Unajua ukishakiri kua yesu ni bwana na mwokozi wa maisha yako unakua umetangaza vita na shetani, na shetani atajaribu kufanya kila njama za kukuporomosha hapo juu ulipo
Unajua kwamba shetani kapewa mamlaka ya kumjaribu binadamu na katika hili shetani kaamua kutumia huu ugonjwa kama jaribio ili kuwateka watu?
Unajua kukubali kusalia nyumbani kwa kuogopa maambukizi ambayo yamepangwa na shetani ni ishara kwamba shetani amekushinda nguvu na umekosa imani ya kupambana naye?
Unaelewa kwamba namna pekee ya kumshinda huyu shetani ilitakiwa yeyote yule ambaye amemkiri yesu kua bwana na mwokozi wa maisha yake ajitokeze katika wodi za wagonjwa wa corona kwa lengo la kuwafanyia sala ya toba kwa kuwashika vichwani?
Mnakumbuka kua ukiwa na yesu hakuna lishindikanalo maana amewaahidi kutengeneza njia mahala pasipo na njia?
Mbona hamponyi corona sasa? Pamoja na kukusanyika kwa siku zote hizo idadi ya wagonjwa inazidi kuongezeka? Kuendelea na mikusanyiko ya ibada hali tunajua wazi ugonjwa unaambukiza sana kutokana na mikusanyiko ni kumjaribu Mungu wala haina tofauti na shetani alivyomtaka Yesu amjaribu Mungu. Majibu ya Yesu kwa jaribu kama lenu ni haya (Lugha Kiingereza na Kiswahili):-
Matthew 4:5-7
"[5]Then the devil taketh him up into the holy city, and setteth him on a pinnacle of the temple,
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu,
[6]And saith unto him, If thou be the Son of God, cast thyself down: for it is written, He shall give his angels charge concerning thee: and in their hands they shall bear thee up, lest at any time thou dash thy foot against a stone.
akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
[7]Jesus said unto him, It is written again, Thou shalt not tempt the Lord thy God.
Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako."
Acheni kuwa mawakala wa shetani kwa kivuli cha Yesu.
Pia tambua kwamba Mungu yupo mahali popote na baadhi ya sifa zake ni hizi:-
1. God is omnipresent - Mungu yupo kila pahali.
2. God is omniscient - Has unlimited knowledge; Uelewa wa Mungu hauna mipaka (hakuna asichokijua).
3. God is omnipotent - God has unlimited power; Mungu ana nguvu/uweza usio na kikomo.
Ndiyo maana hata mkuu wa katoliki (Papa) anawaambia waamini wake Waungame popote pale walipo Mungu yupo na anawasikia badala ya kwenda kwa kasisi/padri kama wengi walivyozoea.