Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo


Dah, yaani umeongea kama wale jamaa wa kulima matikiti kwenye pdf.
 
Ukimsomesha mwanao kayumba mtaani unachekwa,kuna mother mtaani kapanga chumba kimoja halafu anamsomesha mwanae efemu akademia anachukuliwa na gari.......Ni maamuzi tu tuwaache mambo yakiwa magumu watawarudisha KAYUMBA.
Kuna wazazi wanapata stress ikifika kipindi cha kulipa ada mpaka wanatia huruma.
Kuna mtoto amekaa wiki tatu hajaenda shule tatizo ada.
Mwingine alikuwa analalamika hela imekuwa ngumu plus anadaiwa term ya nyuma hivo mtoto hatapokelewa atleast angekuwa anadaiwa mwaka huu mpya wa masomo wangemvumilia kidogo.
Mimi kwakweli nikija jaaliwa kama nikiona maisha yangu tia maji tia maji wala sitaki stress aende tu kayumba nitajitahidi asikose tution na kumsimamia.
Muda mwingine unakuta mtu anateseka na kumhamisha hawezi anawaza walimwengu watamuonaje.
Pata picha una watoto watatu halafu hela yenyew yamawazo lazima akili ikukae sawa.
 
Kwa laki nane hiyo hiyo,watoto wanasomeshwa shule za English medium,assets zinanunuliwa,na mipango mingine ya siku za usoni inajengwa,na unaposema shule za gharama ilibidi ufanunue,we wakati unaona millioni moja ni pesa kibao kulipa Ada,wenzio wanalipa millioni 3!na huyu wa millioni 3,akifikiri analipa ada kubwa,Kuna watoto wanalipiwa millioni 40! Kwa mwaka,Tanganyika international school!
La muhimu ni kulipa Ada kwa uwiano wa kipato chako,
Wakati mwingine,ada kubwa sio Elimu bora,shule yenye ada ya millioni moja,Dodoma,hapa Dar shule ya kiwango hicho na hadhi ni laki sita tu.
 
Huu ni Uongo, mwanao ni Extra Ordinaly na Sio Sababu ya hizi Shule.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mada gongana....
Kuna wengine wanalazimika kutetea kayumba sababu ya hali za kiuchumi..

Kuna wengine hali za kiuchumi ni mbaya ila wamepeleka watoto shule za gharamaa, wanatetea uamuzi wao kumpiga mtoa mada.

Kuna ambao wanaangalia na Uwezo wa mtoto..

Kuna watu akiona mtoto yupo bright sana ndio anaamua kumpeleka shule za kayumba maana anaona haina haja kuumia ikiwa tayari ana uwezo ambao hauhitaji nguvu kubwa.(hapa ni kubeti, either uokoe pesa kweli au ndio ukamharibu).

Kuna wengine akiona mtoto yupo bright hampeleki mwanae kayumba asije akalemazwa hatimaye anaamua kumpeleka kwenye shule kubwa za private ili akatakate vizuri.

Mwingine atasema mwenye uwezo mdogo mpeleke kayumba asikupotezee hela, Mwingine atasema huyo ndio umpeleka Private ili wambadilishe.
Hapa napo ni kubeti, huko kayumba either ukampoteze zaidi au apate cha uwezo wake uokoe pesa zako,
Private nako either ukapoteze hela zako asibadilike kabisaaa, au kweli Akafanye mapinduzi.


Ni kweli watoto huathiliwa na mazingira kadiri anavyokua, ila hakuna ubishi kuna watoto unaweza kuwatambua uelekeo wao mapema,
Mwingine umempeleka kindergarten tuu ashaanza kufunguka akili anaaza kujitambua mapema.
Mwingine unalazimika kumpeleka mpaka STD 7, 4M4, 4M6 mwingine Chuo,
Ila kuna ambao mpaka anamaliza chuo Hajitambui,

Binafsi naona Hata kama huko mbeleni ataenda serikalini ila angalau mpaka darasa la saba aende english medium umwangalie.

