Kama silaha zilizooneshwa ndio za Jeshi letu, bado tupo nyuma sana

Kama silaha zilizooneshwa ndio za Jeshi letu, bado tupo nyuma sana

Waasi wa yemen wanazitungua high tech drone za saudia kwa kutumia buk zilizotumika kwenye vita ya iran na iraq kuhusu mbabe wa ant drone sidhani kama kuna taifa linaifikia iran hata historia inazieleza kati ya irna na israel nani kazishusha drone nyingi tena zenye high tech hivi unaijua operesheni safina linalopaa drone za hezbullah zilovyo penya mpaka kwenye vinu vya nuke vya israel?
Story za vijiweni hzi
 
Haya basi!View attachment 2038292
View attachment 2038293

View attachment 2038294
Umeshajua nchi yenu wananunuaje silaha za kivita. Na sio hizi tu nyengine ni ndege vita za kisasa wamenunua ila hawazionyeshi. Hata hizi taarifa zikitoka Tz wanazikanusha. Na kuna nyengine walishirikiana na North Korea kwenye mambo ya kijeshi. Tz falsafa yao ya kijeshi hawaonyeshi silaha zao zote ama silaha za kisasa. Kama wengine wanafanya ni wao ila Tz hawafanyi. Kama mataifa makubwa yanafanya ujue wanafanya matangazo ya kuuza zana zao. Na marubani wengine walipelekwa Canada kwa mazoezi ya kujifunza zaidi.
Hakuna issue kama hiyo Mzee. Tanzania tungekuwa na silaha, haki ya nani ungeziona.
 
Kasome kuhusu Highway of Death pale jeshi la Saddam Hussein linafanya evacuation kutoka Kuwait ndio utajua umuhimu wa jeshi la anga. Kunakuwa na air denial na naval blockade ila hutosikia wanahangaika kuzuia ground movement mwanzoni. Jeshi la ardhini rahisi kuzuia likiwa halina air cover
Bora uandike kifupifupi hivi kuliko kupoteza muda kuwaandikia maelezo mareeefu sababu hawawezi kukuelewa kaka.
 
Na kama makomandoo ndio sina ya wale walio pelekwa kumlinda Mbowe, wanaokamatwa na mgambo wa polisi, tujitafakari.
Duh ila wakina kingai,Goodluck,Mahita wanajua kutesa aiseee,mpk komando kupiga yowe sio mchezo.
 
Nimetazama maazikisho ya miaka 60 ya Uhuru. Kwa silaha tulizoonesha zinanipa wasiwasi na uwezo wa jeshi letu.

Vitu vingi vilivyooneshwa ni silaha zilizotumika kipindi cha USSR.
Kuna BM 21. Kwa kweli tunatakiwa Ku modernize jeshi letu. Bado lipo nyuma sana.
Sasa wewe kwa akili yako utaweka silaha zako zote modern hadharani?
 
Mimi ni mfuatiliaji wa silaha za nchi mbalimbali. Hakuna silaha za kutisha hapo. Uganda na Kenya display yao inatisha Mzee.
Kinachotokea wakati wa vita huwa ni siri. Silaha zinazooneshwa hapo huenda usizikute kabisa vitani. Lakini vita itaendelea kwa kununua silaha usiku na kuingiza uwanja wa vita halafu ukashangaa mtanange wake.
 
Haya basi!View attachment 2038292
View attachment 2038293

View attachment 2038294
Umeshajua nchi yenu wananunuaje silaha za kivita. Na sio hizi tu nyengine ni ndege vita za kisasa wamenunua ila hawazionyeshi. Hata hizi taarifa zikitoka Tz wanazikanusha. Na kuna nyengine walishirikiana na North Korea kwenye mambo ya kijeshi. Tz falsafa yao ya kijeshi hawaonyeshi silaha zao zote ama silaha za kisasa. Kama wengine wanafanya ni wao ila Tz hawafanyi. Kama mataifa makubwa yanafanya ujue wanafanya matangazo ya kuuza zana zao. Na marubani wengine walipelekwa Canada kwa mazoezi ya kujifunza zaidi.
Oi there was no need for going the extra mile bruh!

Raia wamekalisha masaburi tu wanadhani hii amani iliyopo ni burebure tu.

Acha waamini kuwa hamna chochote tu, vijana wanachojua ni ubishi wa chadema na ccm tu bladifaken kabisa!
 
Hakuna cha low profile wewe. Kwanza wote hapa unaoona wana uelewa na silaha usidhani huwa wanaziona kwenye maonesho. Silaha sio vikombe kwamba utasafirisha umevificha.

Nchi inayouza silaha imesaini mkataba kutouza silaha kwa rogue militaries labda ziwe defensive. Ndio maana nchi kama Iran kuziuzia jet fighters ni ngumu ila Urusi ikijibana inaziuzia air defence systems. Kwa hali hii mauzo ya silaha yako monitored na taasisi binafsi kama SIPRI na Jane's Defense ambazo hutoa machapisho. Sisi tunaenda soma uko na kila silaha ukiwa unafatilia kuna sehemu ya kuona operators. Kama nchi haijakidhi vigezo ikiuziwa ni lawama, nchi ikiuza kwa kukiuka wanaweza kuiwekea vikwazo isiuze tena. South Africa ni nchi pekee ninayojua haijawahi uza silaha kwa nchi ya kutia mashaka, hata Canada wafuatiliaji.

