Kama Marekani ni nchi ya Kishetani ni kwanini mamilioni ya watu duniani hutamani kuishi Marekani?

Kama Marekani ni nchi ya Kishetani ni kwanini mamilioni ya watu duniani hutamani kuishi Marekani?

Huwa nikiona maelfu ya watu kila siku toka nchi za Amerika ya Kusini na kwingineko duniani wanavyolazimisha kuingia Marekani, huwa najiuliza, inakuwaje nchi inayosemwa kwamba ni mhimili wa Ushetani duniani inagombaniwa na watu kwenda kuishi.

Huoni harakati za watu kwenda kwenye zile nchi zenye "Ustaarab" au za "wacha Mungu" kuliko harakati zinazofanywa na watu kwenda kuishi Marekani. Kwa nini watu wanang'ang'ania kwenda kwenye nchi inayoitwa ya kidhalimu?
Kama marekani ni nchi ya kishetani ina maana wanaoenda huko nao wana kaushetani au ?
 
Mbona wanaenda nchi nyingine kama Canada, Uk, South Africa, France nk.
Huoni wahamiaji kutoka Afrika wanakufa maji karibu kila siku Wakikimbilia Ulaya?!
Hii ni Kwa sababu ulaya imepakana na afrika. Laiti kama USA ingekua imepakana na afrika ingekua shida Sana kila mwafrika anataka kuzamia huko. Amin maneno yangu aisee.

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Mi navyojua hata mitaani ukisikia mtu katika stori anakuambia habari za "mambele" huwa hamaanishi China, Urusi, Korea, india, Uk, wala Mexico

Hapo ni Marekani inakusudiwa.

Hata mtu akiwa yuko positive kwa kila jambo utasikia "fulani ni mzungu sana" yani huo uzungu haumaanishi huyo mtu amefananishwa na mfaransa sijui au nani... hapo ni MMarekani

Hata slang, lifestyle watu wanaangalia Marekani wanafanya nini.

Hata wasanii wetu wa hapa hawafanyi mziki kwa kumuangalia msanii fulani maarufu wa China, Urusi, Korea, India ili awe motivated au kama role model wake

Marekani ndio inspiration nation karibia kila Carrier, mapungufu yao kwenye maswala madogo madogo ya ushoga yasiwe sababu ya watu kushindwa kuusema ukweli ambao unaonekana dhahiri.

Kulikuwa na wahindi na wachina walikuwa wanajifanya wao wame-stick kwenye utamaduni wao

Hapa ni mchina akiwa na vazi lake la kiasili ambalo ndio walikuwa wabishi kujifanya watunza misingi

View attachment 2590942

Angalia saizi
View attachment 2590947
Na ndio maana hata Bruce Lee alienda kuishi Marekani, aliona home ni miyeyusho

Wahindi ndio kabisaaa kama ulikuwa unafatilia hata zile nyimbo zao kwenye movies wanazoigiza saizi ni tofauti na za miaka ile.

Kumekuja na evolution yenye taste mpya ya kimarekani ambapo humo na rap zipo, hiyo ni department ya sanaa ya upande wa nyimbo tu, ila kuna mengi.

Na ndio maana Mkorea kaskazini akaona bila kutumia nguvu ya ziada kuweka sheria ngumu hapa baada ya miaka kadhaa nitakuwa natawala Taifa ambalo lina falsa zote za kimarekani.

Na ndio maana akapiga marufuku uvaaji wa jinsi ya blue. Lakini baadaye alipoona hata hizi rangi nyingine nazo zimekuwa zikivaliwa sana akaamua nazo apige marufuku totally.

Nchi yetote ambayo raia wakapewa uhuru bila sheria za kuwabana wote wata adapt culture ya kimarekani.

Ukiona nchi raia wanaishi katika lifestyle tofauti na ya Marekani ujue kuna sheria kali imesimikwa na wala sio jambo la kuwapa pongezi raia kuwa wamekubali asili yao kwasababu wameshurutishwa kuishi hivyo.
Huu ndo ukwel mchungu watu hawautaki kuusikia aisee

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Huwa nikiona maelfu ya watu kila siku toka nchi za Amerika ya Kusini na kwingineko duniani wanavyolazimisha kuingia Marekani, huwa najiuliza, inakuwaje nchi inayosemwa kwamba ni mhimili wa Ushetani duniani inagombaniwa na watu kwenda kuishi.

