Kama silaha zilizooneshwa ndio za Jeshi letu, bado tupo nyuma sana

Hujui hata mambo ya jeshi then unazarau jeshi la nchi yako linalolinda mipaka, mkuu punguza ujuaji wa kijinga.
Sio dharau mkuu. Nikisema fulani ana elimu ya darasa la saba na huyu ana PhD utasema namdharau mwenye la saba B. Yani kuwa muwazi kibongo inaitwa dharau. Nchi nyingine zinaita tenda inajadiliwa na bunge na vyombo vya habari vinahoji, watu wanaanzisha debate kushindanisha silaha gani wanunue kwa fungu walilonalo. Watu wanatoka wanaenda Dubai Airshow, Army Expo, MAKS Airshow na wakirudi wanasema ukweli walioona nchi inaamua.

Last week mpaka leo kuna matukio kadhaa. India kasaini mkataba wa kutengeneza assault rifle za Kalashnikov ya Russia. UAE imenunua Rafales 80 kutoka Ufaransa kwa zaidi ya trilioni 43 za kibongo. Finland imesaini kununua F-35 kutoka Marekani. Hizi zote zinafanyiwa mchuano mkali na tenda zinakuwa wazi na wananchi wana haki ya kuhoji.

Sisi hapa tukisema tunaitwa wajuaji na wajinga. Maana ya jeshi la wananchi haipo wala haizingatiwi. Ila Afrika ndo ilivyo hata ndoto tunazoota sidhani kama wazungu huota hivi
 
Uko sahihi lakini sijui unachonibishia ni nini. Unajua kama wakati huu kuna watu wako training ya silaha ambazo ni toleo jipya na hazijaoneshwa hapo uwanjani? Unajua kama kuna silaha tunazo na watu wameshapewa mafunzo tayari lakini hazijaoneshwa hapo?

Unasemaje kama silaha ndo hizi basi hatuna kitu?

Ukubali ukatae kuna silaha hununuliwa kwa dharura kulingana na mahitaji achilia mbali long term plan unazozizungumzia wewe.

Unajua kuwa kuna tabia ya soko la siri la silaha hasa baina ya nchi marafiki? au kwa kulinda maslahi ya nchi ngeni katika nchi yenye vita?

Mambo ni mengi linapokuja suala la vita. Si tu eti mikataba ya kuuziana silaha pia kuna kufake mikataba hiyo kuficha kufahamika kuwa nchi fulani ina silaha fulani.

Kwa kifupi tu.
 
Point
 
Silaha mpya ilizonunua TZ ni zipi!? A-100 hatujaziona zimeenda wapi!?
 
Hebu kazijaribu hizo silaha, kwani hazi ui?
 
Yaani hii ni kwel aisee... kuna kipindi tulikuwa tunatoka doria usiku ya maliasili. Njia tukiyopita ilikuwa ikatisha kwenye kambi ya jeshi sasa bhana tukasimamish2a huo usiku. Siku ndo nikaelewa kweli kuna wakati wazalendo wanatulinda usiku kucha sisis tumelala tu kama ngedere, tunachekelea tu amani tuliyonayo.... ila kimsingi nchi yetu inalindwa kwa dhati na ari ndo maana vyombo vya ulinzi na usalama siwez wadharau hata siku moja... akinikuta barabarani akanipa tena ntamshukuru...

Imagine watu wanahoj mtu kukamatwa kwa jamaa kabla ya kutenda uhalifu halafu, mtu mwingine anahoji kwani amefanya kosa gani hadi akamatwe.... jaman jaman... tuipende amani yetu na tuilinde kwa hali na mali... i wish hata nngetaman kuwa sehemu ya usalama... ili nam nionyeshe mchango wngu kwa nchi wa moja kwa moja...
 
Hilo jeshi la Ethiopia unalosifia..mbona limechezeshwa segere na Tigray
 
Kuna amani ni kwa sababu ya ukondoo wa watanzania. Na pia rushwa katika jeshi. Kimsingi jeshi limetekwa na CCM na watawala na kuwasaliti wananchi.
 
Nasema usidharau nchi hii kisa hizi siasa za kiccm ila Kuna mambo mengi hufanyika kulinda hii nchi sema Raia tunalaumu vile nchi yetu inausiri mkubwa kuliko unavoweza kufikiria.
Naamini tuko vizuri hvi vya Leo ilikuwa display tu kidogo, pia ukisema tujilinganishe sijui na USA mara Russia ni sawa na kulinganisha mbingu na ardhi
 
Ndo maana walichakazwa vibaya sana walipoenda kukabiliana na magaidi wa Mocambic pale Kitaya, wakatelekeza vifaru
 
Hakuna cha movie hapa Mzee. Jeshi letu lipo outdated. Tunatakiwa ku modernize. Tunaona display za silaha kwa majirani zetu. Uganda na Kenya.
Hao Waganda na Wakenya wanahenyeshwa na vijana kutoka Somalia si mchezo
 
Tofautisha silaha za maonyesho na za kivita.zile ni za kuonyeshea
 
Here again mzee!

Mkuu wewe ulitaka kujua Jwtz imenunua nini na ukajua? 2017 hadi 2020 kwa mfano
Mara nyingi ni vigumu kujua order zilizowekwa ni zipi labda ziwe ni kubwa na zimewekwa wazi. Ila wakati wa delivery ndio inajulikana. Haya mambo sio magumu inategemea na mtu anafatilia nini.

Watu wanafatilia utajiri wa mtu, mali zake, hisa na madeni sembuse silaha zenye regulations. Mimi hushangaa watu hujuaje vikosi, nakuwa nimekaa naangalia let's say Liverpool Vs Man City alafu mchezaji anapasha nje watu wanashangilia mtoe huyo X. Najiuliza wamejuaje X ndio atatoka na ni kweli anatoka yeye, wamejuaje X anapwaya. Huwezi ona nachangia kwenye mpira maana sijui.
 
Ndo maana walichakazwa vibaya sana walipoenda kukabiliana na magaidi wa Mocambic pale Kitaya, wakatelekeza vifaru😀
Magaidi wanastukiza na sio kuweza kupigana, Hakuna kundi lolote la kigaidi lenye kuweza kupigana na jeshi, Ingekuwa rahisi hivyo, serikali nyingi zingeshaanguka,gaidi ni SAwa na panyaroad wao uvizia na ushambulia
 
Jeshi la Mwaka 47
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…