Kama Mungu hayupo, maisha yana maana gani? Na kama yupo, kwanini Dunia inateseka hivi?

Kama Mungu hayupo, maisha yana maana gani? Na kama yupo, kwanini Dunia inateseka hivi?

Nilimwambia disbelief is also a kind of belief, lakini anashupaza shingo kukataa, sidhani kama kuna msomi mwenye uwezo wa kujenga hoja vizuri akashindwa kuelewa akiambiwa kuwa "kutokuamini napo ni imani"

Huyu atakuwa wa kwanza.
Ni imani na maeneo mengine ina dini kabisa inaitwa "Upagani"
 
Kwanza mimi siamini kwenye kuamini.

Sina imani ya aina yeyote ile.

Sihitaji kuamini.

Nahitaji kujua kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho.
"kutokuamini" ni imani . You believe kwamba huamini, bila ushahidi wa mwisho kwamba kila kitu kinaweza kuthibitishwa. Ironically, unahitaji imani kubwa kuishi bila imani.
 
hoja zako zimejaa kelele kuliko mantiki—ni kama mtu anayejaribu kupima uzito wa upendo kwa mizani ya sokoni.

"Unasema nithibitishe Mungu yupo."
kabla hujanitaka ni-thibitishe kitu cha metaphysical kwa kipimo cha fizikia, niambie, Je, umewahi kuiona akili yako?(sitaki porojo za kwamba akili inapimika sijui nini, nambie direct if yes or no)
Sitaki porojo za kumhusisha huyo Mungu na mifano uchwara ya hewa, akili n.k

Eleza ulijuaje huyo Mungu yupo?

Thibitisha uwepo wa huyo Mungu na si imani zako uchwara za vitabuni.
Au unaamini ipo kwa sababu unadhani unafikiri?
That, my friend, is faith in function without physical evidence.

Unasema ni non-sequitur kuhusisha hewa na Mungu.
Yet wewe unavuta hewa usiyoiona, unaishi bila kuuliza ipoje, ilikotoka au inavyoendelea kuwepo.
Na wewe unaamini tu kuna Mungu bila kuuliza alitoka wapi?

Chanzo cha huyo Mungu ni nini?

Huyo Mungu kabla ya kuumba kitu chochote kile alikuwa wapi?

Huko alikokuwa kulitoka wapi?
Lakini ukisikia jina "Mungu" unageuka Professor wa Logic ghafla.
Kuna hypocrisy hapo – kama hewa ipo na huioni, kwa nini si Mungu?

Unasema “Mungu ana exist tu kwenye vitabu na vichwa.”
Bro, hata gravity unaijua kwa vitabu na effects zake—hujaiona, lakini unainyenyekea.
Ni ajabu sana, ukiambiwa Mungu yupo, unaleta habari za kutaka kujua passport yake.
Lakini ukiambiwa dark matter ipo, unasema “science is beautiful.”

"Nilimuona wapi huyo Mungu?
Swali lako linafanana na kumuuliza Beethoven alisikiaje muziki ilhali alikuwa kiziwi.
The answer is simple, Not everything is understood through sensory evidence.
Some truths are revealed, not measured.

“Imani uchwara” unaita?
Huku ukiamini kuwa everything just popped into existence kwa nothing, bila purpose, bila design.
Yaani universe nzima yenye precision kama ya Swiss watch, ilijiumba yenyewe tu kama ajali ya bahati nzuri?
That's not logic,, that’s intellectual gymnastics za kihuni.

Kwa kifupi
You demand divine proof while swimming in daily miracles—life, consciousness, order, morality.
Kama bado huamini, that's fine. Lakini usijifiche nyuma ya sarcasm na pseudo-logic ukidhani umevunja hoja ya imani wakati hujachambua hata the basics of metaphysics.

Kumbuka:
Kutoamini si hoja.
Kejeli bila akili ni makelele ya upweke.
Na mantiki isiyo na unyenyekevu ni kiburi kinachovaa koti la akili.
Unapiga blah! blah! tu.

Chanzo cha huyo Mungu ni nini?

Au huyo Mungu alizuka tu from nowhere?
 
