Kama Ruto must go ilifeli Kenya, kwetu Tanzania Samia must go itafaulu kwa njia zipi?

Umesema vyema, ndiyo inavyotakiwa kuwa. Tuheshimiane hata kama hatukubaliani.
Ila machawa wa CCM wananipa wakati mgumu kuwaheshimu japo najitahidi!
 

Hakika , ndo maana huwa tunawaambia hapa kuwa sisi sio kuwa tunaitetea CCM Ila mbinu za kuikabili CCM zinahitaji kuukabili MFUMO kwanza na sio chama


Mfano hata ukiangalia nchi zinazofanya mapinduzi Mara nyingi mfumo ndo huwa unaruhusu hilo kutokea


Vijana kuandamana 29/10 huku wakijua adui yao mkuu no CCM that was a mistake .

Adui ulikuwa mfumo ambao ni security agency.


Kwahiyo hata ingetoka amri ya shoot to killl bado mfumo ungethibiti hiyo hali


Kwahiyo CCM sio tatizo la nchi hii Ila nchi MFUMO ndo Una shida .

Na mfumo ndo hupanga nani awe Rais na nchi iendeje .

Mpaka sasa GEN Z na washirika wake walibidi kujua hili swala .
 
Niambie wewe, sababu za jeshi kuingilia huwa zinakua ni zipi?
Jeshi huingilia kati pale serikali active ikiwa dhaifu,

Migawanyiko ikitokea (Waziri mkuu anataka A, Makamu anataka B, Bunge linasema C),

Maslahi yake yakiwa hatarini (Mishahara au likishushiwa heshima),

Machafuko makubwa kupita kiasi yanapotokea.
 
Aaah babe shida Tanzania umoja hakuna, utengano ni udhaifu
 
Mandamano yanaweza kusaidia na ndiyo mbinu pekee inayoonekana lakini tatizo ni Stategy za maandamano.

Ukipanic, Hasira ikizidi uwezo wako wa kufikiri ukaanza kuharibu mali za watu badala ya kufocus kwenye kushinikiza mabadiliko hapo ndipo mfumo mbovu unatafuta kiteteo.

Swali ni je, Tutaweza kuandamana bila kuruhusu hisia za kuharibu mali za tunaowadhania ni wadhalimu?
Tukiweza tu hilo, mfumo mbovu hauna pa kutokea tena.
 
Hujaelewa swali

Ameuliza sisi gen z wa Tanzania tutumie mbinu gani
 
Kwanini mtu auliwe au kupewa ulemavu kwenye maandamano wakati ana haki ya kikatiba ya kukusanyika na kujieleza.
Shida ukishapewa jina muhalifu au muhuni wanawesa kuua watu

Wale hawakuitwa waandamanaji waliitwa wahuni this is why tulipoteza ndugu zetu sana
 
Mbona kwa magufuli mlidhindwa. Mange alianzisha movement ya Magufuli must go ikafeli. Muache mama wa watu apige kazi
 

Ile 29/10 ulikuwa unaona watu wanawaza kuichoma nchi na sio maandamano

Nafikiri huu ndo ulikuwa mwanzo wa shoot to kill
 
Tusubiri tuone itakuwaje
 
Gentleman,
Tanzania hakuna anae weza kuwasapoti wavuta bangi na malofa yaliyobebwa ufala wa kifikra na mamluki pamoja na vibaraka wa magharibi kupora mali na kuharibu miundombinu ya umma na binafsi eti hiyo ndio haki yao
 
Tanzania siyo Kenya, kila nchi ina uniqueness yake. Hapo unapoleta mfano wa Kenya vipi mwingine akikuletea mfano wa Madagascar au wa Nepal au wa Mexico? Kinachotokea nchi moja si lazima kitokee nchi nyingine, we're all going through different ordeals and so we tackle them differently.
 
Tanzania na Afrika bado sana, inatukatisha tamaa vijana.
Sasa kujibu mada, unafikiri tutawezaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…