Notorious_Marcc
JF-Expert Member
- Feb 16, 2024
- 2,598
- 6,147
Hatuwezi kujua tusivyo vijua. Lakini tunaendelea kupunguza tusivyo vijua kwa utafiti, udadisi, uchunguzi na majaribio zaidi.
Sasa wewe eleza ulijuaje Mungu yupo na unathibitishaje uwepo wake?
Usilete imani zako za vitabuni ulizo aminishwa na kupumbazwa.
Eleza ulijuaje Mungu yupo?
Eleza huyo Mungu yupoje?
Kwanza eleza na thibitisha ulijuaje Mungu yupo kabla ya kuendelea na vingine.
Hujaeleza ulijuaje Mungu yupo.
Hujathibitisha Mungu yupo.
Uwezo wa kufanya simu iwe na battery life ya masaa mengi upo. Na inawezekana kufanyika hivyo. Kwa sababu simu imetokana na utaalamu wetu wa kibinadamu.
Sasa tukirudi kwenye suala la "kuzaliwa" Kuna watu hawakupenda kabisa kuzaliwa kwenye hii dunia lakini wakashtukia tayari wameshazaliwa bila kuamua wala kutaka.
Sasa je hiyo ni freewill?
Kwa nini usipewe hiyo freewill mapema kabisa kabla hajazaliwa ili uamue hukohuko uzaliwe ama usizaliwe?
Kwa nini ushtukizwe tu kwa kufanyiwa surprise ya kuzaliwa bila kuamua mwenyewe?
Kwa nini huyo Mungu anashtukiza watu kuzaliwa duniani bila wao kuamua wenyewe?
Huoni kwamba hiyo sio freewill?
Kama that is nature, kwa hiyo habari nzima ya uwepo wa Mungu na freewill haipo.
Hakuna Mungu wala freewill.
The universe is self -existing by its own nature.
Ulijuaje kwamba Mungu ni beyond time, space and matter?
Au unatetea habari za kuaminishwa tu na imani zako za kidini?
Hivi unaelewa maana ya I DON'T BELIEVE?
Nimeshakwambia siamini halafu wewe unasema tena, naamini kwenye kutokuamini?
Hivi una elewa lugha kweli?
You need to restore your brain 🧠 to factory settings.
You need urgent brain reset.
Nilijuaje Mungu yupo?”
Wewe unajua hewa ipo? Unaiona? Unaigusa? Acha kujifanya fundi wa "proof" halafu ukikosa kuona kwa macho, unakataa kila kitu.
Kama akili zako zingewezeshwa kuona frequency zote za existence, ungelia kwa aibu ya ujuaji wako wa sasa. Unadai universe iko self-existing, lakini hujui hata roho yako iko wapi kwa mwili. How do you even define self when you can’t fully explain consciousness?
Kuna watu wanajua kwa kupitia experience, wengine kupitia intuition, wengine reason, wengine through divine revelation. Wewe umekalia “naona haipo, basi haipo” – hiyo si hoja, ni mtazamo wa mtoto anayekatalia pipi.
Kwa nini mtu anazaliwa bila kuamua?”
Sasa unataka consent form ya kuzaliwa? Ukiambiwa uisaini ukiwa hujazaliwa bado, uta-sign kwa kidole gani? Unapinga freewill na bado unadai uambiwe mapema kabla hujazaliwa – ni kama kulalamika hukupata remote ya dunia ukiwa bado kwa mbegu ya wazazi wako.
Hii ni sawa na app kujilalamikia developer kwamba iliwekwa kwenye simu bila kupewa choice ya kujifanya app. U exist inside a system and complain about the system using tools given by the system. Irony ya hali ya juu.
Huu ni ushahidi gani wa Mungu?”
Ulipoamka leo, uliamua moyo u-beat? Uliamuru figo ifanye kazi? Au ulishtuka umeshajisaidia na mwili umefanya kazi yake bila wewe kujua? Na bado unafikiri uko in control ya kila kitu? Broh, humility haijawahi ua mtu.
Na ukiona design, order, intelligence na patterns katika nature (kama laws of physics zenye consistency ya ajabu), unastahili kuuliza “Kwa nini kuna order kama hakuna Mind iliyo-organize?” Au universe ilijiandika yenyewe kama AI ambayo hujaiprogram?
“Wewe hauamini, nisikuletee imani zangu!”
Halafu unasema universe “ni ya kiasili” bila kuonesha source ya hiyo asili. Imani yako ya “hakuna Mungu” ni imani pia – tofauti ni kwamba yako haina msingi, ni kelele ya kupinga tu. “I don’t believe” si hoja ya kisomi, ni msimamo wa mtu aliyekata tamaa ya kuuliza maswali kwa unyenyekevu.
"Kwamba ninahitaji factory reset ya ubongo!”
Labda, lakini kabla nianze ku-reset brain yangu, tafadhali tafuta charger ya akili yako kwanza. Inaonekana software yako ya mantiki imepata logic virus – imejaa loops za “Naona haipo, basi haipo.”
Unaweza kuchagua kuamini au kutoamini, but truth exists independently of belief. Kama mtu akisema haamini mvuto wa dunia, bado ataporomoka juu ya dari akijaribu kuruka kama ndege.
So kabla hujawa mfalme wa "I know", kumbuka: Sauti ya mtu anayelala ndani ya boksi haibadili ukubwa wa dunia.
TUTAELEWANA TU KIKEJELI KEJELI HIVI HIVI.
Peace and Paradox.