Kama mlikuwa hamjui: CCM imeliongoza hili Taifa kwa uongo tangu ikiwa TANU hadi sasa.

Kama mlikuwa hamjui: CCM imeliongoza hili Taifa kwa uongo tangu ikiwa TANU hadi sasa.

Wewe Mayor Quimby una sifa za kusifia unachokiponda, nakumbuka kuna nyuzi ulimsema sana Saa100 ukakaa siku 3 nyingi ukaja na nyuzi nyingine ya kumsifia saa100 najiuliza hivi huyu kichwa chake kina matatizo gaani? Lord denning ukimsoma nyuzi zake za kitambo humu ni kuisifia CCM mwanzo mwisho sasa hivi kajivika mabomu anailipua CCM, sasa atakapobadirisha upepo lazima niruke nae maana mnazengua
Ni bendera, fuata upepo!
 
Ni zaidi ya Sahihi. Haya mambo yote hayawezi kutokea kwenye nchi yenye mifumo imara ya checks and balance.

Hatuna budi kubadili Katiba yetu kuhakikisha tuna mifumo imara na kurekebisha Sheria zetu za Uchaguzi ili tupate Viongozi wanaowajibika kwa Wananchi.
Na wengi wanatetea sio kwamba hawajui!,Ni wapiga debe tuu hata humu WAMO, Tlaahtlaah na nduguye Mwashambwa!
 
We umesahau Lissu alipoibua issue ya Hati ya Muungano kwenye Bunge la Katiba hadi watu wakaenda kuitengeneza?

Hii nchi ni vile tu vilaza wengi ila tungekuwa na akili CCM wasingetakiwa kuwepo kabisa madarakani.
Kofia na t-shirt zinatuponza!Ndio maana mdau mmoja humu alianzisha mada Moja,ili sm iondoke,watu waliozaliwa miaka ya 1960_1977,Wanatakiwa waondoke ili kizazi kipya kitawale,ila alituonea sio wote wenye mawazo ya kiesm!
 
Miaka 2 iliyopita ulimalizika mradi mkubwa wa kujenga nji a ya umeme kutoka Singida kwenda Arusha.Tuliaminishwa pia kuwa njia hii itaongeza kama sio kuondoa tatizo la umeme Mikoa ya Kaskazini!😭
Kumbe sakata la Simba kugomea mechi juzi halikuwa la bahati mbaya!
Umepiga kona kali sana hapo!
 
Kofia na t-shirt zinatuponza!Ndio maana mdau mmoja humu alianzisha mada Moja,ili sm iondoke,watu waliozaliwa miaka ya 1960_1977,Wanatakiwa waondoke ili kizazi kipya kitawale,ila alituonea sio wote wenye mawazo ya kiesm!
Ni ujinga tu. Ila ni lazima siku itafika tutaandika upya historia ya nchi yetu
 
Amini maneno yangu. Nchi yetu shida ya umeme haitokuja kamwe kupungua au kuondoka kabisa as long as tunategemea vyanzo vya maji.

China pamoja kuwa na Mabwawa mengi ya Umeme alafu bado anazalisha Umeme wa Nyuklia sio wajinga.

Mataifa ya Marekani, Canada, Uingereza na mengine makubwa kuanza tena kuwekeza kuzalisha umeme wa nyuklia sio wajinga.

Sie tuna madini ya Uranium Bahi na Lindi pale ila haujawahi kusikia hata siku moja wajinga wa CCM hata wakiongelea Jmeme wa nyuklia wakati Kenya tu hapo juu amepata kibali cha kuanza kutengeneza Umeme wa Nyuklia na sasa anahamisha watu kwenye moja ya Pwani zake ili aanze ujenzi wa mradi huo.
Bila kupuuza tatizo la miundombinu ya uchakataji na usafirishaji wa umeme unaozalishwa. Hili nalo bado ni kubwa sana. Serikali haijafanya uwekezaji wa kutosha huko kwa miaka mingi.
 
Bila kupuuza tatizo la miundombinu ya uchakataji na usafirishaji wa umeme unaozalishwa. Hili nalo bado ni kubwa sana. Serikali haijafanya uwekezaji wa kutosha huko kwa miaka mingi.
Still hilo halijustify kununua umeme kutoka Ethiopia wakati viongozi wetu wanajisifu Bwawa kushusha bei ya umeme na nchi kuzalisha umeme zaidi ya kiwango tunachotumia.
 
