Kama Rais Samia ameshindwa kazi basi ajiuzulu maana hali inazidi kuwa mbaya

Jembe halimtupi mtu nenda kalime kama unataka usinunue kwa bei hiyo uliyoitaja.
Yalipokuwa yakiuzwa 1500 jembe lilimtupa mkulima.?

Leo wanatuuzia 3600 kg, halafu wakienda kununua vifaa vya ujenzi wanakuta moto! Pembejeo rushwa kibao, huduma za hospital dawa hakuna na rushwa njenje!

Hapo bado jembe halijamtupa?
 
Kwa mafisadi kama nyinyi sawa!
Miaka mitano ya utawala wake kulikuwa hakuna ajira,kapora uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020,Kaingiza wale wanawake wahuni 19 Bungeni,katusababishia majanga mengi leo Mama Samiah anahangaika namna ya kuboresha nchi iliyoharibiwa na yule Kibaraka wa shetani.
 
Yalipokuwa yakiuzwa 1500 jembe lilimtupa mkulima.?

Leo wanatuuzia 3600 kg, halafu wakienda kununua vifaa vya ujenzi wanakuta moto! Pembejeo rushwa kibao, huduma za hospital dawa hakuna na rushwa njenje!

Hapo bado jembe halijamtupa?
Heri ya leo Wakulima wana enjoy bei ya mazao imepanda.
 
Nilisikia alipotoaka China alienda nchi GANI sijui ,hivi kaisha Rudi, au bado kwa kuanzia apo ,
 
Namba nne imesababisha nipaliwe muhindi wangu wa kuchoma
 
Duh raisi ajiuzulu kwa vifurushi vya internet? kwamba watanzania wote maisha yao yanategemea internet ama mm sijaelewa
Mpaka leo hufahamu kwamba suala la mitandao ya simu ni jambo kubwa sana hapa nchini?

Hivi unajua kwamba uwekezaji kwenye hiyo sekta ni zaidi ya trilioni 8 na kodi inafika karibu trilioni 2 kwa mwaka huku kukiwa na watumiaji zaidi ya milioni 30?

Hii sekta inagusa moja kwa moja uchumi wa watanzania zaidi ya nusu karibu kila siku.
 
Mengine kama mfumuko wa bei, tatizo la maji na umeme hujayaona!!!???
 
Ukitoka misri ataenda Morocco maana nasikia huko pia kuna mikopo ya riba nafuuu
Kukopa sio tatizo. Tatizo Ni kwamba zikishaingia nchini wanazigawana wachache. Umeona Ile clip ya afisa wa halmashauri ya Longido aliye jichotea milioni 200+ mkuu wa wilaya (dogo fulani mwenye kiburi na dharau ) alivyoleta fyoko alichotewa 90M atulie. Sio maneno yangu, Ni maneno ya mbunge wa pande hizo.
Nenda halmashauri ya Bunda ukajionee mabosi wanavyochojichotea mabilion. Mnakumbuka Kuna mtu alijinunulia gari ya ova 450M sawa na dispensary au madarasa saidi ya kumi au complete sekondari school ya mikondo miwili.
Nani amebahatika kuona gari analotembelea Mwigulu? That car is over 500M. Zaidi ya Bei ya Basi la abiria 52.
Mtu mmoja anatembelea gari yenye Bei zaidi ya bus.
Huku Kuna watu hawawezi kununua kilo ya unga kwa sh 2000. Lakini who cares?
 
Hivi mnaona dar slam ndiyo Tanzania nzima? Yaani maji yakose dar basi wote tulie kuna maeneo umeme unakatika kwa nadra sana, yaani mtu unaweza kumaliza hata miezi miwili umeme hujawahi kukatika hata siku moja, ikitokea ukakata hata dk haiwezi kuisha umesharudi, kuna maeneo tangu dunia iumbwe hayajawahi kuona umeme, kuna watu unaposema internet haelewi unazungumzia nini, kuna jamii vizazi na vizazi hawajawahi kutegemea ajira za serikali.....kuna maeneo mtu hajawahi kuona ukame au ukosefu wa maji uliokithiri yaani kuna mito , madimbwi na mvua zinapiga kwa wakati kila mwaka..... hivyo hoja zako si nzito kiasi kumfanya Rais wa Taifa zima kujiondoa madarakani bali uanze na viongozi wa ngazi za chini ambao wanaishia kwenye eneo ambalo lina changamoto hizo
 
Umasikini umeuishi mpaka sasa umefikia hatua ya kuutetea na kujivunia.
 
Na mwenyewe anaona kaandika na kutoa maoni ya maaaanaaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…