Kama mnamuona Rais Samia ameshindwa kusimamia Katiba na kulinda rasilimali zenu muwaombe Wabunge wamuondoe kwa Ibara ya 46A ya Katiba

Mungu mwenyewe atamwondoa; hao wabunge ni dhaifu hawajitambui hawawezi kuthubutu kama mbunge mmoja wa Loliondo ameenda kuwatetea wamasai wenzie amekamatwa na polisi iseuze kwa suala hilo?!
 
We unafikir hawataki Katiba mpya kwanini? Katiba ya Warioba iliyosema Rais akipuuza kutekeleza amri ya Mahakama anaweza kuondolewa madarakani! Leo hii mbona Loliondo na Ngorongoro wangekuwa huru katika ardhi yao.
Naliona tatizo la upungufu wa jamii katika kupata habari sahihi, nchi yetu watu wanapewa sana taarifa za kubuni na za uongo na hii inadumaza na kufanya tunaendelea kuwa wajinga wadumu.

Hao Ngorongoro sidhani kuwa awamu ya sita inalo lengo baya, ni masuala ya kuweka hifadhi za kidunia sawa. Siasa zinakuwa nyingi mno Tanzania hii.
 
Hakuna wabunge kuna kusanyiko la vilaza wa CCM tu
 
Unajua mkuu,possibility hiyo ipo kikatiba,lakini Wabunge wetu hawawezi kufanya hivyo, kwa kuwa wanalambishwa asali sana na serikali:hela nyingi za vikao,maV8,mishahara mikubwa,viinua mgongo vikubwa nk.nk.Wee,wanaangalia maslahi, hawathubutu.Bunge la Tanzania sio la Watanzania,ni rubber stamp ya issues za serikali.Tumeliona hili live kwenye sakata la DP World.
 
Wabunge gani unaowazungumzia?
 
Awamu ya sita (tano mhula wa pili) itakumbukwa kwa kutuletea mkataba wa milele,

Yaani mpaka bahari ikauke.
 
Bunge? Bunge la kupita bila kupingwa? Kwenye vyama vingi unapitaje bila kupingwa?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kwa bahati mbaya sikuona mapema comment yako ila kama utaruhusu tuingie kwenye mjadala juu unachokijua nami ninachokikua kuhusu Ngorongoro na Loliondo basi tuingie kwenye mjadala.

Ila wakati tunaingia kwenye mjadala naomba ujue kuwa Waziri alitoa GN Nom 421 mwaka 2022 ya kuongeza ukubwa wa pori tengefu la Loliondo, tangazo ili lilisababisha majeraha makubwa ikiwemo wakazi wa maeneo hayo kupigwa Risasi na kufa na wanyama wao kuuliwa! Serikali ikaenda kuweka bikon kwa mtutu wa bunduki.

Wananchi walijipanga wakaenda kufungua kesi juu ya tangazo ilo la Waziri, J3 Ruling imetoka imesema tangazo la Waziri lilikiuka sheria na hivo batili.

Pia naomba nikukumbushe kuwa katika eneo ilo sheria ya uhifadhi inawatambua wamasai kuwepo katika eneo la Loliondo na inatambua vijiji vilivyopo! Pia tambua kuwa Ardhi ni kiumma na iko mikononi mwa Rais kama mdhamini na sio mmiliki.

Tukisema tuende kisheria Serikali ina makosa sana juu ya kinachoendelea Loliondo na Ngorongoro na hatusemi hivi sababu ya Samia tu ila haya yalianza tangia enzi za Mwinyi na ndiyo maana mzee Mwinyi katika kitabu chake kiitwacho "Safari ya Maisha Yangu" Rais mstaafu Mzee Mwinyi alikiri kuwa alifanya makosa kuuza eneo la pori tengefu la Loliondo! Na hiki ndicho kimesabisha kutesa Wamasai mpaka leo.
 
Serikali iliwajengea hao watu kule Tanga, ikawasafirisha kwa mabasi, ni ardhi ya kutosha tu. Kitu gani kimekuja kubadilika?, ni changamoto pana.
 
Serikali iliwajengea hao watu kule Tanga, ikawasafirisha kwa mabasi, ni ardhi ya kutosha tu. Kitu gani kimekuja kubadilika?, ni changamoto pana.
Kwani wao waliomba Serikali ikawejengee? Unajua athari gani hasi wamekutanazo ata ao walienda Msomela? Unajua eneo la Msomela kwasasa lina migogoro ya ardhi baada ya kuletwa ao Wamasai? Kama walikuwa na nia njema kwanini Serikali wenyewe walishindwa kufuata Sheria ambazo wanazitunga wenyewe?
 
Hata hao wamasai hapo walipo sio kwao pia, ni wavamizi. Suluhisho litapatikana tu.
 
Mjane wa Marehemu. Mimba ya lile shetani lenu la Chato inakusumbua mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…