Kama Mwanaume haupaswi kula chakula kingi nyumbani heshima yako itashuka

Kweli hasa mbele ya watoto baba wa kweli mwenye kujali ataacha watoto washibe kwanza ndio ale yeye.
 
Ule ushibe hakuna shida..sasa hiyo tunaiitaje nidhamu ya woga au? Yaani uminyane uwatafutie halafu kwenye kula eti uzuge..? Hapana nadhani inafaa kila mtu ale ashibe lakini sio ile kuvimbiwa hapana..lakini sio uguseguse then ukale vichochoroni.
 
Mi sikumbuki ni lini nimekula na Watoto ili niwaachie..Mara nyingi naondoka wamelala narudi wamelala.
 

Ndio maana mada za watoto kuwa viburi jeuri na wakienda ugenini wanawaaibisha haziishi ni kwa sababu hizi

Wengine kuna desturi familia zinakuwa nazo, mfano mwanamke hali firigisi na ni ya baba hiyo na asipoila yeye ni mtoto Wa kiume ataila. Kingine baba ni mtu Wa kuchelewa kwa hiyo anatengewa chakula kwenye hot pot yake na hakuna Wa kuigusa

Watoto tulilelewa kwa kuwekewa limits na boundaries za kuziheshimu katika familia

Siku hizi watoto wanafugwa hawalelewi na kwa sababu wengi mnaona huo ndio upendo endeleeni lakini mjue Tu, kuna vitu vya kuviondoa lakini si vyote ni vya kupuuzwa
 
Hakuna kitu kama hiko. Mimi kama Baba najua wajibu wangu. Eti niache kukaa nyumbani na kula nyumbani kwangu niende kudhurura usiku tena ninaishi sehemu yenye baridi kali alafu sinywi pombe wala sina marafiki mtaani ili niwekewe chakula kwenye poti.

Sijajua kama una familia mkuu, mimi watoto wangu hawajawahi na jawatawahi kunitia aibu na wala siwalei kizungu wala kimaya mayai. Kuna muda wa kufoka, kucheka,kupiga n.k. mchana kutwa nzima nashinda kazini, watoto wapo shuleni eti na usiku nisikae nao wala angalia kazi zao za shule kisa waniogope.
 

Safi na hongera sana kuwa "modern father" 👏👏

Ila kama ulivyojitetea hapa na baba zetu wangepewa nafasi bhasi wangekuelekeza pia kwa hiyo ni vyema pia ukajifunza kuheshimu tamaduni na desturi za watu wengine kuliko kutoa conclusion kuwa hawana chakula au ni maskini

Niiweke kiufupi kwa namna hiyo tu mkuu 🙏🙏
 
Haya bwana mkubwa kuwa na siku njema.
 
Mzee wangu ubwabwa nusu kilo na kombe kubwa la chai kwake ndio kifungua kinywa, hugo mzee anakula kama kiwavi jeshi,,kama mtu anaona mzee wake anaweza, aseme tuandae mechi ya kirafiki hahaha..
 
Mzee wangu ubwabwa nusu kilo na kombe kubwa la chai kwake ndio kifungua kinywa, hugo mzee anakula kama kiwavi jeshi,,kama mtu anaona mzee wake anaweza, aseme tuandae mechi ya kirafiki hahaha..
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 

Huna heshima kwa wazazi wako, unamkomoa mzee wako? Alifanya kwa nafasi yake, ni zamu yako sasa kufundisha watoto wako.
 
Huna heshima kwa wazazi wako, unamkomoa mzee wako? Alifanya kwa nafasi yake, ni zamu yako sasa kufundisha watoto wako.
Yoooo, my nigga chilll bruh.. nakosaje heshima? Sijamdharau in any way. Is it a crime kutumia mkono ambao ni dominant kula?
I think we ni wale watu ambao wanaamini ukila kwa mkono tofauti na kulia then unakosea. Then why people are born left handed?
Ntawafundisha wanangu vitu vingi sana, tena vingi tu kutoka kwa baba yangu. But it doesnt mean kua ntaacha kuwaelejeza vitu ninavyoona ni sawa.
Its a shame kwa wewe kuona kua kutumia mkono wa kushoto kula ni kosa while huo huo ndo unaandikia na kuchezea mpira.
Wake up!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…