Kama Mwanaume haupaswi kula chakula kingi nyumbani heshima yako itashuka

Northern sAwa southern wanapiga king balaa
 
Mshua alikua anasema, ukiweza kucontrol table manners bas hata tabia ya mtoto itakua nzuri anavoendelea kukua. Nnachokumbuka ni kunyimwa kutumia mkono wa kushoto, na kwa kiburi changu nilikua nasema siku nikianza kushika hela yangi hakuna wa kuniambia kitu. Well, nlipomaliza kidato cha 4 miaka hiyo nkaanza kupiga job na kushika hela yangu japo ni kidogo. Baas nkarud kwa fujo kula kwa mashoto yangu. Mpka leo ikitokea nmeenda kwa wazee natumia lefti yangu japo sio kwenye ugali. Naonaga ananicheki tu lakini kwakua nshakua mkongwe baaas hakuna kelele
 
Siku hizi hayo yamepitwa na wakati familia nzima inakula msosi heavy kwahiyo baba huna cha kuwapa watoto maana ulichokula ndicho wamekula muda mwingine wamekula na mengine extra zaidi yako.
Siku hizi watoto wanapewa sana priority ya kula misosi heavy kuliko hata baba. Au familia nzima kula vitu heavy. Enzi za baba anakula vilivyonona wengone wanakula vichwa vya samaki zishapita.
 
Dah umenikumbusha mbali sana ww jamaa, enzi hizo mshua anawekewa masamaki sato wale chukuchuku maana alikuwa anasumbuliwa na sukari, mara nyingi vichwa alikuwa hali kwa hiyo lazima aniite anikatie likichwa langu na nilikuwa nayapenda balaa ndiyo aanze kula. Alikuwa ananikubali kinyama continue RIP mzee
 
Unakuta Zee lishatandika kilo nzima ya mbuzi,ndizi 5 na likashushia na konyagi huko lilikotoka.hiyo hamu ya kula home itatoka wapi?
Afu yaelekea humu jf watu wengi mmetoka kwenye familia zenye dhiki ya chakula?how comes mtu ale abakize then ndio akupasishie wewe makombo?kwetu sisi chakula kilikua kingi tu hakukuwa na mtu ana time sijui ya kuvizia mshua abakize msosi.
 
Ni sijaona mantiki ya mtoa mada. Mimi ni Baba wa Familia nina watoto 5. Chakula kipo kinginhuku kijijini kwetu na mimi kama Baba najitahidi kuhakikisha msosi ni wa kusaza kwa watoto na sina utaratibu wa kula mtaani labda nisafiri kikazi. Sasa nishindwe kula kwangu eti naogopa watoto hawataniheshimu ila nikale Barabarani vyakula vinavyowekwa hamila?

Hiyo ni kwa ajili ya familia zenye uwezo wa chini. Nyumbani kwangu najiachia bwana, na watoto nao wanapiga sima lao tena huwa tunakula pamoja. Mara nyingi ikiwa usiku, namwambia mama yao weka kwenye sinia tule na watoto wetu kwa kushare chakula na mboga pamoja.
 
Hiyo ya kuachiwa sio makombo wala familia maskini. Kwa zamani, huo ulikuwa utaratibu tu wa wazee wetu. Baba alikuwa mfanyakazi na alikuwa anajiweza ila ni raha Baba unapoachia chakula kwa watoto hata kama walikuwa na kushiba. Wengi wetu tumekuwa hivyo toka zamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…