Kama misikiti inaweza kujengwa mitaani kwa uhuru, kwanini kujengwa kwa makanisa kuwe kero Zanzibar?

Kama misikiti inaweza kujengwa mitaani kwa uhuru, kwanini kujengwa kwa makanisa kuwe kero Zanzibar?

Ombeni vibali rasmi vya eneo la kanis muone kama mtakataliwa. Kwanini mkajenge makanisa uswahilini? Kwani hamna akili?
 
F
Hizi dini faida yake kubwa ni ukifaulu kuingia huko zilikoahidiwa!

Hapa duniani kumzuia mwemgine asieneze dini yake, huo ni upumbavu wa jinsi dini ilivyoegemea dunia kuliko kuleee ilikoelekezwa watu wake wafike!

Huu upuuzi unaletwa na ujinga mwingi usio malizwa na elimu dunia!
Mimi staki dini lako, kwa nini usiniache niwe na Uhuru wa dini yangu.??

Upuuzi mtupu
Na nyie wenye dini muache kuleta vurugu za kila namna kwenye makazi ya watu.

Mlipata eneo linalofaa, kisha mkaomba kibali cha ujenzi wa kanisa mkakataliwa?

Muache kufanya ujinga ujinga wa kumdhalilisha Mungu kwa vurugu zenu. Mungu ni wa kumheshimu, siyo unachukua mabati chakavu unasema kanisa.
 
Zanzibar ni nchi ya waislam kama hawataki mueneze ukristo huko Zanzibar sawa tuu nchi yao maamuzi yao.
 
Wazanzibari wameukataa huu uhayawani wa makanisa haya feki.
Inashangaza huku Bara mtaa mmoja kuna makanisa matano!
Makanisa ni mengi kuliko waumini,matokeo yake ni makelele tu mitaani.
Kingine majority ya Wazanzibari ni waislam na huu ni ukweli ulio wazi.Hatuwezi kulazimisha Wazanzibari waishi kinyume na Utamaduni wao.

Jambo linalonishangaza Zanzibar,Sheria hizi na tofauti za Utamaduni haziwabani WAZUNGU kufanya watakavyo.
Mwezi mtukufu ukiwa na Ngozi nyeusi huwezi kula mahala popote Zanzibar,hata hoteli za nyota tatu au nne nilizowahi kutembelea nilinyimwa hata kuuziwa soda tu!
Lakini wazungu wanapata ulabu bila wasiwasi!.This is tantamount to slavery!

Tupo kwenye “Nchi” yetu lakini unabaguliwa na Mzungu wanamtukuza!
Beach wazungu wanakaa uchi lakini mtaani Mwanamke aliyeumbika akivaa nguo wao wanayoiona sio sahihi wanampiga na kumdhalilisha!
Sielewi mantiki yake!!.
Wazanzibari wana mambo ya ajabu sana,inahitaji moyo kuishi nao vizuri,unahitaji kuwa zaidi ya bwege ili uende nao sawa.
Ni ngumu kujifanya bwege kama wewe sio bwege,hasa ukiwa katikati ya mabwege.Bora uwe bwege kwa wenye akili.
Cha msingi tuwaache na Maisha yao.

Wewe Bwege, mbona unasema maneno ya kibwege sana. Unafikiri kila mmoja ni bwege kama wewe. Embu acha huo ubwege
 
Ukiishi Roma,
behave Kama waroma.

Uhuru kwa mgeni ni ruksa,
Ila Uhuru wako unapohatarisha usalama wa Mila,desturi,utamaduni na ustaarabu wa wenyeji husika unakua HAUFAI.

Zanzibar haijawai kua ya makanisa.
Mtoa mada huna hoja Hapa.

Nb: Mimi Ni mkristo na mtanzania bara[emoji4]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada,
Unapaswa ujue kua zanzibar Wana katiba yao.

Na katiba Yao haina mahali pamendikwa habar za makanisa, parokia, shemasi Wala askofu.

