Kama kweli Mungu yupo, basi hana nguvu

Kama kweli Mungu yupo, basi hana nguvu

Freewill haipo.

Huna freewill.

Kwa mfano, Huna uhuru wa kurudi mwaka 1980.

Hukuwa na freewill ya kuchagua uzaliwe ama usizaliwe, Umeshtukia tu umesha zaliwa bila kuamua mwenyewe.

Hivyo hakuna freewill.

Watoto wanakufa kwa njaa, vita, magonjwa halafu unasema wako normal?

Una utimamu huko kichwani kweli wewe?

Nenda Ethiopia huko Tigray, Cabo Delgado Msumbiji, Sudan kusini, Somalia Uone jinsi watoto wanavyo kufa kwa njaa na ukame!

Halafu wewe unakula na kushiba unasema eti hawateseki!!

Gentleman, Do you have common sense?

Ebu tembea uone!

View attachment 3191266

Kuna watu kupata basic needs tu ni shida achilia mbali magari, nyumba na pesa.

Kuna watu hata mlo mmoja tu kwa siku hawapati.

Maji hawapati.

Makazi na malazi hawana.
Uwepo wa mwanadamu hauishii kwenye material world tu. Haya mambo unayoyashuhudio na kukuvunja moyo ni sehemu ndogo sana ya mchakato.

Na kama unataka kuwe hakuna changamoto yoyote hapa duniani, basi hakukua na maana yoyote ya sisi kuwepo hapa duniani.

Ni sawasawa unaenda shule halafu hautaki mitihani, kama hautaki kufeli basi unaweza ukaongeza juhudi na kubadilisha hatima yako ya matokeo, hivyo hivyo katika maisha hapa duniani wewe binafsi unauwezo wa kubadilisha hatima yako.

Chakuzingatia ni kwamba kuna nguvu na uhuru,

Nguvu inahitaji majukumu ili kufanya kazi kudhihirisha uwezo wake. Sasa tutajuaje uwezo wa nguvu zako?

Uhuru ili kufurahia uhuru unahitaji sheria, bila hivyo watu watavuka mipaka, na sheria zipo kwaajili yako na sio dhidi yako... Sheria inakulinda wewe.
 
Sasa kulikuwa na haja gani ya sisi kuwepo kwenye materials world tu?
Na kama unataka kuwe hakuna changamoto yoyote hapa duniani, basi hakukua na maana yoyote ya sisi kuwepo hapa duniani.
Ndio Hakuna maana yeyote sisi tuwepo kwenye dunia yenye changamoto.

Kama huyo Mungu aliweka changamoto hapa duniani halafu yeye kabaki zake huko alipo anakula good time naku enjoy life, Basi huyo Mungu mjinga sana.
Ni sawasawa unaenda shule halafu hautaki mitihani, kama hautaki kufeli basi unaweza ukaongeza juhudi na kubadilisha hatima yako ya matokeo, hivyo hivyo katika maisha hapa duniani wewe binafsi unauwezo wa kubadilisha hatima yako.
Mtoto mchanga anayezaliwa kisha wazazi wake wanafariki, Yeye binafsi atawezaje kubadilisha hatima yake bila kuhitaji msaada?

Au unaongea tu bila kufikiri kwa kina?
Chakuzingatia ni kwamba kuna nguvu na uhuru,

Nguvu inahitaji majukumu ili kufanya kazi kudhihirisha uwezo wake. Sasa tutajuaje uwezo wa nguvu zako?
Mtoto mchanga anayezaliwa kisha wazazi wake wanafariki, Atawezaje kutumia nguvu zake yeye mwenyewe ili akue na kufanikiwa yeye mwenyewe kwa nguvu zake tu?
Uhuru ili kufurahia uhuru unahitaji sheria, bila hivyo watu watavuka mipaka, na sheria zipo kwaajili yako na sio dhidi yako... Sheria inakulinda wewe.
Freewill haipo.

Ndio maana huwezi kuua mtu, Halafu useme ni freewill yako umeamua tu kuitumia kuua.

Ukishaona kuna sheria jua kwamba hakuna uhuru.
 
Kwanini awasaidie wakati hakuwazaa yeye?
Sijasema Mungu asaidie watu.

Nimesema hakuna Mungu wa kusaidia watu.

Mungu hayupo.

Una elewa ninacho andika?

Au unakurupuka tu, ku komenti?
 
Sijasema Mungu asaidie watu.

Nimesema hakuna Mungu wa kusaidia watu.

Mungu hayupo.

Una elewa ninacho andika?

Au unakurupuka tu, ku komenti?
Mungu hayupo kwako na kwa ujinga wako binafsi

Mimi Naamini Mungu yupo na anaweza yote.
 
Kunywa maji mengi,na fanya mazoezi hii husaidia kupungiza frustration
 
Mungu hayupo kwako na kwa ujinga wako binafsi
Uwepo wa ujinga ni uthibitisho tosha kwamba Mungu hayupo.

