Kama sio Maaskofu wa Kanisa Katoliki, Watanzania tulikuwa tunapigwa na kitu kizito sana na DP World

Bandari lazima irudi kwenye ufanisi. Dp World au mwengine lazima awekeze.
Wapi watu wamebishia uwekezaji? Ni vipengele vya kinyonyaji vya mkataba ndio vinaoigiwa kelele, sio uwekezaji..

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
maaskofu wa katoliki kipi wamefanya? serikali haiyumbishwi na maadkofu wa katoliki,walimchezea mwinyi na jakaya,kwa maza anakula nao sahani moja
 
maaskofu wa katoliki kipi wamefanya? serikali haiyumbishwi na maadkofu wa katoliki,walimchezea mwinyi na jakaya,kwa maza anakula nao sahani moja
Labda hufuatilii mambo au unaongea tu bila kufikiria. Iko hivi, Maza amekubali mziki wa waraka akaona yaishe wakasitisha kupitisha sheria ya maliasili. Au hujui kwamba tayari DPW kashawekewa barrier.
 
Maprofesa wa Vyuo vikuu wapo kimya Kanisa ndio limeona umuhimu wa Rasilimali za Nchi...Katoliki mpo sawa sana na mnaangalia mbali aisee...
Ni waajiriwa wa Serikali hao.
Wanaogopa kufutwa kazi, si unajua Maprofesa wetu wanategemea ajira.

Kimaadili Mtumishi wa umma huruhusiwi kumkosoa Raisi wa Nchi hadharani.
 
Ha ha ha!
Kitu kizito!
 
Aliyesaini mkataba ule kule Dubai ni mtaalam mbobezi wa sheria za mikataba ya kimataifa.

DP World anakwenda kupangishwa magati namba tano mpaka saba, namba nane mpaka kumi na moja ni mwekezaji mwingine.

Unapolaumu kilichoandikwa kwenye IGA ya serikali na DPW, umewahi kuiona mikataba mingine inayosimamia utekelezaji wa miradi mingi inayoendelea hivi sasa hapa nchini?, unajua nini kimeandikwa humo?.

Tupunguze ujuaji wetu.
 
👍
 
Wakikusikia....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…