Kama kweli Mungu yupo, basi hana nguvu

Kama kweli Mungu yupo, basi hana nguvu

Kinachonifurahishaga ni jinsi hawa 'watu wa Mungu' wanavyowatukana watu wanaokuja na hoja zinazokinzana na Mungu. Huwa najiuliza kwa matusi hayo mbinguni wataenda kweli?
 
Mungu fala tu, hawezi kukupatia hata senti moja

Eeh Mwenye Enzi Mungu, nakuomba msahama kwa kwa niaba ya huyu mleta uzi, wewe ni Muweza wa Yote, unayempa umtakaye na kumnyima umtakaye.

Endelea kutuzidishia imani, matumaini na mapendo, tunapoendelea na mwaka huu mpya, ili wewe uweze kudhihirka kwa wale wenye subra na wakutumainiao. AMEN
Kumbe Mungu ana upendeleo!!!
 
Ukifikiria sana haya maisha sometimes unaweza kufuru,ila yote kwa yote Mungu yupo ila ndo yataka uvumilivu sana,wakati umekata tamaa,akili yako imefika mwisho ndo unaona majibu

Sijui situation unayopitia ila kwenye maisha Kuna kuanguka na kuinuka,usikate tamaa mizimu Ina ghalimu lazima utoe kafara n.k.
Ngoja nijaribu upande wa pili hakuna namna.
Dharau zimezidi, Mungu naye nilimuamini sana, Lakini kwa sasa nimethibitisha hana nguvu kwenye maisha yangu.
 
Mmhh maandalizi tena yaani Mungu mwenye mamlaka na muumba wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo umfanyie maandalizi tena..
Sasa na waganga nao wasemaje maan kule ndio mambo ya kuku mbuzi ni kawaida.
Tushangae wote, Kama Mungu muweza wa yote mpaka umuandae!!
 
Na kinachowafanya wamuamini Mungu ni kwa sababu ya stori ya kusadikika ( MOTO WA MILELE)
Kinachonifurahishaga ni jinsi hawa 'watu wa Mungu' wanavyowatukana watu wanaokuja na hoja zinazokinzana na Mungu. Huwa najiuliza kwa matusi hayo mbinguni wataenda kweli?
 
kila nikiona kichwa cha huu uzi nacheka!..
jamaa kachapa bila mbwembwe kikatili sana halafu hapohapo anatafuta mizimu!.. aangalie isijekufika mwisho wa mwaka yeye ndo akageuka kuwa huyo mzimu!..🤣
Mkuu nishajiandaa kufa, Anytime ikitokea ni Sawa.

Kifo ni kikombe ambacho kila mtu atakinywa👽
 
Aisee!!
Kabla hujafikiria kumuomba Mungu hakikisha alivyokupa kama akili na afya umevitumia kwa ukamilifu,,,unaweza pia kutumia na akili za wanadamu wengine kupitia USHAURI..

Zaidi ya hapo tafuta sadaka umpelekee Mwamposa.
 
imeandikwa usimjaribu bwana mungu wako kwa chochote hata kwa maombi bali muombe kwa moyo wako wote na kwa akili zako zote utamuona
ZABURI 14 : 1

"Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu !"


Mwambie Mpumbavu mwenzio Yericko Nyerere akuonyeshe mizimu ya mababu zake ukaiabudu uenda inaweza kukusaidia na kutatua matatizo yako!
Yericko huwa hayupo serious.
 
Hauna imani kama unaamini kuna mizimu na mashetani basi amini kuna malaika na kuna mungu
Mwanzoni nilikuwa namuamini Mungu.
Ila kwa sasa imani imepungua sanaaaa, Najaribu asili nayo ikigoma basi nitakamilisha kwamba huenda dunia ilitokea kibahati mbaya
 
Na kinachowafanya wamuamini Mungu ni kwa sababu ya stori ya kusadikika ( MOTO WA MILELE)
Hakuna Jehanam mkuu wala moto wa milele.
Yaani ukifa basi habari zako zimeishia hapo.
Hakuna moto wala Pepo kwamba utaenda kustarehe huko baada ya kufa
 
Mungu yupo sema ujafanya sacrifice

Chinja jogoo rangi yyte pika kula supu,
Sheria chinja kwa mkono wako
Mungu anataka kafara(sacrifice) na hii ni siri ambayo viongozi wa dini weng hawakwambii ila wao wanafanya sana kafara
Sawa Mkuu
 
Back
Top Bottom