Kama silaha zilizooneshwa ndio za Jeshi letu, bado tupo nyuma sana

Kama silaha zilizooneshwa ndio za Jeshi letu, bado tupo nyuma sana

Ndo yenyewe kaka, ni aibu kubwa mno.

Sijui nani utamtungua kwa Anti Aircraft Gun ulimwengu wa sasa, labda haya madege yetu ya miaka ya 60 ndo yanaweza angushwa na hizi takataka.

Uganda ana mashine matataa saaaana za angani, ana Sukhoi SU-30 Sita. Huyu akiamua hata Ikulu anadondosha mzigo na anatembea pasipojulikana.
AA gun zilitumika mara ya mwisho WW2 na kidogo Korean Wars. Hata Vietnam jet age na air to air missiles ndio zimeshika kasi hawakutumia AA system. Hizo labda udungue Bombardier
 
Screenshot_20211209-154425.png
 
Kuna uzi mwaka jana nilisema Kenya wana silaha kutuzidi watu wakanijia juu. Mada kama hizi huwa naongea kidogo mengine unapunguza makali, wewe uliona wapi duniani komandoo anabeba magogo mgongoni. Ukiwauliza hawa watakwambia ni kuonyesha ujasiri. Aisee, Israel ina wanajeshi wengine hata ngumi hawajui sasa fyatuka uingie nao vitani.

Last year walituonesha komandoo ana sufuria kabisaa. Leo angalau hawajaleta vituko
Watu huko nchi za mbali unaweza kuta mtu Koplo, Sajent ana degree au hata Masterz ama ana taaluma nzito mno.

Hapa kwetu ukiwa na Degree lazima ubebe manyota, ila wapiganaji ni wale darasa la 7, form 4 failures n.k sasa umakini ktk field unakuwa wapi?

Unaweza ukachukua maaskar wanne wenye elimu zao kisha ukawaringanisha na wacheza ngoma 4? Yaani mtu anavaa kombat kisa ana taaluma ya kucheza ngoma, kuchonga vinyago, fundi bomba n.k
 
Mzee mambo ya watu kupiganisha yalishapitwa na wakati. Sasa hivi ni technology ndio inapigana. Achana na mawazo ya kijima ya Nduli Idd Amin Dadaa.
Toka 2010 zaidi ya wanajeshi 2300 wa Marekani waliuwawa huko Afghanistan dhidi ya wanamgambo wa Taliban...

Kwa nini wasingetumia tecnolojia kupiganisha vita...

Leo unaambiwa Urus imepeleka wanajeshi zaidi ya 175,000 kwenye mpaka na Ukrane kwa nini wasingepeleka tecnolojia ndio ikapigane.?
 
Kama tunasema huwezi kuonesha siri ya ghala kwa maana ya zilebkali basi Kenya wako juu maana hizo tinazodisplay wao ni kwa ajili ya mazoezi ya mgambo wa jiji maana walishaziondoa kwenye hesabu ya silaha ghalani.
 
Upo sawa zana hizo za vita ni za enzi za USSR,lakini ukae ukijua Tanzania hatuna potential enemy,tangu utawala uliokuwa wenye sera za ubaguzi wa rangi kule Afrika ya kusini ulipoachia madaraka,tangia hapo nchi ya Tanzania haina adui wa moja kwa moja ambaye unaweza kumyoshea kidole kwamba huyu hapa,kwa hiyo hakuna hoja ya msingi ya kutumia mabilioni ya fedha za wakulima na walipa Kodi,kununua vifaa vya vita ambavyo vitakuwa vinaoza taratibu kwenye mabohari ya jeshi,hebu google uone ndege moja ya kivita mfano F16 inauzwa sh ngapi halafu jaribu kucompare hiyo hela na gharama za kujenga shule na kununua madawati,au gharama za kujenga vituo vya afya na kununua vifaa vya afya.
Mfumo kama wa nchi za India na Pakistan wa kuwa na jeshi lenye vifaa vya gharama kubwa sana vyenye teknolojia za Hali ya juu,wakati ambapo hakuna vita yeyote ni ukichaa ulio wazi kabisa.
Hayo mashule, madawati, hospital tunajenga kwa fedha zetu?
 
Hako kadude kadogo vile kenye bendera nyekundu mbili ni ka nini, ka APC au IFV? Sasa kana Impact gabi mbona hata hakaonekani kuwa na armour.

Hiyo Grad moja tulitumia kipindi cha vita ya Amin tena tulipewa kama msaada na USSR. Wanajeshi wa Amin walikuwa wanaiogopa na waliwahi tuma ndege ije kuushambulia ila ilikuwa inahamishwa kila ikifanya attack. Warusi wenyewe walizigundua WW 2 dhidi ya Wajerumani na ziliitwa Katyusha, Wajerumani wakaziita "Stalin's Organs"
Kwa sasa kuna modern version kama TOS.