Mungu huyo angekuwepo, Asingeumba binadamu wajinga wanao sema yeye hayupo.

Au kama huyo Mungu yupo, Na yeye ni mjinga vilevile kwa kuumba binadamu wanaosema yeye hayupo.

Wakati alikuwa na uwezo wa kuumba binadamu watakao sema yeye yupo siku zote na kwa wakati wote.

Mungu huyo na yeye ni mjinga sana.
Mimi Naamini Mungu yupo na anaweza yote.
Kuamini unaweza kuamini hata uongo, Lakini ukianza kudai kwamba imani yako ina ukweli lazima uthibitishe.
 
Ameumba wajinga ili tuweze kuishi vizuri.

Unafikiri wote tungekuwa na akili tungewezana?

Ndiyo maana aliumba maskini na matajiri, wote tungekuwa matajiri tungewezana huko mtaani?

Una uwezo mdogo sana wa kuchanganua mambo ya dunia hii.
 
Kama Mungu aliumba watu wajinga, Basi hana ukamilifu wowote, Na yeye pia ni mjinga vilevile.

Pia kazi yake ya uumbaji ina dosari na kasoro, Kwa kuruhusu ujinga uwepo kwa watu badala ya kuruhusu maarifa yawepo kwa watu wote.

Kama Mungu aliumba maskini na matajiri, Basi ni Mungu mwenye upendeleo na ubaguzi.

Huyo Mungu hafai kabisa anastahili kufurushwa maana ni Mungu mjinga, mbaguzi na mwenye upendeleo.
 
Wakati wako wa kuelewa haya ukifika utaelewa na utakuwa msaada mkubwa sana kwa wengine

Kwa sasa utanipotezea tu muda sababu tayari una mahitimisho yako unayotaka kuyaamini
 
Mimi siamini kwenye kuamini.

Mimi najenga hoja kwa logic.
 
Mungu ni power within waweza itumia kumake whatever you want sasa kama hujui uwezo ulionao na jinsi ya kuutumia pole,ufe ukaonyeshwe faili lako na vitu ambavyo ungeweza kuvifanya ukiwa duniani ndo utashangaa atract those power and use them
 
Mungu ulikuwa unamuabudu kwa kujaribu ukijua utaenda kwa mizimu ndo maana hakujibu maombi yako
 
Wakoloni wameharibu sana waafrika na hizi dini zao za mchongo wamemuumba mtu ambaye hayupo na kujenga chuki baina yetu Leo hii tunachukiana kisa dini
 
Anayechukia mwenzie kisa dini huyo hana akili,kila mtu aamini kwa imani yake
 
Mimi siamini kwenye kuamini.

Mimi najenga hoja kwa logic.
Ndiyo, wewe huamini, na hii ni kutokana na ujinga wako binafsi.

Lakini kuna watu WANAKUAMINI WEWE na ndiyo maana wanafanya biashara na wewe, ndiyo maana wanapanga DILI na wewe. Hii yote ni kwa sababu WANAKUAMINI ingawa mwisho wa siku wewe ni binadamu tu na una mapungufu yako!

Sasa kama kila mtu angeamua kutokukuamini wewe kama vile unavyotaka kutoamini katika Mungu ungeweza kuishi hapa duniani wewe?.

Ufalme wa Mungu upo ndani yako, kazi ni kwako siyo kwa Mungu.
 
Watu wana niamini kwa sababu wananiona nipo.

Sasa wewe unaamini Mungu ambaye hata haonekani na wala hujawahi kumuona.

Una amini illusion zako tu.

Wewe ndio mjinga kwa kuamini kitu ambacho hata Hujawahi kukiona.

Uliomba nini asikupe? Au unaomba ambavyo tayari vipo tele, mfano kama umeomba pesa lazima ufanye kazi, Mungu pia anaweza asiondoe tatizo lako lakini akafanya ukalimili lisiwe kikwazo kwako na pia likakukomaza kukabiliana na tatizo lingine lolote litalotokea lakini pia unaweza kuomba lakni upande wako kuna mambo yasiyompendeza hujaacha pia?
 
Wangapi wanaonekana na hawaaminiki kama wewe?

Kuonekana tu tayari ni kigezo cha mimi kukuamini?

Wewe ni mjinga usiyejielewa

Ni mpumbavu mkubwa
 
Uliomba nini asikupe? Au unaomba ambavyo tayari vipo tele, mfano kama umeomba pesa lazima ufanye kazi, Mungu pia anaweza asiondoe tatizo lako lakini akafanya ukalimili lisiwe kikwazo kwako na pia likakukomaza kukabiliana na tatizo lingine lolote litalotokea lakini pia unaweza kuomba lakni upande wako kuna mambo yasiyompendeza hujaacha pia?
Wengi huwa wanaomba hela! Badala ya kuomba hekima, uzima, afya, akili, ubunifu, uaminifu, uvumilivu, kujitoa mhanga

Wenyewe wanaomba hela! Hela ZENYEWE zimeanza kuwepo miaka ya juzi tu hapo
 
Back
Top Bottom