Yani kama unavyonunua Bombardier ikajulikana. Hata ukinunua silaha itajulikana kwa wanaotaka kujua
Basi kwa uelewa huu kama walichoonesha ndo kilichopo tatizo litaendelea kuwepo!!
 
Vijana wengi wanaangalia movies zinawachanga sana, hawajui mambo kwa ground ni tofauti kabisa.

Tanzania ni nchi ya Kijamaa, mambo yake mengi ni siri, hicho wanachoonyesha sicho kilichopo...

Kila Mwaka bajeti ya wizara ya Ulinzi na usalama inatengwa tena ya kutosha, umewahi kusikia wametangaza kununua hiki ama kile...

Ukiona umekaa sehemu unashushia bia na nyama choma tena kwa amani kabisa jua kuna wanaume hawalali huko.
Vijana wengi wa sasa wakishakuwa na smartphone na user Id fake wanayoamini hawajulikani basi wanajua dunia ipo kama wanavyoitafsiri kichwani.

Ndio maana kuna watu ni wepesi sana kukejeli jeshi wakishashiba ugali. Hawajiulizi hata kwann tuna utulivu na madini yote haya? Ardhi yote hii?
 
Kuna uzi mwaka jana nilisema Kenya wana silaha kutuzidi watu wakanijia juu. Mada kama hizi huwa naongea kidogo mengine unapunguza makali, wewe uliona wapi duniani komandoo anabeba magogo mgongoni. Ukiwauliza hawa watakwambia ni kuonyesha ujasiri. Aisee, Israel ina wanajeshi wengine hata ngumi hawajui sasa fyatuka uingie nao vitani.

Last year walituonesha komandoo ana sufuria kabisaa. Leo angalau hawajaleta vituko
Nimeshangaa kinoma yaan commando anaenda na supply ya kila kitu, kama hawana support ya command yao
 
Hakuna cha low profile wewe. Kwanza wote hapa unaoona wana uelewa na silaha usidhani huwa wanaziona kwenye maonesho. Silaha sio vikombe kwamba utasafirisha umevificha.

Nchi inayouza silaha imesaini mkataba kutouza silaha kwa rogue militaries labda ziwe defensive. Ndio maana nchi kama Iran kuziuzia jet fighters ni ngumu ila Urusi ikijibana inaziuzia air defence systems. Kwa hali hii mauzo ya silaha yako monitored na taasisi binafsi kama SIPRI na Jane's Defense ambazo hutoa machapisho. Sisi tunaenda soma uko na kila silaha ukiwa unafatilia kuna sehemu ya kuona operators. Kama nchi haijakidhi vigezo ikiuziwa ni lawama, nchi ikiuza kwa kukiuka wanaweza kuiwekea vikwazo isiuze tena. South Africa ni nchi pekee ninayojua haijawahi uza silaha kwa nchi ya kutia mashaka, hata Canada wafuatiliaji.

Yani kama unavyonunua Bombardier ikajulikana. Hata ukinunua silaha itajulikana kwa wanaotaka kujua
Here again mzee!

Mkuu wewe ulitaka kujua Jwtz imenunua nini na ukajua? 2017 hadi 2020 kwa mfano
 
ndio uzuri wa Tanzania..

Kila Mtanzania ni dalali..
Kila Mtanzania ni tapeli.
Kila Mtanzania Mwanajeshi.
Kila Mtanzania lawyer.
Kila Mtanzania Mhasibu.
Kila Mtanzania mwanasiasa.
Kila Mtanzania Engineer.
Kila Mtanzania Tajiri hapa JF.
Kila Mtanzania Komando.
Kila Mtanzania mtalaa wa siasa.
Kila Mtanzania Usalama wa Taifa..
 
Huo ni ukweli ambao wengi watakuja kukupinga hapa yaani likitokea taifa lenye silaha advanced ni lazima tulie, watakuja hapa kukwambia jeshi letu tunalipima na waasi wa kongo, waasi wasio na silaha za kisasa wanaojificha misituni

Wenzetu kenya wanawekeza kwenye jeshi lao kila kukicha wananunua silaha za kisasa,hata rwanda pia wapo hivyo hivyo , kuna mandege yanapitaga hapa ya kivita hata milio tu unagundua ni za zamani
Vifaa vya jeshi vinasaidia nini watu hawana majii
 
Hakuna issue kama hiyo Mzee. Tanzania tungekuwa na silaha, haki ya nani ungeziona.
Hayo mawazo yako ila ukweli ni kwamba Tanzania huwa hawaonyeshi silaha zake mpya waziwazi. Kuanzia sasa ufahamu hilo!
Screenshot_20211209-155616.png

Baada ya hii ndiyo yakafanywa manunuzi ya silaha (picha za awali nilizo kuwekea juu). Mi 17 zilinunuliwa zikiwemo air defensive system S-300 kutoka Russia na hizi nilizozitaja ni baadhi tu.
 
Back
Top Bottom