Kama shule za Private zikifanikiwa kumfanya kila mtoto wa primari kupata A nini kitatokea?

Kama shule za Private zikifanikiwa kumfanya kila mtoto wa primari kupata A nini kitatokea?

Ni hatari.
Nilifanikiwa kukutana na dogo msichana ambaye anaongoza darasa zima. Nikamuomba anionyeshe njia yakusolve swali flani la kurahisisha.

Hajui njia ila anajua jibu. Nikagundua karibu wote hawajui na wala hwataki kujua njia ya kufukia kwenye majibu, wamekaririshwa ujanjaujanja. Ukiona hivi ujue ni vile. Walivyopewa mtihani wa kufanya kwa kuonyesha wamefikaje kwenye jibu hatua kwa hatua wote chali. Na mkuu wao na bosi akanuna anaona kama wanacheleweshwa.

Hadi nikamiss enzi zile za Swali, Kazi, Jibu.
Swali gani la kurahisisha? Ambalo mtu anajya jibu lakini hajui njia? Na je vipi ukibadili bamba,pia anapata jibu KWA usahihi bila kuonesha njia?
 
PI ni thamani ambayo haibadiliki na haitokuja kubadilika iliyogunduliwa na itumikayo katika mahesabu mbalimbali
Yaani 22/7 au 3.14
Kwahiyo mtoto angejibu hivyo jamaa angeridhika?
 
Balaa zito. Kuna katoto kanasoma la saba. Kana A za kutosha.

Nilikauliza PI ni nini kwenye hesabu.
Naomba anifundishe nielewe kuhusu PI.
Alishindwa kunieleza. Sababu amekaririshwa
PI ndio nini au unamaanisha pie ya 3.14&22/7

Kama ni hiyo ulimuonea sana mtoto kumuuliza hilo swali.
 
Kwani ni nini?

Pi ni jibu la kihesabu lisilobadilika linalowakilisha uwiano kati ya urefu wa mzunguko wa duara na kipenyo cha duara.

Duara lolote duniani liwe kubwa kama bahari ama liwe dogo kama sarafu uwiano wake kati ya urefu wa duara hilo na kipenyo cha duara hilo jibu huwa linafanana ambalo ni 22/7 ama 3.14

PI ni nguzo muhimu sana kwenye hisabati. Shule ya msingi lazima utoke unaielewa.. na form one inarudiwa tena kufundishwa sababu huwezi kuelewa hesabu za mbeleni kama huielewi PI ni nini ?
 
Tulia huyu huyu? Aisee
1696412265692.png
 
Ndio maana nimeanzisha back to Kayumba campaign
Kampeni ya kimasikini..

We pambana na hali yako bana. 🤣🤣🤣

Msiwapeleke watoto kwenye shule za vichochoroni..

Shule nzuri zipo na mnazijua.
 
Swali gani la kurahisisha? Ambalo mtu anajya jibu lakini hajui njia? Na je vipi ukibadili bamba,pia anapata jibu KWA usahihi bila kuonesha njia?
Nilichogundua wanafanya ila hawajui kwa nini wanafanya hivyo. Kuna mawili walikuwa tayari wameshakariri jibu au mwalimu aliwafundhisha kwa kukariri bila kujua kwa ninj ukate chini na juu.

Yaani mtu huyo
Anaweza kufanya
1+3
Ila ukimpa 3+1 umemvuruga.
Ni kipengere.
 
nilichogundua ni presha za ushindani.
Maana ukivuruga watoto wanahamishiwa shule jirani.
Kinachouza ni matokeo hivyo bora hata uwaburuze wapate A kwa lazima.

Wengine wakiona dogo kichwa ngumu wanamtimua mapema ili asijekuchana mkeka wao.
 
Muulizaji wa swali sijajua alilenga nini lakini PI ni thamani iwakilishwayo na 22/7 na 3.14
sio 22/7 na 3.142 ni 22/7 au 3.142, it is a constant, jamaa katoa maelezo hapa juu ila kimsingi hayana mantik yoyote.
 
Pi ni jibu la kihesabu lisilobadilika linalowakilisha uwiano kati ya urefu wa mzunguko wa duara na kipenyo cha duara.

Duara lolote duniani liwe kubwa kama bahari ama liwe dogo kama sarafu uwiano wake kati ya urefu wa duara hilo na kipenyo cha duara hilo jibu huwa linafanana ambalo ni 22/7 ama 3.14

PI ni nguzo muhimu sana kwenye hisabati. Shule ya msingi lazima utoe unaielewa.. na form one inarudiwa tena kufundishwa sababu huwezi kuelewa hesabu za mbeleni kama huielewi PI ni nini ?
Hayo maelezo ilikuwa nayo lasaba?
 
sio 22/7 na 3.142 ni 22/7 au 3.142, it is a constant, jamaa katoa maelezo hapa juu ila kimsingi hayana mantik yoyote.
Jamaa hajui pai kweli. Mbona hata sisi vilaza tuliifahamu na kuiogopa kwelikweli.
 
sio 22/7 na 3.142 ni 22/7 au 3.142, it is a constant, jamaa katoa maelezo hapa juu ila kimsingi hayana mantik yoyote.
Hebu nieleweshe hiyo 22/7 yangu ina tofauti gani na 22/7 yako.
Huko kwenye decimals nimekuelewa.
 
PI ndio nini au unamaanisha pie ya 3.14&22/7

Kama ni hiyo ulimuonea sana mtoto kumuuliza hilo swali.

Kwa sisi Tanzania Shule ya msingi kuanzia darasa la tano tunaanza kufundishwa elementary geometry. Yaani introduction to geometry. Ni lazima ufundishwe kuhusu PI kwanza. Ndipo unaanza kufundishwa kutafuta eneo, mzunguko ama ujazo wa duara.

Labda kama ulikuwa kilaza wa hesabu hivyo hata ukumbuki topic za primary.

Pia sio Tanzania tu.

Sylabus ya hesabu ya nchi yoyote dunia nzima. PI lazima ifundishwe kwenye elimu ya msingi.

Elementary mathematics kwa kiswahili ndio elimu ya msingi.. PI huwa inafundishwa kwenye elementary mathematics ili mtoto aweze kuelewa msingi wa geometry
 
Back
Top Bottom