Kama Mungu hayupo, maisha yana maana gani? Na kama yupo, kwanini Dunia inateseka hivi?

Thibitisha Mungu anajua kila kitu na kwamba hiyo habari na hoja nzima kwamba Mungu yupo si hadithi tu.
 
Bado hujathibitisha kwamba imani yako imejengwa katika ukweli.

Unaweka a string of logical fallacies tu kama personal experience.

Personal experience unaweza kupata hata ya uongo kutokana na ugonjwa wa akili.
 
Ni kweli kuona si uthibitisho wa mwisho wa kuwepo kwa kitu, lakini pia kuona ni aina moja ya ushahidi wa kihisia (empirical evidence). Hoja yako inategemea mifano ya optical illusions na astrophysics, ambayo ni valid katika muktadha wake, lakini haibadilishi kabisa maana ya kuona kama ushahidi wa kihalisia (factual evidence).

Kwa mfano:
Yes, a mirage shows water that isn’t there—but the illusion itself is observable and explainable by physics. It doesn’t prove all seeing is false, it proves some perceptions need verification

Kwa hiyo, kuona si uhakika wa 100%, lakini si irrelevanti—ni sehemu ya mchakato wa ushahidi unaohitaji kuthibitishwa kwa njia nyingine pia, kama vile kusikia, kupima, au kutumia vifaa vya kisayansi.

"Seeing is not always believing—but dismissing seeing altogether is intellectually lazy."
 
Siku moja nilikuwa naangalia commentary ya wild life,nikamuona somba ananyemelea ndama aliezaliea na nyati mda mfupi uliopita.kulikuwa na mapambano kati ya nyati na simba hadi kundi lanyati lilipokuja kisaidia na yule ndama alipona
Hoja yangu ni kwamba kwanini Mungu aliumba wanyama kama simba ili wategemee wanyama wengine Tena kwa kuwakamata kikatili kabisa na kuwala. Hii inamanisha kuwa Bila Swala simba haiwezi kuishi.
Hitimisho ni kuwa Maisha ni haya tunayoishi na hakina Maisha mengine ndio maana usipopambana kama simba ili upate chakula imeisha!
 
Thibitisha Mungu anajua kila kitu na kwamba hiyo habari na hoja nzima kwamba Mungu yupo si hadithi tu.
Tuanze na swali rahisi—kama hakuna Mungu, basi nani aliweka akili kwa akili yako hadi ukaweza kuuliza swali hilo la kina? Siri ya kiumbe hujulikana na Muumba wake tu. Unadhani simu inaweza kuelewa mwenye kuitengeneza?

Even Google needs a server, data, and an engineer behind it. So what makes you think your existence, consciousness, and the entire universe just popped out of nowhere like a cheap magician's trick? This isn’t Netflix writing a random plot—this is divine coding at its finest!

Kwa kifupi, Mungu hajawahi kuwa hadithi. Ni wewe tu uko kwenye chapter moja ya kitabu ambacho hujasoma hata introduction. He knows everything—not because He guesses right, but because He wrote the whole script. While you're busy flipping today's page, Yeye aliandika from Genesis to your next sneeze.

So next time you doubt He exists, jaribu ku-create uhai bila kutumia uhai uliowekwa. Try creating a soul—if you succeed, then maybe, just maybe, you can question the Author.
 
Bado hujathibitisha kwamba imani yako imejengwa katika ukweli.

Unaweka a string of logical fallacies tu kama personal experience.

Personal experience unaweza kupata hata ya uongo kutokana na ugonjwa wa akili.
Unasema bado sija "thibitisha kwamba imani yangu imejengwa katika ukweli," lakini hujaeleza kweli ni nini, wala hujaweka kipimo gani cha kuitambua. Unadai ni "string of logical fallacies," lakini unashindwa hata ku-name moja—hiyo si fallacy ya sweeping generalization au ni wishful thinking yako inafanya overtime?

Kuhusu "personal experience inaweza kuwa ya uongo kutokana na ugonjwa wa akili"—sasa hapo umeteleza kwenye ad hominem na ukaingia kwa strawman kama unapigana na kivuli chako. Experience ya mtu haithibitishi uongo wake automatically eti kwa sababu kuna possibility ya mental illness. By that logic, hata wewe huwezi kuwa na uhakika na ulichokisema—unless uko na psychiatric clearance letter from heaven
 
Uwepo wako ni wako wewe.

