Kama Mungu hayupo, maisha yana maana gani? Na kama yupo, kwanini Dunia inateseka hivi?


Nilijuaje Mungu yupo?”
Wewe unajua hewa ipo? Unaiona? Unaigusa? Acha kujifanya fundi wa "proof" halafu ukikosa kuona kwa macho, unakataa kila kitu.
Kama akili zako zingewezeshwa kuona frequency zote za existence, ungelia kwa aibu ya ujuaji wako wa sasa. Unadai universe iko self-existing, lakini hujui hata roho yako iko wapi kwa mwili. How do you even define self when you can’t fully explain consciousness?

Kuna watu wanajua kwa kupitia experience, wengine kupitia intuition, wengine reason, wengine through divine revelation. Wewe umekalia “naona haipo, basi haipo” – hiyo si hoja, ni mtazamo wa mtoto anayekatalia pipi.

Kwa nini mtu anazaliwa bila kuamua?”

Sasa unataka consent form ya kuzaliwa? Ukiambiwa uisaini ukiwa hujazaliwa bado, uta-sign kwa kidole gani? Unapinga freewill na bado unadai uambiwe mapema kabla hujazaliwa – ni kama kulalamika hukupata remote ya dunia ukiwa bado kwa mbegu ya wazazi wako.

Hii ni sawa na app kujilalamikia developer kwamba iliwekwa kwenye simu bila kupewa choice ya kujifanya app. U exist inside a system and complain about the system using tools given by the system. Irony ya hali ya juu.

Huu ni ushahidi gani wa Mungu?”
Ulipoamka leo, uliamua moyo u-beat? Uliamuru figo ifanye kazi? Au ulishtuka umeshajisaidia na mwili umefanya kazi yake bila wewe kujua? Na bado unafikiri uko in control ya kila kitu? Broh, humility haijawahi ua mtu.

Na ukiona design, order, intelligence na patterns katika nature (kama laws of physics zenye consistency ya ajabu), unastahili kuuliza “Kwa nini kuna order kama hakuna Mind iliyo-organize?” Au universe ilijiandika yenyewe kama AI ambayo hujaiprogram?

“Wewe hauamini, nisikuletee imani zangu!”
Halafu unasema universe “ni ya kiasili” bila kuonesha source ya hiyo asili. Imani yako ya “hakuna Mungu” ni imani pia – tofauti ni kwamba yako haina msingi, ni kelele ya kupinga tu. “I don’t believe” si hoja ya kisomi, ni msimamo wa mtu aliyekata tamaa ya kuuliza maswali kwa unyenyekevu.

"Kwamba ninahitaji factory reset ya ubongo!”
Labda, lakini kabla nianze ku-reset brain yangu, tafadhali tafuta charger ya akili yako kwanza. Inaonekana software yako ya mantiki imepata logic virus – imejaa loops za “Naona haipo, basi haipo.”

Unaweza kuchagua kuamini au kutoamini, but truth exists independently of belief. Kama mtu akisema haamini mvuto wa dunia, bado ataporomoka juu ya dari akijaribu kuruka kama ndege.

So kabla hujawa mfalme wa "I know", kumbuka: Sauti ya mtu anayelala ndani ya boksi haibadili ukubwa wa dunia.

TUTAELEWANA TU KIKEJELI KEJELI HIVI HIVI.

Peace and Paradox.
 
Sasa unaelewa kuwa huyo mzazi ndiye Mungu na sisi ndio huyo mtoto na umemuita Mungu mzembe.

Umesema kuwa Mungu anahatarisha maisha yetu kwa kisingizio cha uhuru wakati jukumu la Mungu mwenye upendo wote ni kulinda, kuelekeza na kuchuja chaguzi hatarishi.

Kwa nini unampa mzazi wa mtoto, mtu tu mwenye ujuzi wenye mwisho, uwezo wenye mwisho na upendo wenye nwisho, wajibu mkubwa kwa mtoto wake, zaidi ya unavyompa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote wajibu kwa dunia nzima?
 
Hujathibitisha Mungu yupo bado.
 
Usilete habari za oxygen.

Jikite kwenye mada, Mada inahusu Mungu sio oxygen.

Wewe si unajua Mungu yupo, Sasa eleza yukoje na ulimuona wapi?

Acha kuzunguka zunguka.

Eleza huyo Mungu yukoje?

Na ulimuona wapi ukajua yupo?
Naona unalia ,Mungu yupo na wewe unajua
 
Nilijuaje Mungu yupo?”
Wewe unajua hewa ipo? Unaiona? Unaigusa? Acha kujifanya fundi wa "proof" halafu ukikosa kuona kwa macho, unakataa kila kitu.
Unafanya Logical fallacy ya non-sequitur.

Umeshindwa kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu, unaanza kuhusisha hewa na Mungu.

Una unganisha vitu viwili tofauti visivyo na uhusiano wowote ule kuunda hitimisho potofu.

Thibitisha Mungu yupo, Acha porojo na mifano uchwara.
Wewe hujui hata Mungu yukoje, Hujui huyo Mungu alitokana na nini, Umeshindwa kuelezea ulijuaje Mungu yupo, Unafosi na kulazimisha imani zako za kidini tu.

Hujaeleza ulijuaje Mungu yupo, unafosi imani zako uchwara tu.
Kuna watu wanajua kwa kupitia experience, wengine kupitia intuition, wengine reason, wengine through divine revelation. Wewe umekalia “naona haipo, basi haipo” – hiyo si hoja, ni mtazamo wa mtoto anayekatalia pipi.
Nakuuliza hivi 👇

Ulimuona wapi huyo Mungu ukajua yupo?

Unaleta habari za experience, Intuition bila kueleza ni wapi ulimuona huyo Mungu?

