Kama kweli Paroko katajwa kimakosa kifo cha Albino, Polisi Mtawaambia nini Watanzania?

Kama kweli Paroko katajwa kimakosa kifo cha Albino, Polisi Mtawaambia nini Watanzania?

Taarifa zinasema huyo mtajwa ni Padre aliyesimamishwa kufanya huduma kutokana na tatizo la uraibu wa pombe.
Upadre ni sacramenti huwa hautoki milele huyo ni padre

Upadre wake haujafutika Kwa hiyo sababu .

Huyo bado ni Padre hizo zingine zote porojo ohhh sijui Teja sio padre sio kweli.Pl
Huyo ni padre asilimia Mia moja
 
Ni paroko kweli mimi pia ni mkatoliki na nipo uku kagera mkuu inauma sana.
Afadhali wewe kuwa mkweli ubarikiwr na Mungu

Hakuna watu wabaya kama watu wenye tabia ya kupenda MTU akiwa vizuri likitokea la kumkuta wanaanzà ohhh sijui Teja Tu mbwa Koko Tu huyo simjui mlevi Tu ngedule Tu huyo

mbaya sana
 
Wanajumuiya kina nani?

Ina maana jeshi la polisi limekurupuka kusema kwamba huyo alikuwa paroko?

Polisi wamewezaje kusema ni paroko?

Ina maana wananchi wa hilo eneo walikuwa hawajui mpaka wawambie polisi huyo mtuhumiwa ni paroko?
Kufahamu kuwa huyu ni Paroko au siyo Paroko unasikiliza wananchi wa hilo eneo au unawauliza waliompa hiyo kazi ya kuwa Paroko..kulikuwa na ugumu sana kupigia watu wa Jimboni kuuliza kama kweli huyo mtu ni mtumishi wao, au ni namna ya kuhamisha mjadala, msemaji wa polisi anawezaje kutamka cheo cha mtu bila kuwauliza waliompa hicho cheo??? Jimbo Katoliki la mahali husika wanawajua maparoko wote wa jimboni kwao..
 
Kawaida mtu ukikamatwa na polisi lazima utoe maelezo yako yanayokuhusu wewe mtuhumiwa na maelezo yaliyotolewa na polisi ameyatoa mwenyewe mtuhumiwa kama mtuhumiwa amedanganya itajulikana mbele ya safari.
 
Kufahamu kuwa huyu ni Paroko au siyo Paroko unasikiliza wananchi wa hilo eneo au unawauliza waliompa hiyo kazi ya kuwa Paroko..kulikuwa na ugumu sana kupigia watu wa Jimboni kuuliza kama kweli huyo mtu ni mtumishi wao, au ni namna ya kuhamisha mjadala, msemaji wa polisi anawezaje kutamka cheo cha mtu bila kuwauliza waliompa hicho cheo??? Jimbo Katoliki la mahali husika wanawajua maparoko wote wa jimboni kwao..
Kwa hiyo jeshi la polisi limekurupuka kusema kwamba alikuwa paroko?

Au wewe ndio mjuaji sana kwamba huyo mtuhumiwa sio paroko?
 
Kwani mtuhumiwa hajui kuongea mpaka wakaulize jirani? Maelezo aliyoyatoa ndiyo yametangazwa na utakuta kasaini kuthibitisha alichotamka kutoka kwenye kinywa chake.
 
Sasa badala ya kuombeleza kifo cha mtoto na kutaka wote waliohusika wanyongwe ..tutaanza kutetea Imani zetu zisichafuke?..kwani hata akiwa Askofu...si ni yeye binafsi na uovu wake? Imani yake inaingiaje,?
Cheo chake ndicho kimefanya uovu au yeye mtu binafsi, kwa nini msemaji anataja Paroko...angetaja jina tu kuna ubaya au mapungufu gani..
 
Kwani mtuhumiwa hajui kuongea mpaka wakaulize jirani? Maelezo aliyoyatoa ndiyo yametangazwa na utakuta kasaini kuthibitisha alichotamka kutoka kwenye kinywa chake.
Wewe unapoandika ni mfagizi ofisin halmashauri, wanaoandika maelezo wanazuiwa kuuliza halmashauri unakofanyia kazi? angesema yeye ni mpishi ikulu wasingeuliza ikulu kama mtu huyo wanamfahamu? kuna tofauti mtu anapotaja jina lake au cheo chake, jina ni lake binafsi, cheo si chake na hivyo ni vyema kuwauliza wenye hicho cheo kama kweli muhusika ni mtu wao..
 
Kwa hiyo jeshi la polisi limekurupuka kusema kwamba alikuwa paroko?

Au wewe ndio mjuaji sana kwamba huyo mtuhumiwa sio paroko?
Wewe hutaki mtu awe mjuaji..ni kosa kuwa mjuaji? angetaja kuwa ni Polisi mwenzao wasingetaka kupata uhakika wa hayo anayosema huko anakofanyia kazi?
 
Jeshi harikurupuki mpaka taarifa zinatoka wameshapewa kibano cha kutosha na wametapika nyongo, yaani kukomesha vitendo hivyo, wakule shaba hadharani au na wao wakatwe mikono kwanza na ndimi zao ili wasikie uchungu aliouhisi Asimwe kabla ya kifo chake.
 
Tim
Salaam Wakuu,

Mambo ya dini yanaamsha hisia sana.

Inadaiwa Paroko aliyetajwa si Paroko wala nini. Ni kweli Polisi nao ni Binadamu. Kwa hili tunaomba uwajibikaji.

Inadaiwa Paroko ni Deodatus Tibakwasa na msaidizi wake ni Fr. Mathias.

"Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime amewataja watuhumiwa waliokamatwa ambao walieleza jinsi walivyoshiriki katika tukio hilo ni pamoja Baba mzazi wa mtoto huyo aitwaye Novart Venant, Desideli Evarist ambaye ni mganga wa jadi mkazi wa Nyakahama, Elipidius Rwegoshora Paroko Maidizi wa Parokia ya Bugandika ambaye anadaiwa kumfuata na kumshawishi Baba mzazi wa mtoto ili wafanye biashara ya viungo vya binadamu.".

Huyu Rwegoshora inadaiwa ni teja ambaye alikuwa anaenda kwa Paroko kupata msaada.

Bado naamini Taarifa ya Polisi. Ila pia natamani Msaidizi wa Paroko ajitokeze hadharani kukanusha mwenyewe.
Time will tell .
 
Wewe hutaki mtu awe mjuaji..ni kosa kuwa mjuaji? angetaja kuwa ni Polisi mwenzao wasingetaka kupata uhakika wa hayo anayosema huko anakofanyia kazi?
Kwa hiyo jeshi la polisi limekurupuka kusema kwamba huyo mtuhumiwa ni paroko msaidizi?

Wewe una uthibitisho upi kwamba huyo mtuhumiwa sio paroko?
 
Limekosa weledi kisa anaetuhumiwa ni Paroko? au una maana gan mkuu.
Kwani mtu akiitwa Paroko, Sheikh, mchungaji au Askofu au cheo kingine chochote Cha kidini hawi binadam wa kawaida tena? Shetani hamtafuti? Hawezi kutenda dhambi tena? Hawezi kuanguka dhambini? Kama hahusiki si ataachiwa? Si ni mtuhumiwa tu? Kwani Mahakama imethibitisha? Kama kahusika Mahakama au Polisi wenyewe si watakamilisha upelelezi?
 
Back
Top Bottom