Kama misikiti inaweza kujengwa mitaani kwa uhuru, kwanini kujengwa kwa makanisa kuwe kero Zanzibar?

Kama misikiti inaweza kujengwa mitaani kwa uhuru, kwanini kujengwa kwa makanisa kuwe kero Zanzibar?

Ndio wanachokofanya huko moshi, kuna sehemu ukitaka kujenga msikiti wakikubaini tu biashara imeishia hapo
Acha uongo na unafiki, misikiti imejengwa toka enzi na enzi huko Kilimanjaro pasipo tatizo lolote. Kuanzia Same, Mwanga, Rombo, Moshi, Siha na Hai kote huko kuna misikiti na taasisi kubwa na nzuri za kiislamu pasipo tatizo lolote na watu wanaishi fresh sana.

Mwaka juzi nilifika huko na kujionea mimi mwenyewe kwa macho yangu. Wakazi wa kule ni wastaarabu mnoo linapokuja suala la uvumilivu wa kiimani.
 
Mimi naona huyo jamaa aliyejenga kanisa hapo hakufanya sawa. Kwasababu asilimia 98 ya wazanzibar ni waislam. Ni hatari hata kwa maisha yake japo gharama ya ukristo ni zaidi ya uhai na mali. Kuna vitu vingine unatumia tu common sense na kupotezea.
Makanisa hapo hadi Saudia, isitoshe Zanzibar.
 
akina zumaridi nao wajenge makanisa yao. Uhuru wa kupitiliza hauna maana. makanisa yaliyopo hamjajaza mnajenga makanisa mengine ya nini
Makanisa yanakuhusu nini wewe sheikh ?
 
Saudi Arabia ni taifa la kidini la Kiislamu, Tanzania ni taifa lisilo na dini. Hujui haya mpaka leo?!
Sahii kabisa,
Ni sawa uende ukauze kiti Moto siku ya kuhiji kule MECCA ukitegemea sheria ya free trade ya umoja wa mataifa itakulinda endapo madhira yakikukuta[emoji28]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Saudi Arabia ni taifa la kidini la Kiislamu, Tanzania ni taifa lisilo na dini. Hujui haya mpaka leo?!
Kwahiyo unajisahaulisha kuwa hujui Zanzibar ni nchi yenye Rais wake na katiba yake?
 
Zanzibar ni nchi ya kiislam, hivi ktk nchi ya vatican kuna msikiti hata mmoja tuu?
 
kuna mwenzako kaja na thread kma hii hlf akaleta updates kua Uyo alouziwa kiwanja kwenye makubaliano walisema ni kiwanja cha makazi yy akajenga kanisa wakamwambia kuhusu makubaliano akakataa na kma huyajui makanisa ya TAG ulizia vzr jinsi yanavopiga zogo usiku na mchana

Sasa usielemee upande mmoja tafuta ukweli na uhakika kwanza usijepotosha wengi kwa chuki zako na serikali.

Nawasilisha
Bado sijaona tatizo kuhusu makubaliano ya aliyeuza na kuuziwa, na ikiwa kuna shida basi jibu lingekuwa ni kwenye vyombo vya sheria.

Ngoja nifafanue kidogo hapa.
Kikubwa mauziano yalifanyika kwa njia halali na kila mtu kupata haki yake hivyo sioni mantiki kwa muuzaji kutaka kulazimisha namna ya kulitumia hilo eneo wakati umiliki hauko tena mikononi mwake.

Pili shida sio nyumba ya ibada kuwepo maeneo ya makazi ya watu (kwa Zanzibar zaidi ya 90% ya nyumba za ibada ziko karibu kabisa na makazi ya watu), shida ni wakazi wa hilo eneo kukosa uvumilivu wa kidini dhidi ya kanisa lililojengwa hapo.
 
Zanzibar ni nchi ya kiislam, hivi ktk nchi ya vatican kuna msikiti hata mmoja tuu?
Nani kasema Zanzibar ni nchi ya kiislamu?
Toka lini Zanzibar imekuwa nchi ya Kiislamu?
Nchi za kiislamu ni kama Misri, Algeria, Tunisia, Saudi Arabia (Maka na Madina) na kote huko makanisa yapo na wakristo wapo.
Vatican ni nchi ndogo sana (infact ni kasehemu tu ndani ya Italy kalikopewa mamlaka yake ya ndani) na sina uhakika utaratibu wa kidini ukoje kwa imani zingine tofauti na Ukatoliki.
 
Acha uongo na unafiki, misikiti imejengwa toka enzi na enzi huko Kilimanjaro pasipo tatizo lolote. Kuanzia Same, Mwanga, Rombo, Moshi, Siha na Hai kote huko kuna misikiti na taasisi kubwa na nzuri za kiislamu pasipo tatizo lolote na watu wanaishi fresh sana.

