Kama misikiti inaweza kujengwa mitaani kwa uhuru, kwanini kujengwa kwa makanisa kuwe kero Zanzibar?

Duh Kwa kweli kama tumefika huko hii itakua chuki kubwa Sana mama Samia amiri jeshi mkuu kemea hili lisizae mizizi
Ninakumbuka yule aliykanyaga quruan Kilosa alishughulikiwa haraka sana. Ila kubomolewa kwa kanisa si tatizo.

Makanisa yanapiga kelele ila yale mavipasa sauti ya msikitini siyo tatizo.

Iko siku kisasi kitalipwa.
 
Hili suala la wazanzibari kutotaka ukristo visiwani humo iingia rasmi kama Kero jipya ya Muungano.
 
Aliekwambia serekali haina dini nani ? Zanzibar wakaazi wake wa kiislamu lakini skuli zinafuata kalenda ya kikristo na wala hawajalalmika miaka yote wakati wao ndio majority....
Hapo ndio kutakua na shida zaidi na hujafikiria sawasawa.

Una maana sehemu ambazo huku bara Kuna wakristo wengi mtaani , hakupaswi kujengwa msikiti?
 
Aliyewaambia wazanzibari wanahitaji makanisa ni nani?

Wazanzibar 99% ni waislamu hata hiyo misikiti iliyopo sasa haitoshi..

Hivyo anayehitaji kujenga nyumba ya ibada Zenji ajenge Msikiti ili kuCover mahitaji sahihi.

Unajenga kanisa la Tsh mil 100 halafu waumini wawili hiyo ni wastage of resources..

Eboo..!
 
Wanapotoshaje? Wewe si ushike Imani yako? Nyie huwa sijui mnawazaga vipi wenzetu
Ndio maana mkifunga ramadhani hamtaki watu wengine wale mchana, eti watawatamanisha. Wtf......??
 
Hili Swala inabidi tuliendee bila kutumia hisia,nani hajui KERO ya makanisa ya kilokole yaliyotapakaa kila Kona ya nchi hii,kwa wakazi wa Dar,pale kawe Kuna makanisa kila Kona...
Tafakari pia haya;
-Hivi vile vipaza sauti vya misikiti vinavyopiga adhana alfajiri, adhuhuri, Alasiri, jioni na usiku huwa waviwapi kero wakristo au wapagani?

-Hivi ni misikiti mingapi huku kwenye mitaa ya Zanzibar ilijengwa kwa kibali?

-Hivi ni mamlaka gani ya SMZ itakupa kibali ujenge kanisa mitaani?

-Ni mamlaka gani iliyotoa kuvunjwa kwa hilo kanisa kwa sababu limejengwa bila kibali?
 
Mimi naona huyo jamaa aliyejenga kanisa hapo hakufanya sawa. Kwasababu asilimia 98 ya wazanzibar ni waislam. Ni hatari hata kwa maisha yake japo gharama ya ukristo ni zaidi ya uhai na mali. Kuna vitu vingine unatumia tu common sense na kupotezea.
Bado sijapata mantiki ya hoja yako.

Kosa ni kujenga kanisa kwenye waislamu wengi? How?

Wewe ulitaka ajenge wapi kanisa hapa Zanzibar?

Ni vipi uislamu uhatarishe maisha ya waumini wa kikristo hapa Zanzibar?

Nini mantiki ya kuwa na Uhuru wa kuabudu na uvumilivu wa kiimani unaotaja na kutafsiriwa katika katiba?
 
hawa wazanzibar ni wapuuzi Sana, 2010 niliwahi kushushwa kwenye gari zao za chai maharage bila sababu yoyote kisa tuu nimemuongelesha msichana aliyekuwa ameketi kando yangu kumuulizia kitu ninachoenda kushukia.


pia sokoni hapo darajani lijamaa limoja lilikataa kuniuzia mashine ya kukamua juisi ya miwa, mpaka nilitafuta mzanzibar akanisaidia kununua Kwa niaba yangu.
 