"kutokuamini" ni imani . You believe kwamba huamini, bila ushahidi wa mwisho kwamba kila kitu kinaweza kuthibitishwa. Ironically, unahitaji imani kubwa kuishi bila imani.
Una elewa maana ya siamini?

Can you differentiate between belief and disbelief?
 
Sitaki porojo za kumhusisha huyo Mungu na mifano uchwara ya hewa, akili n.k

Eleza ulijuaje huyo Mungu yupo?

Thibitisha uwepo wa huyo Mungu na si imani zako uchwara za vitabuni.

Na wewe unaamini tu kuna Mungu bila kuuliza alitoka wapi?

Chanzo cha huyo Mungu ni nini?

Huyo Mungu kabla ya kuumba kitu chochote kile alikuwa wapi?

Huko alikokuwa kulitoka wapi?

Unapiga blah! blah! tu.

Chanzo cha huyo Mungu ni nini?

Au huyo Mungu alizuka tu from nowhere?
So wewe unadhani everything popped into existence from nothing, by nothing, for nothing — halafu unabeza idea ya Mungu? Hapa ni sawa na kusema dictionary ilijiandika yenyewe after explosion ya printing press. Come on, logic pia ina mipaka yake.

Hapo sasa, changanya na zako.
 
Na huyo Mungu alizuka tu from nothing?

Kwa nini hujiulizi chanzo cha huyo Mungu ni nini?

Unataka kufanya special pleading fallacy.

Unaona haiwezekani ulimwengu utokee from nothing, ila unaona sawa Mungu kutokea from nothing.

This is a special pleading fallacy.
 
Una elewa maana ya siamini?

Can you differentiate between belief and disbelief?
Yes, I can,, just understand that disbelief is also a form of belief, just in the opposite direction. Let me explain.

Ukisema "naamini", unakubali kuwa jambo fulani ni kweli.
Ukisema "siamini", hujakataa tu bila msingi – mara nyingi, unakuwa na imani tofauti kinyume na lile linalodaiwa.

Kwa mfano:

Mtu asemapo "I believe God exists," ana imani katika kuwepo kwa Mungu.

Mwingine akisema "I don't believe God exists," hajasema hana imani kabisa – badala yake, ana imani kwamba Mungu hayupo. Hiyo pia ni imani, ya aina tofauti.

Kwa hivyo, disbelief siyo kukosa imani kabisa, bali ni kuamini kuwa jambo fulani si kweli. Ni msimamo wa kiakili unaotegemea mantiki au ushahidi fulani – just like belief.

You either believe X is true, or you believe X is not true – in both cases, you're still holding a belief.

"Disbelief" is not the absence of belief – it’s the presence of an opposing belief.
Siamini = naamini vinginevyo.

UMEELEWA??
 
So wewe unadhani everything popped into existence from nothing, by nothing, for nothing — halafu unabeza idea ya Mungu? Hapa ni sawa na kusema dictionary ilijiandika yenyewe after explosion ya printing press. Come on, logic pia ina mipaka yake.

Hapo sasa, changanya na zako.
Ndio mkuu, kulikuwa na vyuma chakavu ikapita billions of years vikajipanga ikatokea Boeing 777X yenyewe.

:peepoGiggle:

I Do not have enough faith to be an Atheist.
 
"Siamini" ni upande wa pili wa shilingi wa "naamini". Maneno yote msingi wake ni imani.
Sio imani.

Msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika, ushahidi na uthibitisho.

Unaweza kuamini hata uongo.

Lakini ili tuhakikishe kwamba unacho kiamini ni ukweli lazima kuwe na uthibitisho.
 
Yes, I can,, just understand that disbelief is also a form of belief, just in the opposite direction. Let me explain.

Ukisema "naamini", unakubali kuwa jambo fulani ni kweli.
Ukisema "siamini", hujakataa tu bila msingi – mara nyingi, unakuwa na imani tofauti kinyume na lile linalodaiwa.

Kwa mfano:

Mtu asemapo "I believe God exists," ana imani katika kuwepo kwa Mungu.

Mwingine akisema "I don't believe God exists," hajasema hana imani kabisa – badala yake, ana imani kwamba Mungu hayupo. Hiyo pia ni imani, ya aina tofauti.