Huoni harakati za watu kwenda kwenye zile nchi zenye "Ustaarab" au za "wacha Mungu" kuliko harakati zinazofanywa na watu kwenda kuishi Marekani. Kwa nini watu wanang'ang'ania kwenda kwenye nchi inayoitwa ya kidhalimu?
Marekani sio nchi ya kishetani Ila kuna watu wanatumia nguvu aliyonayo marekani kuoneza agenda za kishetani.so marekani kuna watu wa Mungu na pia watu wa shetani.
 
Huwa nikiona maelfu ya watu kila siku toka nchi za Amerika ya Kusini na kwingineko duniani wanavyolazimisha kuingia Marekani, huwa najiuliza, inakuwaje nchi inayosemwa kwamba ni mhimili wa Ushetani duniani inagombaniwa na watu kwenda kuishi.

Huoni harakati za watu kwenda kwenye zile nchi zenye "Ustaarab" au za "wacha Mungu" kuliko harakati zinazofanywa na watu kwenda kuishi Marekani. Kwa nini watu wanang'ang'ania kwenda kwenye nchi inayoitwa ya kidhalimu?
Wewe ndio hujui wanaokimbilia huko wengi ni wale wenye hulka za kishetani pepo ipo Africa
 
Hata kina mudi kila siku wanakimbilia huko

Wachina
Warusi
Wahindi
Waarabu

Hawa wengi hukimbilia Marekani
Kwani wananchi wanasemaje

California School District Votes in Favor of Keeping a Child’s Gender Transition Status from Parents​

...a mother who is currently suing the district. Regino alleged that a school counselor facilitated her 11-year-old daughter’s transition without her consent.

Comments

a.jpg

a1.jpg

b.jpg

d.jpg

e.jpg

c.jpg

Na huku

A new bill passed in the state of Washington seeks to undermine parental rights by allowing “shelters” to provide gender transition medical services to minors without parental consent

Endelea tu kishupaza shingo, shauriyako!
Bado hujathibitisha.

Yani hata mimi kushupaza shingo ni ushahidi Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo, wote tungejua hilo bila utata na kushupaza shingo kusingewezekana.
 
ACHA UJINGA, thibitisha kwamba mungu hayupo
 
ACHA UJINGA, thibitisha kwamba mungu hayupo
Kisichopo, nje ya thibitisho za kidhahania, hakithibitishiki kwamba kipo au hakipo, kwa sababu hakipo, na kama hakipo, hakithibitishiki, kwa sababu ili kithibitishike, nje ya hoja za dhahania, inabidi kiwepo.

Kwenye thibitisho za kidhahania, kama "proof by contradiction", Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, anathibitishika kwamba hayupo, kwa sababu dhana ya kuwepo kwake inakuwa contradicted na ulimwengu tunaouona ambao unaruhusu mabaya.

Ama Mungu huyo yupo na ulimwengu unaorusu mabaya haupo.

Ama ulimwengu unaoruhusu mabaya upo na Mungu huyo hayupo.

Mawili haya hayawezi kuwapo kwa pamoja.

Tunaona ulimwengu unaoruhusu mabaya upo.

Hivyo, Mungu huyo hayupo.

Angaia Epicurean Paradox, halafu uitatue kama utaweza.

epicurean_paradox.jpg
 
Huwa nikiona maelfu ya watu kila siku toka nchi za Amerika ya Kusini na kwingineko duniani wanavyolazimisha kuingia Marekani, huwa najiuliza, inakuwaje nchi inayosemwa kwamba ni mhimili wa Ushetani duniani inagombaniwa na watu kwenda kuishi.

Huoni harakati za watu kwenda kwenye zile nchi zenye "Ustaarab" au za "wacha Mungu" kuliko harakati zinazofanywa na watu kwenda kuishi Marekani. Kwa nini watu wanang'ang'ania kwenda kwenye nchi inayoitwa ya kidhalimu?
Jiulize ni kwanini watu wanapenda sana mambo ya kishetena. Hata wewe huo uzinzi unaoupenda ni Shetani huyo. Shetani huvutia ilimradi tu atimize huo ushetani wake
 
Back
Top Bottom