoomba, usiache kuruhusu hekima ya Mungu itende kazi. Ebu fikiria sala ile ya Kristu Masiha wetu.

Bwana wetu Yesu Kristu, kabla ya kukamatwa na kuanza kusulibishwa, aliyaona mateso yote atakayoyapitia. Aliumia sana, hata kutoa jasho la damu. Akaamua kumwomba Mungu Baba akisema, ' Baba kama inawezekana, kikombe hiki kinipitie mbali, LAKINI si nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe Baba'. Mungu hakuyafuta mateso wala kifo cha msalaba kwa mtakatifu wake, bali alimjaza ujasiri wa kukipokea kikombe cha mateso, hata kuwa tayari kumkaripia Petro alipotaka kuanza kupambana na wale askari wa makuhani, akamwambia Petro, "rudisha upanga wako alani, unataka kikombe alichonipa Baba nisikinywe?"
 
Kuto kupata majibu ya maombi wala usimlaumu Mungu wala dini wala mtu yeyote, changamoto ni wewe mwenyewe,

IMANI Mkuu hauna imani... full stop 🛑

Mbona wenzako wanajibiwa... Mkuu inabidi ujiulize kwanini mimi!?
 
Kuto kupata majibu ya maombi wala usimlaumu Mungu wala dini wala mtu yeyote, changamoto ni wewe mwenyewe,

IMANI Mkuu hauna imani... full stop 🛑

Mbona wenzako wanajibiwa... Mkuu inabidi ujiulize kwanini mimi!?
Watoto wachanga na wadogo wanaoteseka na kupata shida hapa duniani, Je na wao wanakuwa wamekosa imani hadi wateseke?

Hivi huyo Mungu hajui kwamba watoto wachanga na wadogo hawana ufahamu wa kuwa na imani?

Kwa nini huyo Mungu Hawasaidii watoto wachanga na wadogo wasio na imani hadi wanabaki kuteseka?

Kwa nini huyo Mungu anaruhusu na kuacha watoto wadogo wateseke, ilhali anajua kwamba hawana ufahamu wa kuwa na imani?

Hivi huyo Mungu wako anajielewa kweli?
 
Mungu yupo .mwambie atatenda
Huyo Mungu ameshindwa kutekeleza, kutenda na kujibu maombi ya maelfu ya watu.

Ndio maana mpaka leo hii bado watu wanahangaika kumpigia kelele huyo Mungu kwa kusali, kufunga na kupayuka kama mbayuwayu wakimlilia awasaidie shida zao, Lakini Holaaaa!!!

Hakuna kinacho tokea.

Nothing happens.
 
Kinachonifurahishaga ni jinsi hawa 'watu wa Mungu' wanavyowatukana watu wanaokuja na hoja zinazokinzana na Mungu. Huwa najiuliza kwa matusi hayo mbinguni wataenda kweli?
Ukiona Mungu anahangaikiwa na watu ajulikane yupo badala ya kuja yeye mwenyewe kujidhihirisha yupo, Fahamu kwamba huyo Mungu alitengenezwa na watu tu.

Hakuna Mungu.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.
 
Mungu awasaidie hao watoto kwani amewazaa yeye?
 
Usimuombe Mungu moja kwa moja huwa yupo bize na mambo mengi

Watumie Malaika, wajulishe Malaika shida zako watamfikishia ujumbe

Hata mkuu wa mkoa tu huwezi kumuona kirahisi rahisi bila kupita kwa wasaidizi wake kwanza

Pia Mungu alishakupa kila kitu ni wewe tu kwenda kuchukua
 
Free will; una uhuru wakufanya chochote na kwa chochote utakacho ukifanya uwe tayari kuwajibika kwa matokeo yake kiwe kibaya ama kizuri.

Kuhusu hao watoto, We ndio unawaona wanateseka, unajilinganisha na hali yako ila wao katika dunia yao wako normal... Wazazi wao ndio wanajisikia vibaya ila ni wajibu wao kwasababu waliamua kufanya hivyo.

Kuna kitu kinaitwa matumaini faraja(usawa kati ya furaha na huzuni) katika hili binadamu wote tupo sawa haijalishi unamali au hauna, kihisia wote tipo sawa ndio maana wote tunakuwa na matumaini ya kuendelea kuishi.

Pia material things vitu kama pesa ardhi magari nyumba ni vitu vya kumiliki tu, lakini sio utajili au vina thamani, huo uthamani wake tunaouona ni mtizamo tu, fikra(just perception) , tuliojengewa na mfumo wa maisha umeundwa katika namna ya kutufubaza, (illusion), mfano pesa ni number katika sarafu au karatasi.
 
Ili Mungu akusikie na kukupa yale unayomuomba, kuna vigezo na masharti. Baadhi ya vigezo vipo katika Andiko hili:
:Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, wakijinyenyekeza na kuomba na kunitafuta uso wangu, na kuziacha njia zao mbaya, ndipo nitawasikia kutoka mbinguni, na kuwasamehe dhambi zao, na kuiponya nchi yao.” (2 Mambo ya Nyakati 7:14)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…