Kwa hivyo, disbelief siyo kukosa imani kabisa, bali ni kuamini kuwa jambo fulani si kweli. Ni msimamo wa kiakili unaotegemea mantiki au ushahidi fulani – just like belief.

"Disbelief" is not the absence of belief – it’s the presence of an opposing belief.
Siamini = naamini vinginevyo.

UMEELEWA??
Unaweza kuamini hata uongo. Kwa sababu msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika, ushahidi na uthibitisho.

Sasa tutahakikisha vipi imani yako ya uwepo wa Mungu ni ukweli na si uongo?

Unathibitisha vipi Mungu yupo kweli na si imani zako za kufikirika tu?

Nikisema kwamba nina imani ya kwamba kuna Dragons 🐉 watemao moto midomoni mwao bila uthibitisho wowote ule, utakubali tu?
 
Ndio mkuu, kulikuwa na vyuma chakavu ikapita billions of years vikajipanga ikatokea Boeing 777X yenyewe.

:peepoGiggle:

I Do not have enough faith to be an Atheist.
Hoja yako ni false analogy — kulinganisha vitu viwili visivyolingana. Evolution na natural processes hazidai kuwa "vyuma vilijipanga," bali ni mchakato wa taratibu unaoongozwa na sheria za asili, si chaos.
 
Unaweza kuamini hata uongo. Kwa sababu msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika, ushahidi na uthibitisho.

Sasa tutahakikisha vipi imani yako ya uwepo wa Mungu ni ukweli na si uongo?

Unathibitisha vipi Mungu yupo kweli na si imani zako za kufikirika tu?

Nikisema kwamba nina imani ya kwamba kuna Dragons 🐉 watemao moto midomoni mwao bila uthibitisho wowote ule, utakubali tu?
Sitoamini bila ushahidi—na vivyo hivyo, si kila kitu kinachokosa ushahidi wa moja kwa moja ni uongo.

The existence of God, unlike dragons, is not a scientific claim but a metaphysical one—it deals with meaning, purpose, and origin beyond what science can test.

Imani kwa Mungu haijajengwa juu ya ushahidi wa moja kwa moja pekee, bali pia juu ya uzoefu binafsi, historia, falsafa, na mabadiliko halisi ya maisha.

To compare God with fire-breathing dragons is a category error—ni kama kulinganisha dhana ya upendo na ladha ya chakula; zote ni halali lakini hupimika kwa vigezo tofauti.
 
Hoja yako ni false analogy — kulinganisha vitu viwili visivyolingana. Evolution na natural processes hazidai kuwa "vyuma vilijipanga," bali ni mchakato wa taratibu unaoongozwa na sheria za asili, si chaos.
Aisee nilikuwa nishaanza kushusha paragraph, but I'm done debating God and Evolution! ! !

#JesusIsLord
 
Kosa kubwa huwa naliona kwa watu wengi ukiwemo mleta uzi ni kutokuelewa namna MUNGU na namna zake anavyo operate.

Wengi huwa tunakwenda kwa MUNGU tayari tukiwa na matarajio ya vitu tunataka wakati tulitakiwa kwenda mbele za MUNGU tukiwa tumejinyenyekesha kama mtumishi mbele ya mfalme na kumwambia "Baba,nimekuja mbele yako,wewe ndie unajua nahitaji nini,nipo tayari kupokea naomba ulinzi na muongozo wa malaika wako niyapate yale yote ninayohitaji" halafu nenda sasa huko duniani huku ukiziishi amri zake 10 uone kama hautaona ulinzi wake kwenye maisha yako.

Unakuta mtu anakazi let's say inamlipa laki 9 kwa mwezi. Ila kutokana na life style yake anashindwa kubalance mambo anaona haimtoshi anakwenda kwa MUNGU na lawama moyoni akitaka awe na biashara kubwa au vyanzo vya mapato vikubwa.

MUNGU anasikia matakwa yako ambayo umejenga kwa msingi wa fikra zitokanazo na tamaa yako. Anatuma malaika wake waaanze kukupa hitaji lako. Unashangaa ghafla kazini kunaanza figisu,mara bosi akubadilikie,mara aje mtu akutengenezee chuki kazini,mara kampuni ipate shida ya kufeli. Mwisho wa siku unarudi mtaani ukiwa hauna hata mia. Mkeo aliyekuwa anajiapiza kukupenda anakuacha kwasababu hauna kazi tena na maisha yameanza kuwa magumu kwako.