Still hilo halijustify kununua umeme kutoka Ethiopia wakati viongozi wetu wanajisifu Bwawa kushusha bei ya umeme na nchi kuzalisha umeme zaidi ya kiwango tunachotumia.
Sikuwa nahalalisha bali naongezea hoja yako ya mambo YASIYOSEMWA yanayokwamisha upatikanaji wa umeme nchini.
 
Lord denning.
Umechanganyikiwa. Hakuna anaye weza kukusaidia utaishi maisha yako yote kama kichaa kichaa vile, bila kujua unasimamia wapi!
Wewe ni mtu asiye kuwa na umakini juu ya jambo lolote lile. Unayumba yumba tu.
You have an ectopic mind. Mara akili imo tumboni, mata makalioni, na wakati mwingine inaonekana kuwa mahala pake sahihi, kichwani!
 
Kwa nini mkuu? Nani kakwambia sina pa kusimamia?
 
Wewe Mayor Quimby una sifa za kusifia unachokiponda, nakumbuka kuna nyuzi ulimsema sana Saa100 ukakaa siku 3 nyingi ukaja na nyuzi nyingine ya kumsifia saa100 najiuliza hivi huyu kichwa chake kina matatizo gaani? Lord denning ukimsoma nyuzi zake za kitambo humu ni kuisifia CCM mwanzo mwisho sasa hivi kajivika mabomu anailipua CCM, sasa atakapobadirisha upepo lazima niruke nae maana mnazengua
Huyo itakua kanyanganywa tonge mdomoni.sasa hivi anajifanya kuponda.Watu vigeugeu ni hatari sana.kwasababu mara nyingi wako kwa maslahi binafsi.
 
Huyo itakua kanyanganywa tonge mdomoni.sasa hivi anajifanya kuponda.Watu vigeugeu ni hatari sana.kwasababu mara nyingi wako kwa maslahi binafsi.
Hunijui vizuri wewe!

Nifuatilie vizuri humu JF utaona mwenye Lord denning ni nani? Mie ni mzalendo kweli niliye kwa maslahi ya Taifa na sio yangu.

Pia nina kipato changu cha uhakika huku ughaibunikoa hata sijawahi kufikiri kufanya kazi za kuteuliwa na hao Wanasiasa sasa nimenyang'anywa Tonge gani?
 
Ni vile tu Watanzania wengi ni wajinga na sio wasomaji sana wa vitabu na wafuatiliaji wa masuala ya nchi yao.

Mlioshtuka leo kuhusu habari ya Tanzania kununua umeme nje kwa ajili ya matumizi ya mikoa ya Kaskazini wakati Serikali imekuwa ikijisifu kuzalisha umeme kuzidi matumizi yetu nawashangaa sana.

Kwa wale msiofahamu hakuna Chama cha siasa Afrika hii na nadhani duniani kinachoishi kwa uongo kama CCM. Na uongo wa CCM haujaanza leo, ulianza tangu ikiwa TANU na uliasisiwa na aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Tanganyika na Tanzania , Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Vitabu vya dini vinasema Shetani ni Baba wa Uongo ila kwa hapa Tanzania, baba wa uongo ni CCM.

Yafuatayo ni maeneo ambayo TANU na CCM waliwadanganya/Wamewadanganya Watanzania na wao wakaamini.

1. Suala la Oscar Kambona kutangazwa kuwa mhaini na ameolewa Uingereza. Jambo hili lilitangazwa na Serikali ya Nyerere mwaka 1967 baada ya Kambona kuamua kujiuzuru nafasi zote za Uongozi ndani ya Serikali na Chama baada ya kupingana na Nyerere kuhusu sera za Ujamaa. Watanzania kama mazuzu tuliamini huu uongo wa Nyerere na hadi tukatungishwa nyimbo mashuleni kuwa kambona Kaolewa Uingereza. Huu ulikuwa uongo wa Nyerere ili kuwarubuni Watanzania na kuwa label vibaya wanaompinga.

