Kama Rais hataki kufanya kazi na Kassim Majaliwa amuombe ajiuzuru kama Philip Mpango

Kwenye Mkutano ulihudhuria kufanya nn kama haya yote unakuja kuyaongelea huku JF.

Wewe na mama hakuna tofauti, ni kwamba una maslai binafsi na Majaliwa
 
Na kama waziri mkuu Majaliwa hapendi kufanya kazi na Rais Samia aandike barua ya kujihudhuru.
Majaliwa amekaa ki-kutaka kugombea urais sana.
Baada ya uchaguzi mkuu, huyu bwana atakuwa mbunge wa kawaida au hata raia wa kawaida.
 
Wakulaumiwa ni Mabeyo, watu walishamaliza kazi.

Mobeyo alitimiza wajibu wake kwa kulazimisha katiba ifuatwe, Kwa sababu hata walio kua wana taka otherwise ilikua ni kwa maslai yao binafsi SIO MASLAI YA TAIFA HILI.


Wajumbe wa kamati tuu, Ndo wamekosea kwa kukubali kuisigina katiba yao ya CCM.
 
Mobeyo alitimiza wajibu wake kwa kulazimisha katiba ifuatwe, Kwa sababu hata walio kua wana taka otherwise ilikua ni kwa maslai yao binafsi SIO MASLAI YA TAIFA HILI.


Wajumbe wa kamati tuu, Ndo wamekosea kwa kukubali kuisigina katiba yao ya CCM.
Sawa lakini Kama kizimkazi, anaweza kuvunja katiba ya chama, hawezi kuvunja Katiba ya nchi?
 
Umeandika ujinga sana,kwa hiyo ww ukitaka majaliwa awe Waziri pia awe makamu wa Rais
 
Unalalamikia hilo!
Mwaka 1984 baada ya kifo cha aliyekuwa Waziri mkuu Edward Sokoine Mwalimu alimteua Salim Ahmed Salim kuwa Waziri mkuu lakini mwaka 1985 alipoingia Mzee Mwinyi alimteua Joseph Warioba kuwa Waziri mkuu na akamteua Salim kuwa Naibu Waziri mkuu.
Kama ulikuwepo ulionaje hilo hilo?
 
KM ni mtu poa anapotezwa na washenzi wachache
Mapoyoyo ya JF hasa jukwaa la siasa tunajuana. .

Inakera mnapotokea watu kama nyie, instincts says mnajua zaidi; halafu amtoi full story hata kwa hizi burner ID’s.

Tuelimishe nini kinaendelea huko sio kuandika kama walinzi wako wanasoma unachoandika (what a coward).

Jiachie kiongozi, ili ni jukwaa la elimu pia; gademu.
 
Kama Mijitu yenyewe haijielewi tuifanyaje?? Kweli nyie kwa akili zenu mnaona kuna serikali ?? Kuna barabara ziliharibiwa na Mvua ya mwaka jana mwezi 4 mpaka leo ziko vile vile huduma zote zimerudi hovyo kama enzi za kikwete hovyo kabisa kabisa lakini unaambiwa kuna kazi imefanyika kubwa
 
Watanganyika waelimishwe jinsi rasilimali zao zinavyotapanywa bila kuwanufaisha, naamini somo likiwaingia hata ccm wenyewe wataukataa huu ukoloni.

Bila shaka ubovu wa muungano itakuwa moja ya ajenda muhimu chini ya uongozi wa Lissu.
Tatizo taasisi ya urais imepewa u mungu mtu, hata mbuzi akikalia kiti hicho anakuwa juu ya yote atafanya atakavyo hakuna wa kuinua kamdomo
 
Sioni shida na hakuna ulazima wa PM kuwa Vice president. Na pia majaliwa kakaa kwenye uPM awamu mbili hapo tu apumzike kama wengine maana toka enzi za mkapa hakuna PM ambaye amewahi kupanda cheo kuzidi hapo, kuanzia Sumaye, Lowassa, Pinda wote hawakuzidi uPM.
 
Hakuna kosa mnalotendea watanzania kama kuishanikoa CCM licha ya maovu yote ya miaka nenda miaka rudi.

Mngeikataa CCM, yote haya yasingetokea.
Mkuu unapo fukuza mke lazima unaye mbadala wake.
Sasa Kuikataa CCM ni bonge la kosa maana bado hayupo mbadala wake waliopo bado wana safari ndeefu ya kujifunza utulivu na mengine mengi.
Kwa sasa CCM ndiyo CHAMA CHENYE NGUVU .
 
'Shikamoo' yako kwetu haiwezi kuondoa logic ya thread, jirekebishe.

Umeandika madini tupu, lakini imekuwa kama umetoka nchi za nje umefika leo na ulikuwa hujui kinachoendelea katika siasa za uongozi wa Samia.

Team Magufuli keshawang'oa takribani wote, ila Majaliwa alionewa aibu za kuua nyani ndo kisa cha kuwekewa Naibu waziri mkuu cheo ambacho hakipo, maana yake hatakiwi.

Sasa mtu asiyekupenda atakuteuaje tena kukusogeza karibu yake zaidi?

Kipindi cha utawala wa Magufuli na kwa namna ya utendaji wa Majaliwa ulivyokuwa wa kutukuka, kila mtu alihisi kuwa huyu mtu anaandaliwa kuwa Rais ajaye.

Kifo cha Magufuli kilizika na paformance ya Majaliwa, sasa kawa simba kibogoyo atishaye lakini hawezi kufanya lolote hata ukimchezea sharubu zake.

Kwa hiyo mchawi wenu anayewagonganisha vichwa ni kizimkazi.

Lakini cha ajabu kila uchao ni kumsifia kwa kumwabudu wakati akikanyaga katiba hadharani.

WanaCcm mmekumbwa na nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…