Mwaka juzi nilifika huko na kujionea mimi mwenyewe kwa macho yangu. Wakazi wa kule ni wastaarabu mnoo linapokuja suala la uvumilivu wa kiimani.
Kwani zanzibar hakuna makanisa? Iweje hilo libomolewe? Hata moshi kunasehemu jamaa alinunua eneo akataka kujenga msikiti kilimkuta kilichomkuta huyo wa znz
 
Mbumbumbu ni wewe usiyefahamu Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni taifa lisilo la kidini.
Sasa ngoja nikupe shule kidogo bwanamdogo. Tanzania inaundwa na nchi 2 zilizo huru kabisa. Zanzibar na Tangayika . Katika muungano yapo masuala ya muungano na yasiyo ya muungano katika uendeshaji wa serikali ( Nenda kayatafute uyasome). Suala la Tanganyika kuvaa koti la muungano siyo ticket ya kuingia zanzibar na kuharibu mila na desturi za watu wa Zanzibar. Kwanini tusijivunie utanganyika wetu kama wazanzibari wanaojivunia uzanzibari wao? Mila zetu sisi ni mchanganyiko kula kiti moto, makanisa mengi ya kina mfalme zumaridi n.k, uislam pia upo tanganyika. Lakini kwa zanzibar ni tofauti na hawataki sasa kwanini kulazimishana?
 
Tatizo la waislamu majini yao hayapatani na jina la Yesu Kristo. Likitajwa wanaungua moto. Na ukumbuke waislamu wengi wanaishi na majini na wengi ndiyo chanzo cha vipato.
Ongea na toa haja kama great thinker.

Binafsi, nimezaliwa familia ya kiislam. Lakini, sipokei masuala ya kiimani kibubusa. Kwangu mimi hilo la suala la makanisa Zanzibar ni uonevu wa muda mrefu. Na kusema kweli hawatendi haki kwa waumini wasio waislamu.

Pili, serikali kwa kweli ingepiga marufuku matumizi ya loudspeakers kwani imekua kero. Na hili ni kwa upande wa haya makanisa ya kilokole na adhana. Nchi yetu nyumba za ibada zipo mazingira ya watu, suala la makelele ni la kudhibitiwa bila kuogopa waumini watachukuliaje.
 
Nani kasema Zanzibar ni nchi ya kiislamu?
Toka lini Zanzibar imekuwa nchi ya Kiislamu?
Nchi za kiislamu ni kama Misri, Algeria, Tunisia, Saudi Arabia (Maka na Madina) na kote huko makanisa yapo na wakristo wapo.
Vatican ni nchi ndogo sana (infact ni kasehemu tu ndani ya Italy kalikopewa mamlaka yake ya ndani) na sina uhakika utaratibu wa kidini ukoje kwa imani zingine tofauti na Ukatoliki.
Kwahiyo unataka kusema Vatican siyo nchi?
 
Ninakumbuka yule aliykanyaga quruan Kilosa alishughulikiwa haraka sana. Ila kubomolewa kwa kanisa si tatizo.

Makanisa yanapiga kelele ila yale mavipasa sauti ya msikitini siyo tatizo.

Iko siku kisasi kitalipwa.
Na hili ndiyo nalolikemea.
Mimi bado lawama zangu ni kwa serikali.
Mambo hayako regulated, sijui wanaogopa nini hasa?
Maadam wameshindwa kupangilia makazi ya watu na nyumba za ibada, basi waangalie nukta ya noise pollution bila kuogopa imani za watu. Binafsi, sipingi nyumba za ibada kuwa kwenye makazi ya watu, nachopinga ni makelele maana kwangu mimi hizi ndiyo hasa usumbufu wenyewe.
Ningekua na mamlaka, ningedhibiti loudspeakers misikitini na makanisa ya kilokole. Period!
 
Aliyewaambia wazanzibari wanahitaji makanisa ni nani?

Wazanzibar 99% ni waislamu hata hiyo misikiti iliyopo sasa haitoshi..

Hivyo anayehitaji kujenga nyumba ya ibada Zenji ajenge Msikiti ili kuCover mahitaji sahihi.

Unajenga kanisa la Tsh mil 100 halafu waumini wawili hiyo ni wastage of resources..

Eboo..!
Mkuu unaposema hivyo unakosea.

Ina maana hakuna watu waliotoka huku bara wanafanya kazi Zanzibar ambao si waislam?

Hakuna watalii wanaoingia Zanzibar ambao wanahitaji kuabudu? Kwahiyo unamaanisha Zanzibar haina muingiliano? Shughulisha ubongo kabla ya kuandika
 
Back
Top Bottom