Kama mwanamke hajakuomba pesa, usijipendekeze kumpa. Kuomba ni sehemu ya kujishusha kwako

Kama mwanamke hajakuomba pesa, usijipendekeze kumpa. Kuomba ni sehemu ya kujishusha kwako

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
KAMA MWANAMKE HAJAKUOMBA PESA USIJIPENDEKEZE KUMPA. KUOMBA NI SEHEMU YA KUJISHUSHA KWAKE

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Usipendi kujiongeza kwenye ujingaujinga. Mpe hizo hela mama yako au Baba yako kama yupo kama unajihisi unakiherehere. Au kama ni wale wakujipendekeza jipendekeze kwa Mamaako.

Mwanamke mwenyewe sio mkeo. Hujamuoa. Hana mtoto wako. Kiherehere cha nini Bro.

Hakuna tuzo ya kiherehere Bro. Tena huna chochote cha maana utapata kwa kujikomba kwa kutoa pesa bila kuombwa.

Muache akuombe. Tena akikuomba mcheleweshee hata siku Tatu au wiki nzima.

Moja ya njia ya ku store power yako ni kutoitoa na kuwa mrahisi rahisi.
Wewe nenda serikalini ukaombe msaada uone kama kama watakupa harakaharaka. Lazima uwekwe benchi, uzungushwe na ukisusa shauri yako hakuna anayejali.
Mamlaka ziko hivyo.

Mungu ukimwomba hawezi kukujibu papoose hapo. Wewe nani? Hata kama anakupenda vipi hakujubu papo hapo.

Mwanamke kama hajakuomba usitoe pesa. Lazima akuombe. Tena akikuomba mcheleweshe.
Kumcheleweshe kunamfanya awe lower, awe chini, akae kwenye nafasi yake, unamkumbusha kwamba wewe ni nani. Na yeye ni muombaji tuu.

Kuna majinga yanatishiwaga na wanawake, oooh! Usipotoa pesa wengine watoe. Waache wengine watoe kwani wanatoa kwenye hela yako? Waache.

Oooh! Utaibiwa mwanamke. Hivi wanawake walivyojaa huko mitaani mtu anakuwaje na hofu ya kuibiwa. Unaibiwa mtu mzima na akili Zake.

Mwanamke akikuambia hivyo, mwambie fungasha virago, mpe kadi nyekundu. Akafie mbele huko.

Hela yako bado mtu akupelekeshe. Zinakutosha kweli.
Huyo mwanamke anayekutishia mwambie kwa laki moja unaweza kuwapata wanawake kama yeye hata watano. Hivyo yeye kama ni kusepa asepe.

Vijana wakiume, msiwe legelege, mioyo yenu isiwe laini, huo ni ushoga.

Sio lazima uwe na mwanamke yeyote kwenye hii Dunia. Narudia sio lazima.
Sio lazima nasema sio lazima.
Kuwa na msimamo wa Kitibeli kuwa mwanamke yeyote mwenye sifa ulizoziweka, atakayefuata masharti yako na ambaye atakubali mifumo yako atakuwa mkeo.
Na baadaye akizingua utamfukuza bila vikao.

Oooh! Sijui maswala ya kuzikana.
Sijui ninampenda sana. Hivi umekuwa mtoto anayebalehe wewe. Watoto waliobalehe ndio wanamioyo hiyo. Ukifikisha miaka kuanzia ishirini kuendelea moyo hauna kazi, moyo unatakiwa umilikiwe na Akili yako.sawa Kijana.

Niliwaambia, kama mwanamke hawezi kujilipia nauli achana naye. Huyo hajakupenda. Wanawake wakipenda hawezi kukosa elfu 20 kuja kukuona Ghetto kwako.

Ninasema hivi kwa sababu nimetoka huko Mlipo ninyi.

Usikubali kutishwa na vitu vya kitoto, vyakijinga. Wewe ni mwanaume sio mdoli.

Hajakuomba pesa. Usimpe.
Kumpa ni kujishusha.
Anashida muache aeleze mwenyewe. Kama haelezi hata kama unaona shida yake usimuulize. Jifanye hauoni. Ndivyo Watibeli tunavyofanya mambo yetu. Na ndio maana tumefanikiwa.

Usijifanye unahuruma huruma. Wewe ni mwanaume jielewe boya wewe. Mwanaume na huruma wapi kwa wapi.
Huruma mhurumie mkeo, na watoto na wazazi wako huko
Tena huruma za akili sio upelekwe pelekwe.

Kwa sababu wanawake wanasura kama paka. Wanaweza kuigiza kama Ngedere. Kiasi kwamba ukileta utoto utawaonea huruma. Na watakuchezea akili yako na kukumaliza.

Namaliza, lazima ujue mwanamke atahakikisha anakuvuta kwenye mihemko na hisia kwa sababu ndipo nguvu zao zilipo. Huku wakikutoa kwenye mantiki, reasoning ili usifikiri kwa usahihi.
Na ukishaingia kwenye huo mfumo umemfuata mamba kwenye kina kirefu. Lazima wakuchape tuu.

Mimi nimemaliza.
Sabato Njema.

TaikonMaster
Kwa sasa Mbezi, Dar es salaam
 
Mimi sipendi kuomba hela nataka atoe yeye mwenyewe,
Kwani hajui kama mimi nina mahitaji yangu muhimu hadi asitoe mpaka aombwe hii ni tabia mbaya, If a day comes nikipata mwanaume who gives me money bila kumuomba,never never sitomuacha aende.
 
Mimi sipendi kuomba hela nataka atoe yeye mwenyewe,
Kwani hajui kama mimi nina mahitaji yangu muhimu hadi asitoe mpaka aombwe hii ni tabia mbaya, If a day comes nikipata mwanaume who gives me money bila kumuomba,never never sitomuacha aende.

Mimi najua unashida.
Nakuona huna nguo,
Nakuona umechoka.
Lakini kama hujaomba kamwe siwezi kukupa pesa.

Sisi Watibeli hiyo kanuni inatusaidia sana hasa kwenye future life

Wewe kama unashida nini kinakuzuia kuomba kama sio kiburi?

Huna, unashida, kwa nini usiombe?

Subiri huyo mwanaume mwehu atakayekuja kukupa bila wewe kumuomba.

Sisi Watibeli utaisoma namba, ukileta kisirani tunakikata kama Ngariba vile
 
Mimi sipendi kuomba hela nataka atoe yeye mwenyewe,
Kwani hajui kama mimi nina mahitaji yangu muhimu hadi asitoe mpaka aombwe hii ni tabia mbaya, If a day comes nikipata mwanaume who gives me money bila kumuomba,never never sitomuacha aende.
Utampata wapi!!
 
Endelea kujifariji wenzio wanatoa huku! 🙄

Unafikiri vinegar wakipigwa wenye akili inawauma?

Ilimradi hawatoi kwenye mfuko wangu.

Inajulikana tangu zamani, wanaume wengi wanawaabudu wanawake na kuwatumikia kwa mali na miili yao.

Lakini sio sisi Watibeli.
Sisi ndio tunatumikiwa
 
Unafikiri vinegar wakipigwa wenye akili inawauma?

Ilimradi hawatoi kwenye mfuko wangu.

Inajulikana tangu zamani, wanaume wengi wanawaabudu wanawake na kuwatumikia kwa mali na miili yao.

Lakini sio sisi Watibeli.
Sisi ndio tunatumikiwa
Basi sawa,

ila atakayetoa napokea, asiyetoa namuomba vizuri tu bila kupepesa jicho lol!
 
Back
Top Bottom