Sasa hapa ndipo wengi huwa wanafeli. Wanaenda tena kwa MUNGU kumlaumu kwann haya yanatokea. Kumbe malaika wa MUNGU wapo kazini kutimiza matakwa yako.

Umepoteza kazi sio kwasababu MUNGU amekupuuza, hapana. Umepoteza kazi kwasababu MUNGU anataka sasa uanze upya, unataka kuwa tajiri kupitia mshahara wa laki 9? Haitawezekana,lazima uache kazi uanze,urudi mtaani,uteseke, mke uliye nae sio mke wa hadhi ya tajiri ni mke wa mtu wa kawaida, mke wako atakuja baada ya wewe kuachana na huyu uliyenae na ukimuona tu utamjua maana atakuelewa na mipango yako na atakukubali na hali yako huku akikutii kila mipango hewa unayomwambia akikusapoti, so lazima uliyenae akukimbie,usilalamike ulitaka haya yote, akili yako itoke kwenye kutegemea ajira iwaze kujiajiri na hapo ndipo safari ya utajiri uliyoitaka itaanza.

Marafiki watakutenga,usiseme "fake friends" MUNGU anakutengenezea crew mpya ya marafiki watakaoendana na wewe mpya,hawa wasasa ni wa toleo lako la mshahara wa laki 9. Utakaoletewa ni wale ambao ukimtext unataka milioni 5 hata kama hana anakwenda kukopa kwa niaba yako,au hakuulizi "milioni 5 za nini" bali atakuuliza "nikutumie kwenye namba ipi au account ipi". Usichukie ni MUNGU anaongea na wewe kwa lugha yake. Lugha ya MUNGU ni ya vitendo sio maneno mengi.

Unasema unataka kuwa kama baba yako, MUNGU alikuumba uwe wewe toleo lako ila ukasema mimi nataka kuwa kama baba yangu. Baba yako alikuwa ni mtu mwenye roho mbaya kwa ndani kutokana na makuzi aliyopitia utotoni mwake ila wewe hakukuonyesha roho mbaya sababu ni mtoto wake. Unashangaa ghafla watu wanaokuzunguka wanaanza kukufanyia matendo ya kukukwaza na hata haukuwakosea chochote. Unamuendea tena MUNGU na lawama kwamba walimwengu wanakukosea bila sababu (usichojua anafanyia kazi matakwa yako sababu ulimlalamikia aache kukupa mahitaji yako akupe matakwa). Unashangaa MUNGU hajibu unasema wacha nitadeal nao jicho kwa jicho. Unaanza kuwa katili na roho mbaya. Hadi mtoto wako anakuja kukwambia "baba watu wanasema unaroho mbaya sana"

Usichokijua ubaya sio wa MUNGU kufanya maisha yako kuwa hivyo, ubaya ni wewe ulitaka kuwa copy ya baba yako. Amekufanya kuwa toleo la baba yako. Why sasa unashangaa mtoto wako kuja kukupa ujumbe wa matokeo ya maombi yako kujibiwa. Ungemuachia MUNGU akuumbe kwa mpango wake ungekuwa vile alivyotaka na ungefurahia.

MUNGU huwa anawapa watu vyote,wavyotaka na wanavyohitaji. Ila mpango wake ni kukupa mahitaji yako na sio matakwa yako.

Wadada wangapi walitaka mwanaume handsome,mwenye pesa,anatokea familia yenye fedha na jina kubwa ila bado akishampata hitaji lake la furaha ya ndoa anakosa. Anajikuta kila akimtazama dereva wa mume wake au mlinzi, au yule kijana wa kawaida kabisa asiye na utajiri wala mali nyingi moyo wake unajawa na faraja na majibu ya furaha yake anayaona mbele yake?

Sababu ni kwamba aliruhusu tamaa iongoze fikra zake,fikra zikatengeza matakwa,matakwa yakamjaza na hali ya kukosa akamkimbilia MUNGU akimlilia kwa tamaa zake akitaka afanyie hivyo. Ila MUNGU alishajua mpango wake juu ya huyu dada kabla hata hajazaliwa.

