Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

Kwahyo wanaosoma st kayumba hawawezi kujieleza kwa kiingereza aiseee unashida mahali sio siri
 
then unadhani atawachaleng kwenye kupata ukwasi huko mbeleni kwa A in class ni sawa na A kwenye maisha....mzee wekeza asset ama mtaji wa kutosha.... kama unataka kutengeneza bright future ya mwanao... we elimu yako sasa hivi ukifa haimsaidii kitu kama ambavyo ungemwachia ngombe... kuliko kutumia ada kubwa kumpeleka shule hizo nyingine bakiza mnunulie ngombe....(asset)
 
Mtoa mada shule za bei nafuu ni kuanzia kiasi gani kwa mwaka?
Nadhani mtoa mada atakuwa niwakukurupuka. Hajui tanzania elimu ni bure kuanzia chekechea hadi Form 4? Elimu bei nafuu ni form five to six tu ambayo mzazi analipa elf70. Na hauwezi kwenda f5-6 kama hujasoma elimu ya bure.
 
Shule za kayumba ni za kipimbi mi sina kitu ila nikiwa hai na nguvu zangu sitakubali mwanangu apitie niliyo yapitia Eee Mungu nisaidie
Ulikuwa kilaza tu usimuaminishe mwanao yale uloshindwa akija kujua ataja kukuchukia
 
Unaandaa bomu I will tell you that right now.

Mtoto mswahili kujidai mzungu na mzazi kufurahia ni recipe ya bomu. Ipo siku huyo mtoto atakuuliza kwanini yeye sio mzungu maana anaona uzungu ndo utu, uafrika sio. Hii haina maana mtoto asijifunze kiingereza.
 
Tatizo tumetekwa na fikra potofu utasikia yani nimeenda kwa mtu flani nimekuta watoto wake wanaongea kiingereza tu hadi raha je wanafundishwa kuwa wabunifu ? Je mtoto anafundishwa kutumia kipaji alichonacho ili kiweze kuja kumsaidia baadae? hivyo wazazi wengi hawaviangalii wao wana focus kwenye kiingereza tu ukimpeleka mfano kwenye maths , Physics bure ukimpeleka kwenye Biology mtupu kwenye swala la kuwa mbunifu kutokana na kipaji alichozaliwa nacho ni bure mwisho wa siku mtoto anamaliza shule anakaa nyumbani bila kazi anashindwa kabisa kuwa mbunifu

Somesha mtoto kutokana na kipato chako ila usimamizi wa maendeleo yake kwa karibu ni muhimu, kila mtoto ana uwezo katika kitu tofauti kama hawezi A anaweza B
 
Moja ya comment bora sana,

Swali ni je,serikali ya zamani ambayo haikua vizuri financially iliwezaje Ku offer package nzuri ya elimu kiasi hiki wakati hii serikali ya uchumi wa kati ni utopolo tu?
 
[emoji15]
 
Mkuu pole sana kwa kuchelewa,dunia ishafika mbali sana tena sana.

Endelea kuwazia siasa za ujamaa na kujitegemea.

Uafrica siio utu ni unafiki mtupu,chuki nk.
 
Huku dasarama Mali asili hawaruhusu ng,ombe kufugwa mjini.
MPE mtoto elimu bora sio bora elimu ,akiipata basis ndo urithi wake mpaka kufa kwake.
 
Nadhani mtoa mada atakuwa niwakukurupuka. Hajui tanzania elimu ni bure kuanzia chekechea hadi Form 4? Elimu bei nafuu ni form five to six tu ambayo mzazi analipa elf70. Na hauwezi kwenda f5-6 kama hujasoma elimu ya bure.
Kwa hiyo waliosoma private hawafanyi mtihani wakitaifa w4m4_akifaulu anachaguluwa kwenda hizi five za gava pia ujue.

Uongo hautakuweka huru kamwe.
 
Bosi huyo anakipaji hata angekuwa st kayumba angekuwa juu tu mimi nina mdogo wangu yupo form Three Now Ilboru anawakimbiza mbaya hao wa sijui international school na dogo kasoma st kayumba
Nakubaliana na wewe 90%,Dogo Akiwa home likizo zake no kuangalia national geographic na labda Nickelodeon, etc,na umri alionao anaelewa mambo mengi sana through hizo tamthilia pia kwa msaada Wa shule anayosoma anaelewa kidhungu kinachongelewa humo kwwnye series.
 
Bosi huyo anakipaji hata angekuwa st kayumba angekuwa juu tu mimi nina mdogo wangu yupo form Three Now Ilboru anawakimbiza mbaya hao wa sijui international school na dogo kasoma st kayumba
Ila kidhungu chake kitakuwa poor, ,atawakimbiza kwenye hesabu na kiswahili labda.
 
Huku dasarama Mali asili hawaruhusu ng,ombe kufugwa mjini.
MPE mtoto elimu bora sio bora elimu ,akiipata basis ndo urithi wake mpaka kufa kwake.

Hiyo misemo wanasema maskini tu. Urithi wa mtoto ni mali, watu wanaachia mali watoto wao na wajukuu nyie mpambana kuwaachia vyeti tu.
 
Mkuu pole sana kwa kuchelewa,dunia ishafika mbali sana tena sana.

Endelea kuwazia siasa za ujamaa na kujitegemea.

Uafrica siio utu ni unafiki mtupu,chuki nk.

Mwanao akisoma mary mary anakua mzungu?

Wote waliosoma hizo shule wamekua wazungu au kutoboa?
 
Mwanao akisoma mary mary anakua mzungu?

Wote waliosoma hizo shule wamekua wazungu au kutoboa?
Wametoboa mkuu,so ndo hao wako BOT na TRA walitoboa interview. Wako alisoma kata mpaka chuo hawezi hata kujitambulisha, kutwa mpaka Leo anatembea na bahasha ya khaki ya A4 imejaa vyeti anapigwa tu kwenye interview.

NGOs kibao tu hapa nchini walioajiriwa in hawa wakwetu waliopita private,u
Huko hakuna uswahili.
 
Hiyo misemo wanasema maskini tu. Urithi wa mtoto ni mali, watu wanaachia mali watoto wao na wajukuu nyie mpambana kuwaachia vyeti tu.
Tunawaachia elimu kichwani,Mali ukiwaachia watanyang,anywa na nduguzo ukifa,ila elimu inabaki kichwani mwao mpaka wafe.
 
Huku dasarama Mali asili hawaruhusu ng,ombe kufugwa mjini.
MPE mtoto elimu bora sio bora elimu ,akiipata basis ndo urithi wake mpaka kufa kwake.
ukisikia ngombe akili unaipeleka kwa mnyama sawa...mooo... hio elimu iliyo bora umeshindwa kuelewa andiko langu....biblia inasema kwa lugha nyepesi fedha na mali mtu huridhi kwa babaye..usikimbie majukumu ya kumiliki mali kwa ajili ya uridhi ukidanganyia elimu ndio urithi... tafuta fedha na mali ya kurithisha wanao...(ndio maana ya ng'ombe)
 
Sasa hivi priority ya wazazi wengi ni Chakula, ada afu ndiyo hela ikibakia Mavazi kidogo na ujenzi..

Wazazi wengi wana site miaka 10 hadi 15 nyumba haijapauliwa maisha ni magumu sana kwa kweli.

Ada ya 2.5m kwa mwaka kwa mtoto ni kitanzi kikubwa kwa wazazi..na ukifikiri kumpeleka hizi za umma za bure ni kama mwanao unammaliza kabisa...hazina ubora!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…