Baada ya hapo kama unawaza kumpeleka serikali basi angalia vitu viwili, Nini umegundua kutoka kwake(japo hapa napo ni mtihani sababu mda mwingi hukua nae?) lakini pia angalia na hio shule pia.

Lakini pia kumpeleka shule za gharamaa mwanzo mwisho halafu chuo anagombania mkopo ambao haukua na lazima mwishowe anapata kazi mkopo unamtesa au anarudi mtaani kabisa, hapo lazima uwaze noti zako.

Binafsi naona kwa dunia ya sasa kila yule kupata elimu ni jambo la kawaida, Mtoto mwenye uwezo mkubwa hasa huyo ndio wa kumgharamikia hasa kwenye elimu,

Sio tuu mfano mwenye uwezo wa div 1, maana hii ni kawaida, hapa namaanisha unaona kabisa huyu ana cha ziada zaidi ya hapo.
 
Unafiki wa siasa za afrika wanaosema hiz shule ni nzuri Sana watoto wao hawasomi huko sasa utajiuliza huyu anasimamia hiz shule na kuzisifia kuwa zipo vizuri mbona hampeleki mwanae....Unafiki wa muafrika
 
Huu ni Uongo, mwanao ni Extra Ordinaly na Sio Sababu ya hizi Shule.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu baadhi ya shule za private zina makusudi sana,yani wanatafuta kuzipatia shule sifa katika ufaulu ili wapate wateja.

Ila mkuu usijali mi mwenyewe ni zao la shule za kata,kwa hivyo nimeona utofauti kwa kweli.ingawa sio shule zote ziko vizuri.
 
Anakutana na A level waliosoma kuanzia la kwanza hadi form six shule za kata,ila wale waliotoka shule za private wakaenda A level shule za sirikali hao nadhani hajakutana nao maana watakuwa vizuri mkuu.
 
Angalia huyu mshamba mwingine huku duniani, watu wanamaanisha maisha ya mtu baadae pamoja na kusoma hizo english school na mtu aliyesoma kayumba,ukweli ni kwamba watu wa kayumba wengi ndo utakuta wanatoboa maisha, hawa wa kwenu ambo unakuta wanasoma wengine mihula ya uingereza huishiaga kwenye ubishoo tu na wanatafuta kwenda kufanya kazi nje, kule ukubwani au uzeeni wanarudi na mikogo tu ya kutembea wametanua mikono na miwani ya jua machoni huku wameacha kizazi chao kikiishi utumwani ugenini na kua wamekimbia aridhi ya uzao wao,endelea kumsifia wa kwako bado yuko darasa la 7, huyo siyo jiwe anakua, akikua utaona kitakacho tokea labda tu awe amezaliwa na utashi wa asili, vinginevyo utajuta tu maana tumewaona wengi kwenye familia na majirani
 
Uhakika wa kufaulu upo kwenye private schools. Pitia matokeo shule za serikali. Hali ni mbaya.
hayo maneno ya "ufaulu umeongezeka" yasikie hivyo hivyo
Kufaulu maisha?
 
Hata kiingereza chenyewe wanachokijua si kwa kiwango hicho kwani hata Waalimu wanaowafundisha wanababaisha tu. Mi nazani wazazi wengi wanafuata mkumbo tu ila sizani km wanafanya tathmini ya gharama za huo uwekezaji.

Mbaya zaidi mfumo wetu wa ajira unaangalia sana ufauru wa kwenye cheti bila kujali kujua au kutokujua kiingereza.
 
OK.
Ndio wanatoboa maisha,na wanakua viongozi kweli hebu angalia wanakotupeleka kama taifa kimataifa yani ni aibu tupu.

Hii nchi sa hivi hata wewe ukitoka nje ya nchi huwezi tembea kifua mberee kuwa unajivunia utanzania,katika east Africa sa hivi Rwanda wanatupita.
 

Sikuelewi unaposema mtoto wako wa Std 7 medium School Ana m Challenge Mtu wa A Level za Kata !!!
Mtu wa Combination gani ipi hasa.
Kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…