Demand ya nchi ni kiasi gani?
Installed capacity ni kiasi gani?
Bwawa linaenda kuongeza kiasi gani?
Unajua tatizo kubwa la umeme uliopo sasa kushindwa kukidhi mahitaji ya viwanda vingi na pengine hata majumbani sio Outage? Ndo mambo ya kukwamisha kama lile la kule Congo?
Nini kingine? Usimamizi mbovu?
Wanasema mpango wa kujenga Transmission line ulikuwepo, ukichochewa na yule aliyeiacha mi-turbine yake inaoza bandari mojawapo huko pwani.
Inanong'onwa kuwa plan ilikuwa, serikali iwajengee transmission line ili wao wajenge plant itakayoweza kuzaliza 2,100MW na kuuza ndani na nje, line ifikishwe mpakani pale.
Inasemwa kuwa mpango uliuliwa na mwamba kwakuwa lengo lilikuwa ni chafu, kuua Power Generation ya Tanesco ili wao ndo washike hatamu, mzigo wa transmission na madeni ya distribution yabaki kwa serikali. Unadhani nini kingefuata baada ya muda mfupi, WAULIZE SA.
Kwani mradi wa umeme wa upepo pale Singida ni wa nani eti? Wanaanz a na 100MW?
Kwanini hatutaki kwenda na Geothermal ambayo imeshasemwa kuwa na uwezo wa kutupa 600MW? Kenya wanakimbiza kweli kweli kwenye hiyo!