So kwasababu MUNGU anatupenda watoto wake huwa anatupatia vyote. Atampa mwanaume anayemtaka lakini atamletea mwanaume anayemuhitaji baadae. Then baada ya hapo, huzuni itarudi na ukweli ndio huwa unauma. Sasa unashindwa kubakia na tamaa zako au ukidhi mahitaji.

Unakuja kusema life is not fair. Hapana ni wewe haupo fair.

Kuna lugha ya MUNGU halafu kuna lugha na mitazamo yetu sisi wanadamu. Hatumjui MUNGU kwasababu tunatumia muda mwingi kupretend tunamjua badala ya kumjua kweli.

Ulinzi wake upo na sisi masaa 24/7. Anatupenda kuliko yeyote aliyewahi kutupenda. Ametuumba kwa mfano wake ( unaemuona mbaya machoni mwako kwa mtu mwingine ndie mtu mzuri kuliko mtu yoyote yule aliyewahi kukutana nae) na hivyo hatuwezi teseka wala kukosa hifadhi hapa ulimwenguni. Vyote vilivyomo hapa ulimwenguni vina wenyewe na hakuna ambaye kapangiwa kukosa.

Furaha na amani ni ya kila m'moja wetu,wenye nacho na wasio nacho. Kuwa makini unapomuendea MUNGU. Hakikisha haupigi goti la lawama bila kujijua. Hakikisha unaongea nae na sio kumlalamikia na kulaumu. Hesabu baraka zake kwako na sio kuchambua mipango yake kwako na kuwachanganya malaika wake wakiwa kazini.

Umepata kazi,mambo yakiwa magumu mwambie "baba,nashukuru kwa baraka zako,kwasasa nakosa uelekeo naomba uniongoze,nakusikiliza" kisha fuata ishara atakazo kupa atazungumza na wewe kwa njia zake na hekima ndio itakuunganisha nae kiutendaji. Ukikosa hekima piga goti muombe akupe msaada wa hekima. Inaweza hekima ikaja kwa sura ya mtoto wako, jirani,baba yako,rafiki yako,ndugu yako,mdogo wako, mkeo, kiongozi wa dini,na pengine anaweza hata tumia mitandao ya kijamii kama hapa kanitumia kukufikishia hemika,au anaweza kukujaza na hekima wewe binafsi ya kiutendaji.

Kuwa msafi wa matendo, jaza fikra zako na mawazo chanya, na kila siku sikilizia sana ishara zake. Utapata unachohitaji.
 
Na huyo Mungu alizuka tu from nothing?

Kwa nini hujiulizi chanzo cha huyo Mungu ni nini?

Unataka kufanya special pleading fallacy.

Unaona haiwezekani ulimwengu utokee from nothing, ila unaona sawa Mungu kutokea from nothing.

This is a special pleading fallacy.
Hoja yako inajaribu kulinganisha vitu viwili visivyolingana—Mungu na ulimwengu—na hapo ndipo logical error inaingia.

Mungu, kwa tafsiri ya kifalsafa (na hata ya kidini), ni "necessary being"—yeye hasababishwi, hayuko ndani ya muda wala nafasi, na hahitaji chanzo. Ulimwengu, on the other hand, unaonekana kuwa "contingent"—una mwanzo, umefungwa na muda, na unaonyesha mabadiliko, hivyo unahitaji explanation ya chanzo chake.

Kusema “Mungu alitokea from nothing” ni category mistake, kwa sababu Mungu, kama asemapo classical theism, hakuumbwa wala hakutokea—yuko milele. Sasa, kusema "kila kitu kina chanzo" halafu kumwuliza Mungu alitoka wapi ni ku-miss point ya hoja ya Mungu kuwa chanzo kisichohitaji chanzo kingine.

"Universe coming from nothing needs an explanation. God, by definition, is the explanation—not something that also needs one."
 
Sio imani.

Msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika, ushahidi na uthibitisho.

Unaweza kuamini hata uongo.

Lakini ili tuhakikishe kwamba unacho kiamini ni ukweli lazima kuwe na uthibitisho.
Tofauti ya anayeamini bila uthibitisho na wewe ni nini?
 
Back
Top Bottom