Huyo Mungu wenu ana exist kwenye hekaya zenu za vitabuni na kwenye vichwa vyenu tu.

In reality, Hakuna Mungu.

Logical non sequitur.
Unaleta mifano uchwara kutetea imani zako zisizo na ukweli wala uthibitisho wowote ule.
 
Naona unalia ,Mungu yupo na wewe unajua
Huyo Mungu angekuwepo, kusingekuwa hata na haja ya kuhoji uwepo wake.

Kila mtu angejua na kufahamu kwa uhakika kabisa kwamba Mungu yupo.

Mungu hayupo ndio maana mnahangaika sana kumwelezea na kumtetea aonekane yupo.
 
Unadai huamini chochote, lakini unapigana kama mtu aliyeumizwa na kitu anachodai hakipo. That’s like arguing passionately against unicorns—if God is a fantasy, why are you so emotionally invested? 🤔

Unauliza “nlijuaje Mungu yupo?” lakini hushughuliki na swali la “ulijuaje Mungu hayupo ?”,, hoja yako hazina mizizi wala matawi. Na kuhusu free will, hujui umezaliwa mpaka uzaliwe, sawa na hujui umetapika hadi pale tumbo limeshaamua. Nature itself doesn’t owe you a democratic vote.

Unadai "You don’t believe," lakini kila hoja yako imejengwa juu ya imani yako binafsi ya kuwa hakuna. Mkuu hiyo nayo ni imani—just without rituals. Ni kama atheism yako imevaa kanzu ya dharau.

Sasa, before you ask for a brain reset, jaribu kwanza ku update software ya logic zako . You might be running on emotions 2.0 instead of reasoning 5.1.

Jaribu kuiga hata kidogo kwa Atheist mwenzako Kiranga the way anavyo jenga hoja zenye mantiki.

Peace and paradox.
 
Magonjwa mateso umaskini yote hayo ni matokeo ya dhambi na Mungu ana ushirika na dhambi
 
Na wapo wanaoamini MUNGU yupo ila uwezo wake ndo hawaujui.
 
Bado haujathibitisha uwepo wa Mungu...
 
Infropreneur anaamini tu hayupo ila hoja zake hana tufauti na wanaomini yupo. Wote ni imani.
 
hoja zako zimejaa kelele kuliko mantiki—ni kama mtu anayejaribu kupima uzito wa upendo kwa mizani ya sokoni.

"Unasema nithibitishe Mungu yupo."
kabla hujanitaka ni-thibitishe kitu cha metaphysical kwa kipimo cha fizikia, niambie, Je, umewahi kuiona akili yako?(sitaki porojo za kwamba akili inapimika sijui nini, nambie direct if yes or no)
Au unaamini ipo kwa sababu unadhani unafikiri?
That, my friend, is faith in function without physical evidence.

Unasema ni non-sequitur kuhusisha hewa na Mungu.
Yet wewe unavuta hewa usiyoiona, unaishi bila kuuliza ipoje, ilikotoka au inavyoendelea kuwepo.
Lakini ukisikia jina "Mungu" unageuka Professor wa Logic ghafla.
Kuna hypocrisy hapo – kama hewa ipo na huioni, kwa nini si Mungu?

Unasema “Mungu ana exist tu kwenye vitabu na vichwa.”
Bro, hata gravity unaijua kwa vitabu na effects zake—hujaiona, lakini unainyenyekea.
Ni ajabu sana, ukiambiwa Mungu yupo, unaleta habari za kutaka kujua passport yake.
Lakini ukiambiwa dark matter ipo, unasema “science is beautiful.”

"Nilimuona wapi huyo Mungu?
Swali lako linafanana na kumuuliza Beethoven alisikiaje muziki ilhali alikuwa kiziwi.
The answer is simple, Not everything is understood through sensory evidence.
Some truths are revealed, not measured.

“Imani uchwara” unaita?
Huku ukiamini kuwa everything just popped into existence kwa nothing, bila purpose, bila design.
Yaani universe nzima yenye precision kama ya Swiss watch, ilijiumba yenyewe tu kama ajali ya bahati nzuri?
That's not logic,, that’s intellectual gymnastics za kihuni.

Kwa kifupi
You demand divine proof while swimming in daily miracles—life, consciousness, order, morality.
Kama bado huamini, that's fine. Lakini usijifiche nyuma ya sarcasm na pseudo-logic ukidhani umevunja hoja ya imani wakati hujachambua hata the basics of metaphysics.

Kumbuka:
Kutoamini si hoja.
Kejeli bila akili ni makelele ya upweke.
Na mantiki isiyo na unyenyekevu ni kiburi kinachovaa koti la akili.
 
Reactions: Tsh
Infropreneur anaamini tu hayupo ila hoja zake hana tufauti na wanaomini yupo. Wote ni imani.
Kwanza mimi siamini kwenye kuamini.

Sina imani ya aina yeyote ile.

Sihitaji kuamini.

Nahitaji kujua kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho.
 
Kwanza mimi siamini kwenye kuamini.

Sina imani ya aina yeyote ile.

Sihitaji kuamini.

Nahitaji kujua kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho.
Ok, Mkuu. Kama hayupo yako si suala la kiimani, embu tuambie, kwanini hakuna MUNGU?
 
Infropreneur anaamini tu hayupo ila hoja zake hana tufauti na wanaomini yupo. Wote ni imani.
Nilimwambia disbelief is also a kind of belief, lakini anashupaza shingo kukataa, sidhani kama kuna msomi mwenye uwezo wa kujenga hoja vizuri akashindwa kuelewa akiambiwa kuwa "kutokuamini napo ni imani"

Huyu atakuwa wa kwanza.
 
Reactions: Tsh
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…