Katiba Yao iko Islamic based,
Kwaiyo unaponukuu vifungu vya katiba yao, usiifananishe na ya huku bara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeshuhudia taarifa na video mtandaoni ikionyesha kanisa dogo la TAG maeneo ya Zanzibar likivunjwa na greda kwa amri ya wakuu fulani wa serikali wa Zanzibar.

Sababu za kimsingi za hayo kutokea ni kukosekana kwa uvumilivu wa kidini kwa baadhi ya wakazi wa Zanzibar dhidi ya imani zingine, jambo ambalo linalindwa na watawala wa Zanzibar kwa miongo yote. Japokuwa wakuu wa serikali huko Zanzibar wamekuja na sababu nyingine duni na kijinga (wanadai wamevunja kanisa hilo kwa sababu za taarifa za kitisho cha hali ya hewa kuhusu mvua inayoweza kuleta mafuriko maeneo hayo!)

Tunapaswa kutambua haya.
1. Karibu mitaa yote ya Zanzibar kuna misikiti mikubwa au midogo.

2. Karibu misikiti yote ya Zanzibar ina vipaza sauti (horn speaker) zinazopiga adhana kila siku kutwa mara tano.

3. Karibu misikiti yote ya Zanzibar imejengwa kwenye makazi ya watu au jirani kabisa na makazi ya watu.

4. Mpaka sasa Zanzibar haina maeneo rasmi ya wazi yaliyotengwa mahususi kujenga nyumba za Ibada tu na kujulikana kwa watu wote.

5. Serikali ya Zanzibar na serikali ya Tanzania kikatiba zote hazina dini na hazipaswi kufuata mlengo wa imani yoyote ya kidini zaidi ya kuheshimu na kulinda uhuru wa imani zote.

MAMBO MUHIMU YA KUTAFAKARI
-Kwanini kuwe na shida kila mara dhidi ya taasisi za kikristo zinapotaka kujenga makanisa, kuabudu kwa uhuru au kueneza imani yao maeneo ya Zanzibar?

-Kwanini Serikali ya mapinduzi Zanzibar na serikali ya muungano zinashindwa kulinda uhuru wa kuabudu kwa wakristo waliopo Zanzibar?

-Kwanini jamii za imani ya kikristo zionekane kama ni wavamizi, wapitaji na wageni waliokosa mwenyeji kila mara huko Zanzibar?

TAFAKARI
Asante umeandika vema sana
 
Naona kuna tatizo hapa, masharti vigezo, desturi, imani na tamaduni haikuzingatiwa.

Unaweza kumiliki eneo lakini kuna masuala mtambuka ambayo mnunuzi hakuyazingatia akayaona ni mepesi, kumbe kuna mengine hayaandikwi lakini yanafuatwa na jamii husika wakaazi wenyeji wa mwanzo kabisa .


Serikali inaongozwa na watu, ila watu hao wana imani, desturi, tamaduni pia taratibu zao hivyo mtu makini hawezi kupuuza yale ambayo hayajaandikwa katika katiba.



Mfano hai wa babu zetu wanaelezea umuhimu wa utamaduni wao na unavyowasaidia kuishi wao kama jamii kwa amani


Sahii kabisa,
Ndo Maana zbc Ni televisheni ya taifa.

ila kamwe hawawezi kurusha mahubiri ya kilokole Wala wakristo.

Utaona wanarusha wamawaidha ya kiislamu TU

Watanganyika tumeridhika na tunaheshimu maamuz yao.

Mtoa mada hana Nia nzur na mila na desturi za wanzibar, na yeye ndio anayeanzisha hizi chokochoko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada anatafuta TU chokochoko kwny mila,desturi na tamaduni za watu,

Wee umewahi kuskia wapi mzanzibar mkristo, achilia mbali mlokole wa TAG?[emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zanzibar msikiti wanachukulia kama bar kupata kibali jasho litakutoka.
 
Back
Top Bottom