Ni sijaona mantiki ya mtoa mada. Mimi ni Baba wa Familia nina watoto 5. Chakula kipo kinginhuku kijijini kwetu na mimi kama Baba najitahidi kuhakikisha msosi ni wa kusaza kwa watoto na sina utaratibu wa kula mtaani labda nisafiri kikazi. Sasa nishindwe kula kwangu eti naogopa watoto hawataniheshimu ila nikale Barabarani vyakula vinavyowekwa hamila?
Hiyo ni kwa ajili ya familia zenye uwezo wa chini. Nyumbani kwangu najiachia bwana, na watoto nao wanapiga sima lao tena huwa tunakula pamoja. Mara nyingi ikiwa usiku, namwambia mama yao weka kwenye sinia tule na watoto wetu kwa kushare chakula na mboga pamoja.