Vifaru vyetu ni Chinese model flani nimeisahau niliona na Chad wanavyo. Vya sasa vitakuwa modernized ila ni type ya 1960s
Ni T series nadhan ni T -56 kitu kama hcho
 
Mtaleban hana mokorokoro lakini US mwenye kila aina ya silaha za kisasa kakimbia mchana kweupe.
US wa Kimara bonyokwa povu ruksa.
 
Toka 2010 zaidi ya wanajeshi 2300 wa Marekani waliuwawa huko Afghanistan dhidi ya wanamgambo wa Taliban...

Kwa nini wasingetumia tecnolojia kupiganisha vita...

Leo unaambiwa Urus imepeleka wanajeshi zaidi ya 175,000 kwenye mpaka na Ukrane kwa nini wasingepeleka tecnolojia ndio ikapigane.?
Kwahiyo unategemea wanajeshi wetu 27,000 ndio wapiganishwe kupambana na Su-30 inakuingia akilini kweli!?

We need to modernize our army.
 
Na hazijawa obsolete bradha bado ziko kazini kama ilivyo AK 47! Hiyo ni ya 1947 lakini bado ni moto wa kuotea mbali hata hizo za kisasa kama UZI ya Israeli na nyingine nyingi hazioni ndani!
Ina maana hujui kama AK47 zilishastop kutengenezwa muda tu? Kweli tunajadili haya mambo na watu ambao hawana uelewa wa kutosha.
 
Hao wanaoonesha silaha kali unafkiri hazina yao itakuwa ina nini?
Haya basi!
Screenshot_20211209-152123.png

Screenshot_20211209-152148.png




Screenshot_20211209-152202.png

Umeshajua nchi yenu wananunuaje silaha za kivita. Na sio hizi tu nyengine ni ndege vita za kisasa wamenunua ila hawazionyeshi. Hata hizi taarifa zikitoka Tz wanazikanusha. Na kuna nyengine walishirikiana na North Korea kwenye mambo ya kijeshi. Tz falsafa yao ya kijeshi hawaonyeshi silaha zao zote ama silaha za kisasa. Kama wengine wanafanya ni wao ila Tz hawafanyi. Kama mataifa makubwa yanafanya ujue wanafanya matangazo ya kuuza zana zao. Na marubani wengine walipelekwa Canada kwa mazoezi ya kujifunza zaidi.
 
1.Nacho amini, uwezi unyesha kila kitu ulichonacho utawapa advantage maadui wako
2.Nchi zilizokua za kikomunist ziliwekeza sana kwny jeshi bila kujitangaza, ila ikitaka kazi ziguse ndo utajua uwezo wao.
3.Kwa jwtz hii ndo outing yao kubwa kitaifa kwahiyo wansheherekea wakiwa pamoja nasi lkn bila kuuza siri za kazi.
4.Nachowapendea zaidi jwtz ukiwa nao wanajitambulisha kama JESHI LENU sio JESHI LETU.
Mfano: jeshi lenu litaenda Kongo kulinda amani, na sio hutaenda au jeshi letu litaenda ........
ALL IN ALL JWTZ NI MOJA YA MAJESHI YENYE NIDHAMU SANA DUNIANI.
Kwenye maonyesho kama haya, si rahisi nchi kuonesha nguvu yake halisi ya kijeshi.
 
Ni risk sana kuleta silaha mpya kwenye maonesho ya wazi kama ya leo pale uhuru stadium...
Nakumbushia tu... Komandoo Kagame alikuwepo...

NB: Always play low profile to confuse your enemies...
Hakuna cha low profile wewe. Kwanza wote hapa unaoona wana uelewa na silaha usidhani huwa wanaziona kwenye maonesho. Silaha sio vikombe kwamba utasafirisha umevificha.

Nchi inayouza silaha imesaini mkataba kutouza silaha kwa rogue militaries labda ziwe defensive. Ndio maana nchi kama Iran kuziuzia jet fighters ni ngumu ila Urusi ikijibana inaziuzia air defence systems. Kwa hali hii mauzo ya silaha yako monitored na taasisi binafsi kama SIPRI na Jane's Defense ambazo hutoa machapisho. Sisi tunaenda soma uko na kila silaha ukiwa unafatilia kuna sehemu ya kuona operators. Kama nchi haijakidhi vigezo ikiuziwa ni lawama, nchi ikiuza kwa kukiuka wanaweza kuiwekea vikwazo isiuze tena. South Africa ni nchi pekee ninayojua haijawahi uza silaha kwa nchi ya kutia mashaka, hata Canada wafuatiliaji.

Yani kama unavyonunua Bombardier ikajulikana. Hata ukinunua silaha itajulikana kwa wanaotaka kujua
 
Back
Top Bottom