Mi navyojua hata mitaani ukisikia mtu katika stori anakuambia habari za "mambele" huwa hamaanishi China, Urusi, Korea, india, Uk, wala Mexico
Hapo ni Marekani inakusudiwa.
Hata mtu akiwa yuko positive kwa kila jambo utasikia "fulani ni mzungu sana" yani huo uzungu haumaanishi huyo mtu amefananishwa na mfaransa sijui au nani... hapo ni MMarekani
Hata slang, lifestyle watu wanaangalia Marekani wanafanya nini.
Hata wasanii wetu wa hapa hawafanyi mziki kwa kumuangalia msanii fulani maarufu wa China, Urusi, Korea, India ili awe motivated au kama role model wake
Marekani ndio inspiration nation karibia kila Carrier, mapungufu yao kwenye maswala madogo madogo ya ushoga yasiwe sababu ya watu kushindwa kuusema ukweli ambao unaonekana dhahiri.
Kulikuwa na wahindi na wachina walikuwa wanajifanya wao wame-stick kwenye utamaduni wao
Hapa ni mchina akiwa na vazi lake la kiasili ambalo ndio walikuwa wabishi kujifanya watunza misingi
Angalia saizi
Na ndio maana hata Bruce Lee alienda kuishi Marekani, aliona home ni miyeyusho
Wahindi ndio kabisaaa kama ulikuwa unafatilia hata zile nyimbo zao kwenye movies wanazoigiza saizi ni tofauti na za miaka ile.
Kumekuja na evolution yenye taste mpya ya kimarekani ambapo humo na rap zipo, hiyo ni department ya sanaa ya upande wa nyimbo tu, ila kuna mengi.
Na ndio maana Mkorea kaskazini akaona bila kutumia nguvu ya ziada kuweka sheria ngumu hapa baada ya miaka kadhaa nitakuwa natawala Taifa ambalo lina falsafa zote za kimarekani.
Na ndio maana akapiga marufuku uvaaji wa jinsi ya blue. Lakini baadaye alipoona hata hizi rangi nyingine nazo zimekuwa zikivaliwa sana akaamua nazo apige marufuku totally.
Nchi yetote ambayo raia wakapewa uhuru bila sheria za kuwabana wote wata adapt culture ya kimarekani.
Ukiona nchi raia wanaishi katika lifestyle tofauti na ya Marekani ujue kuna sheria kali imesimikwa na wala sio jambo la kuwapa pongezi raia kuwa wamekubali asili yao kwasababu wameshurutishwa kuishi hivyo.