Nikugeuzie kibao kidogo.
Sasa kwenye hili bandiko mi nataka kufaham kama Mungu hajaumbwa na mungu mwingine kaumbwa na nani? Au kajileta mwenyewe hapa duniani/ulimwenguni? Unajua hata ukiliona gari barabani yupo aliyeunda gari hilo. Waamini, walokole, wakristo,waislam wanaosema mungu hajaumbwa wamejitahidi sana kueleza asili ya Mungu na vitu vingine. Naomba izingatiwe kwamba nataka kufahamu asili ya Mungu sio mwanadamu. Ni kweli muumbaji wa huyo mungu aliyemuumba huyu mungu wanayesema kaumba vitu vingine anaweza akawa hayupo je? Mungu kaumbwa na nani? Uje na lengo la kuelimishana. Nawasilisha.
Mtazamo wa AKILIhuru.
Ukijiangalia wewe pamoja na mazingira yanayokuzunguka ukastaajabu sana isiwe kigezo cha kusema mungu yupo kisa tu umekosa majibu ya baadhi ya vitu!
Kwanini usimtazame huyo mungu na mazingira yake unayoyasoma kwenye vitabu????
Kwa mujibu wa maandiko ujuzi wa maisha ya mwanadamu na mazingira yake haujafikia hata nusu ya ujuzi wa maisha ya huyo mungu.
Sasa jiulize hivi...kwanini ukijiangalia wewe ukastaajabu unasema umeumbwa, lakini ukimuangalia huyo mungu unastaajabu zaidi lakini unasema hajaumbwa. Hii ikoje? Tatizo ni imani za ovyo zimewaharibu.