Wazanzibari wameukataa huu uhayawani wa makanisa haya feki.
Inashangaza huku Bara mtaa mmoja kuna makanisa matano!
Makanisa ni mengi kuliko waumini,matokeo yake ni makelele tu mitaani.
Kingine majority ya Wazanzibari ni waislam na huu ni ukweli ulio wazi.Hatuwezi kulazimisha Wazanzibari waishi kinyume na Utamaduni wao.

Jambo linalonishangaza Zanzibar,Sheria hizi na tofauti za Utamaduni haziwabani WAZUNGU kufanya watakavyo.
Mwezi mtukufu ukiwa na Ngozi nyeusi huwezi kula mahala popote Zanzibar,hata hoteli za nyota tatu au nne nilizowahi kutembelea nilinyimwa hata kuuziwa soda tu!
Lakini wazungu wanapata ulabu bila wasiwasi!.This is tantamount to slavery!

Tupo kwenye “Nchi” yetu lakini unabaguliwa na Mzungu wanamtukuza!
Beach wazungu wanakaa uchi lakini mtaani Mwanamke aliyeumbika akivaa nguo wao wanayoiona sio sahihi wanampiga na kumdhalilisha!
Sielewi mantiki yake!!.
Wazanzibari wana mambo ya ajabu sana,inahitaji moyo kuishi nao vizuri,unahitaji kuwa zaidi ya bwege ili uende nao sawa.
Ni ngumu kujifanya bwege kama wewe sio bwege,hasa ukiwa katikati ya mabwege.Bora uwe bwege kwa wenye akili.
Cha msingi tuwaache na Maisha yao.
 
OK OK OK enough! naona engi wanakuja hapa na kelele za kutaka Samia aingilie kati etc etc. Kwanza niwajuze suali la ardhi na majenzi haliko katika muungano kwa hivyo Samia hana ubavu katika suali la serikali ya zanzibar. Mkitaka mabadiliko kwanzabadilini katiba, muingize suali la ardhi na majenzi katika muungano, jambo ambalo hatutolikubali NG'O!!!!!

Pili duniani kote huibuki tu ukanunua kiwanja na kujenga unachotaka, ni lazima upate kibali. Kadhalika duniani kote wakaazi wa sehemu huwa wana haki ya kupinga ujenzi wa aina yeyote ile katika sehemu zao wanazoishi. Ndio maana daima kunakuwepo uwasilishwaji wa maombi na kufuatiwa consultationust kabla ya kukubaliwa ua kukataliwa kwa project yeyote ile. Just because tanzania na nchi nyingi za afrika serikali hutumia ubavu na kufanya walitakalo, haimaanishi ni kosa kwa serikali kusikiliza na kukubaliana na pingamizi za wananchi wake.

Zanzibar wananchi wake wengi ni waisilamu na hatuhitaji makanisa kila mahali. hatupingi kujengwa kwa makanisa tu, bali pia tunapinga kujengwa kwa bars na night clubs katika kila pembe ya visiwa vyetu. Kubaliana nasi au usikubaiane nasi, huo ndio msimamo wetu. Mna hiari zenu huko kwenu lakini sio kwetu.
 
Mjomba unatakiwa urudi shule..maana unaonkana hata elimu huna na hujaelemika sasa mtu akifundishwa kiingereza ndo anakua amejua biblia..?
 
Wanapotoshaje? Wewe si ushike Imani yako? Nyie huwa sijui mnawazaga vipi wenzetu
Ndio maana mkifunga ramadhani hamtaki watu wengine wale mchana, eti watawatamanisha. Wtf......?

Ni shida sana kujaribu kumfahamisha mtu ambae hafahamu dini yetu na ni vigumu zaidi ikiwa anaeuliza hataki kufahamishwa bali anataka kubishana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…