2. Suala la Nyerere kung'atuka kutangazwa ni kwa sababu eti ni Kiongozi mzuri na hataki kung'ang'ania madaraka. Mwaka 1985 CCM walitangaza na kueneza uongo unaoaminika hadi leo kuwa Nyerere aling'atuka kwa sababu hakuwa na tamaa ya madaraka wakati kiukweli kilichomkimbiza Nyerere ikulu ni mfululizo wa majaribio ya mapinduzi dhidi yake hasa ya mwaka 1981/1982 na lile la kutekwa kwa ndege ya ATCL kutokana na kushinikiza aondoke madarakani kwa sababu ya hali mbaya ya kimaisha/ kiuchumi iliyotokana na kufeli kwa sera zake za ujamaa.

3. Suala la kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 kuwa ni busara za Nyerere wakati ukweli ni kwamba baada ya kuanguka kwa Shirikisho la Kikokumunisti (USSR) nchi zote zilizokuwa zinaitegemea Urusi ziliamua kuchukua sera zinazofanana na za kimagharibi ili kuendelea kupata misaada kutoka Mataifa ya Magharibi.

4. Suala la Nyerere kuwa alikuwa kiongozi bora na hakuwa dikteta wakati kiuhalisia hakuna Kiongozi aliyekuwa dikteta nchi hii kama Mwalimu Nyerere. Kipindi cha Uongozi wake ndipo Watanzania wengi waliotofautiana nae kimawazo kama kina Bibi Titi Mohamed na Oscar Kambona walifunguliwa kesi za Uhaini na wengine wengi kuwekwa vizuizini chini ya Sheria ya kuweka watu kizuizini. Waliopona wachache walikimbia nje ya nchi na kurudi baada ya Nyerere kuondoka madarakani.

5. Suala la vita vya Uganda kuwa ilitokana na Iddi Amini kutaka kuuchukua mkoa wa Kagera wakati ukweli ni kwamba ugomvi wa Iddi Amini na Nyerere ulitokana na Nyerere kumpa hifadhi Obote aliyepinduliwa na Iddi Amini. Amini aliamini vikundi vinavyompinga ambavyo vingi vilikuwa vinashambulia Uganda kutokea Mkoa wa Kagera nchini Tanzania vinakuwa supported na Nyerere hivyo kuanza kuleta chokochoko mpakani na kuivamia Tanzania.

6. Suala la Corona kutokuwepo Tanzania kipindi cha awamu ya 5 (mwaka 2020/21) wakati kipindi hicho maelfu kama sio mamia ya watanzania walikuwa wanakufa kwenye hospitali zetu kwa ugonjwa wa Corona.

Kutokana na mifano hii michache, napenda kuwaambia Watanzania, CCM hawajawahi kuongoza hii nchi kwa ukweli. Kama wanashangaa leo kuambiwa tutanunua umeme Ethiopia wakati waliambiwa tunazalisha umeme unaozidi matumizi yetu basi watakuwa hawaijui CCM vizuri.

Ukweli uliopo kwenye suala la umeme ni kwamba matumizi yetu yanazidi kuongezeka kila kukicha hivyo hata huo Umeme wa Bwawa la Nyerere hautoshi. Pia pamoja na kuanza kazi kwa Bwawa la Nyerere, mabwawa mengine yanazidi kupunguza uzalishaji kila siku kutokana na kujaa matope na mabadiliko ya tabia nchi yaliyopunguza uwezo wa mabwawa hayo kuzalisha umeme kwa kiwango kinachopaswa. Ila ukweli huu kamwe Watanzania hamtaambiwa mtaletewa uongo wa kila na post za watu mbalimbali kutengeneza hoja uchwara kuutetea huo Uongo (Spinning)

Ikitokea CCM ikaanguka kwenye taifa letu jambo la kwanza watakalotakiwa kulifanya Viongozi wapya wa Tanzania ni kufanya maombi ya toba kwa Taifa kutokana na nchi hii kuendeshwa kwa uongo kwa miongo mingi sana.

Lord denning.

Ndiyo maana bado watu masikini
 
Kwa nini mkuu? Nani kakwambia sina pa kusimamia?
Naona unarudi kule kule kwa mwanzo ulipo ingia JF!
Mada hii ulivyo iweka haina miguu wala kiuno. Kwa mfano: utaiweka vipi kwenye kapu moja hii CCM ya Samia na TANU kwa mfano? Hata CCM ya mwanzo haina uhusiano wowote na CCM hii ya akina Kikwete na wengineo!
 
Tulia soma uelewe ndo utoe maoni yako. Mada inasema kuhusu CCM kuongoza hili Taifa kwa kutumia uongo. Na hili limeanzia tangu kipindi cha TANU.
 
Back
Top Bottom