Mungu hayupo.

Huyo Mungu kama yupo ajitokeze mwenyewe ajitetee kama ana huo uwezo.

Sio wewe unahangaika kumuelezea na kumtetea.
Akitokea unavyotaka wewe uwe na uhakika hutakuwepo wewe
 
Kuona si kuthibitisha kitu kipo. Katika uthibitisho kuwa kitu kipo usitegemee kuona.

Kwa sababu kuna vitu vinaonekana lakini havipo na vingine havionekani lakini vipo.

Kuona hakuthibitishi kitu kipo au hakipo.
 
Kama hajamlimit binadamu zile Amri kumi za Mungu logic yake ni nini ?


Na kama hajamlimit kwanini binadamu akifanya mambo mengine Ambayo hajawa limited Huyo Mungu anasema ni dhambi
Amri Kuu ni moja ya kupendana. Amri Kumi ziliwekwa kutufaa sisi wenyewe, wewe ukimla mke wa mtu au ukimuibia mtu kitu chake unadhani nini kitatokea.
 
Kwa nini swali lako linakuwa "nani"?
 
Personal experience ni logical fallacy. Wewe hujajua tu.
 
Kuona si kuthibitisha kitu kipo. Katika uthibitisho kuwa kitu kipo usitegemee kuona.

Kwa sababu kuna vitu vinaonekana lakini havipo na vingine havionekani lakini vipo.

Kuona hakuthibitishi kitu kipo au hakipo.
Let me get this straight – ukiingia jikoni ukaona moshi unafuka, utasema “Ah, siwezi kuthibitisha kama kuna moto, maana kuona si uthibitisho”? Mkuu hiyo si falsafa, hiyo ni kuchanganyikiwa kwa akili za kutafuta deep meaning kwenye jambo rahisi

Unavyosema "vitu vinaonekana lakini havipo" – unamaanisha Instagram models? Au zile likes za watu wasiojitokeza real life?

Yes, kuna vitu havionekani lakini vipo – kama stress, oxygen, au utopolo huu wa hoja yako – lakini hiyo haimaanishi kuona haina maana. Seeing is not always believing, true – but sometimes, seeing is the very alert your brain needs to survive.

Kwa hiyo, next time ukiona gari linakuja kasi barabarani, kumbuka tu hoja yako “Kuona si kuthibitisha kuwa ipo.” Then uende ukasimame katikati ya barabara kwa imani. Tutaandika ripoti kwa hekima zako.

Vision isn’t perfect, but dismissing it kama useless ni kama kusema GPS si muhimu kwa sababu kuna watu walifika bila ramani. Come on, my guy. Think twice before you unsee common sense.
 
Personal experience ni logical fallacy. Wewe hujajua tu.
Si kila personal experience ni logical fallacy — huwezi kukataa ushahidi wa mtu kwa sababu tu ni wa kibinafsi. Sometimes personal experience is valid evidence, especially kama inathibitishwa na patterns au data nyingine.

Dismissal bila sababu ni intellectual laziness.
 
we upande wako upi
 
Kuna nyota zinaonekana zipo lakini hazipo.

Kuziona zipo hakuthibitishi zipo.

Mimi nipo lakini hunioni kuwa nipo.

Kutoniona kuwa nipo hakuthibitishi kuwa sipo.

Kuna vitu vinaonekana vipo lakini havipo.

Kuna vitu havionekani kuwepo lakini vipo.

Kuona au kutoona hakuthibitishi kitu kipo au hakipo.

Huelewi wapi?
 
Jibu lipo ndani ya maelezo niliyo toa.
Wapi? Weka maneno yaliyojibu swali hili.

Kwa nini swali lako ni "nani"?

Umekuta jani la muembe mlangoni mwako.

Hujui limefikaje.

Unauliza nani kaliweka.

Kwa nini unauliza nani?

Ikiwa jani limepeperushwa na upepo tu huoni kuwa swali lako la "nani" litakuwa limejielekeza vibaya?
 
Katika logical fallacies kuna fallacy hiyo ya anecdotal evidence, personal experience.

Unabisha?

Kama kuna pattern zaidi ya personal experience hiyo si personal experience tena, tutaangalia hiyo pattern na logic yake.

Inaonekana hata wewe mwenyewe katika kuitetea personal experience unaondoka kutoka personal experience na kwenda nje yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…