Kama Mwanaume haupaswi kula chakula kingi nyumbani heshima yako itashuka

Kwetu sie huu utaratibu haukuwepo ndio maana nashangaa.
 
Au na mzee wangu atakuwa hivyo make ana mwili mkubwa ila anakula chakula hakiendani na mwili wake yaani maswala ya kula hayazingatii na akiwa home hawezi kula peke yake kama sio mkewe basi sie vihelehere tunaenda kumlisha baba chakula

[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Kwetu sie huu utaratibu haukuwepo ndio maana nashangaa.
Huo ni utaratibu wa familia za WAPUMBAVU zilizokuwa zinaongozwa na wazee WAPUMBAVU. Ni ujinga sana kusifia haya mambo. Ni mambo ya aibu watu wanatakiwa wawe wanaficha maana hapa conclusion tunayopata ni kuwa chakula kilikuwa hakitoshi. UMASIKINI MZIGO
 
Nyie ndio wale nyumbani umeacha hela ya mchicha huko umekula nyama choma na bia au vizuri vizuri.
Halafu akitengewa anaonja onja anasema ameshiba kumbe keshajilia vinono huko atokako.
Sasa unajiuliza hiyo hela aliyoenda kutapanya huko si angeacha tu kwa familia wakala vizuri kwa pamoja.
 
Kweli kabisa mkuu
 
Yawezekana hii ni sababu nyingine ya wanaume kufa mapema.Kujitwisha huruma na kufanya maigizo yanayoumiza aka "fujo inayoumiza/ua/tesa/kondesha.
Unafikiri hawali basi
Wengine wanakula huko watokapo wanakuja nyumbani wamejishibia na kama kumepikwa chakula sio kizuri ndo kabisaa anaishia kuonja.
Halafu wangine wana tabia mbaya nyumbani wanaacha hela ya mawazo halafu huko mtaani wanajilia vinono.
Mtoto hajui alikula kuku lini au samaki ila baba hamalizi wiki hajala hivo vitu.
 
Mzee alikua mjanja alikua anakwepa kulishwa sumu au kuwekewa limbwata.

Ndio maana anaonja halafu anawaachia na nyie ili kama ni madhara mpate wote au mhusika aogope kufanya hivyo kwani madhara yangekua makubwa.
 
Siyo kuvizia msosi maana sio kila wakati unapasishiwa chakula kuna time chakula kinamwaga pointi ni kuwa mwanaume hupaswi kula sana ili kujijengea heshima yako.
 
Heshima sio kwa watoto pekee ni kwa familia nzima hususani mama mtu inabidi awe na hofu ya kukupoteza wabaki na imani maisha yao bila wewe ni kipengele lakini ya kwako bila yao still yataendelea tena comfortable kabisa.
 
Yaani ule afu ubakishe ndo uwape watoto? Huo ni upendo wa wapi? Mzee wako alikuwa ni MPUMBAVU
Wewe mzee wako atakuwa mchoyo unakulaje bila ya kuwa na uhakika ya kuwa watoto wako wameshiba
 
sio rahisi kutenganisha familia za kitanzania na umasikini hata kama wewe kwenu zilikuwa zipo ila kuna mjomba, shangazi, baba yako mkubwa alikuwa masikini.

Huo ni utaratibu wa kawaida kabisa baba kuhakikisha familia yake sio imekula tu bali imekula na kushiba somo kubwa ni kuwa unapokuwa kiongozi wa familia lazima uhakikishe wategemezi wako wanapata basic needs hususani chakula ili kujenga heshima ndani ya familia.
 
Mtoto akila heavy inamsaidia sana kukua. Baba akila heavy, sababu tayari amekuwa anapata obesity. Na kama mtu ulidumaa utotoni halafu ukaanza kula heavy ukubwani ni hatari sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…