1. Mtu hujatubu madhambi yako ila unataka Mungu akutendee. ...Hilo sahau.
2. Mtu hutoi sadaka,zaka,malimbuko nk..bado unataka Mungu akuonekanie....Hilo sahau.
3.Mtu huna mahusiano mazuri na wenzako,ndugu zako na jamaa zako ..bado unataka Mungu akufanyie wepesi..Hilo sahau.
4. Mtu hujitoi Kwa kazi za Mungu,familia,jamii ..bado unataka Mungu ajibu maombi .Hilo sahau.
5.mtu unaishi Kwa kibri,unajisikia,si msikivu,hutaki ushauri,Wala huna chembe ya Huruma Kwa wenzako na Tabia ya wizi huachi...bado unataka Mungu akupe miujiza Hilo sahau..
6.mtu husomi neno la Mungu,hufungi..ukioomba Mungu unaomba Kwa kumshurutisha na malalamiko mengi..bado unataka MUNGU AKupende na kukutendea..Hilo sahau...
7.Mungu ana vigezo vyake..kama hutaki kuvijua ila unajiendea kama nyumbu...hakika sahau kupata majibu ...
8.mtu umekaa tu,hujaribu,huonyeshi jitihada Ili Mungu atie Kudra zake..wewe unataka maombi yashushe majibu kama Mana ..huna pa kushika Wala kuanzia huna connection...halafu eti Mungu mbona umeniachia...atakuacha kweli..
Kwa hiyo rekebisha njia zako...Mungu Hana sikio zito asisikie Maombi yako...