Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

Kujiamini unamjengea mtoto wewe mwenyewe.

Kujifunza kutafuta maarifa ni zao la malezi hasa nyumbani.. mtoto anatakiwa ajifunze kupata kwa kutafuta.. sio kupewa..

Wengi majobless wanaopaka Poda Sinza wamesoma Medium kwa wengi ni swala jipya.. maana ndio tunashtuka.. ila hazina jipya lolote.. niamini.

Tumesomesha sana huko private na kumalizia Bablo na bado anafika UD anakuta vipanga wamesoma shule ya msingi Yombo, sekondari Gongo la Mboto, high school Benjamini na wananyoosha na in two or three years kingereza nao wanakijua na wanajua kuona fursa na kuzitumia.

Wanamuuzia mwanao T-shirt za kuprint, wanamleta visheti ambavyo yeye hajui hata kupika, wanaleta ubuyu.. yeye anatoka umtafutie na kazi...
Acha kupretend kwamba wanaoshinda vijiweni kubet na kucheza pool table wanawazidi wapaka poda sinza

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
90% ya wasomi wanafanikiwa?? Ebu tupe definition ya kufanikiwa kwanza!! Maana hao wasomi wa kutegemea mshahara na kununua gari na kujenga kwa mkopo,mshahara ukitoka tarehe 28 baada ya siku 10 ushakata ndio mafanikio hayo?
Tofautisha kati ya utajiri na kufanikiwa standard za kufanikiwa ni basic need good food, good shelter na good cloth achana na illusion za lamborghini so wasomi kweli wamefanikiwa

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Ukiwa mji wa kielimu.. ni kumjengea mtoto tabia.. anasoma shule ya kawaida.. anatumia muda wake vizuri. Anaratiba ya library, ana tembelea maeneo kujifunza kwa vitendo ndio kumjengea mtoto uwezo. Sio kulipa hela nyingi apewe taarifa na kuaminishwa vitu.

Apate vitabu, mtembeze aonane na Mainjinia, tofauti tofauti.. aone processes mbalimbali anazojifunza kwa nadharia.. hivyo ndio kumpa mtoto elimu..
Halafu aende shule ambazo wanaambukizana vichocho wanachapwa viboko vinatoa hadi nyama wanakuwa wachafu kijiamini hafifu wanashindwa lugha ya kujielezea kimataifa na kushndwa kujifunza ulimwengu mpya ambao ni internet

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Hiyo ni sawa na yule mtu aliyemuuliza mlevi wa pombe, kiasi anachokunywa kwa siku,mwezi na hadi mwaka, gharama yake ilikuwa ni sawa na bei ya kununulia Benzi, lakini muulizaji alipoulizwa wewe ni mlevi?akajibu hapana, akaulizwa una benzi ngapi? Akajibu hana hata moja. So kwa kutomsomesha mtoto kwenye hizo shule hakumaanishi kuwa utaserve hela na kumnunulia huyo mtoto any asset, kama uwezo upo, hata wa kuteseka msomeshe mtoto, vinginevyo waweza kosa mwana na maji ya moto
Bars!! Nimeongea kihip hop kuongeza msisitizo wanaprerend kuwa hawana ulevi hawana nyumba ndogo hhhhh ila 2 wamtese mtt. Trust Me watt wa kayumba waliozingua ni wengi kuliko watoto wa shule bora waliozingua unaleta mfano wa mtu moja katika mamia haukidhi vigezo

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Unatumia nguvu nyingi sana ktk kumsomesha mtoto, mwisho mtoto anamaliza Shule hana kazi na wewe mzazi huna kitu. Hata akipata kazi fedha anaanza kukurudishia kwa kukulea.

Ila ukianza kuwekeza, hata kama atapata Elimu ya kawaida. Mzazi akipata hela mtoto lazima atapata hela.
Em acheni roho za kimasikini na kukata tamaa kwani shule nd inafirisi mtu mtaje huyo mtu je akiwa kayumba nd ana uhakika wa kufaulu sasa kwamba ukifulia atakusaidia asset zinakufa na mtt hana elimu whats next

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Tofautisha kati ya utajiri na kufanikiwa standard za kufanikiwa ni basic need good food, good shelter na good cloth achana na illusion za lamborghini so wasomi kweli wamefanikiwa

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app

Hata hizo basic needs kwa wasomi bado mkuu ,ikifika tarehe 8 hawana kitu wanaishi kwa kudunduliza kwa mangi na mizinga....Kufanikiwa kwa wasomi inatakiwa awe Middle class......Maana hata hizo Basic needs mmachinga anapata zaidi ya hao wasomi.
 
Chuoni ndo nimegundua kuwa wale walosoma private na government kumbe wanakutana na hapa atakayekuwa mzembe anaachwa na mtu active anasonga mbele...wala hawana tofauti.

Kama mzazi utaona mwanao kuna mahali anapwaya, mpeleke private, ila kama unajua ni jembe, hakuna haja ya kumpeleka private.

Nimesoma shule zote, naelewa.

wadogo zangu walonifata wote nlimshauri mzee awaache government na kwa sasa mmoja yupo chuo na anaperform vzur tu.

wengine wapo advance.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajichanganya au umechanganyikiwa na hoja yako!!

Unamuongelea kapuku hana chochote kwamba anashindana na wenzie kusomesha shule za gharama.

Hapo hapo unahoji kama shule aliyosoma haijamsaidia amewezaje kupata kazi nzuri!

Huyo huyo kapuku ndo huyu mwenye kazi nzuri au umeungaunga kwa gundi watu tofauti?

Hoja yako ni ya kuokoteza.
Naongelea wote wawili kwa pamoja.
--yule aliyesoma shule ya kayumba na ana kazi nzuri.
-- yule kapuku hana chochote hata chumba kapanga kwa Mzee jangala.

Wote kwa pamoja mnapoteza gharama zenu.
Mtoto akifika chuoni hawana tofauti yeyote kati ya aliyesoma kayumba na shule za gharama.
 
Haya mambo yako very tricky! Lengo la kila mmoja ni mtoto wake apate elimu nzuri baadae aje aitumie elimu hiyo kupata pesa nzuri. Let us do whatever it takes kuweza kuyaachieve haya yote walau kwa usambamba.

Msije mkawa kama mtu fulani anayejenga miradi ya kimkakati akimaliza ndio aongeze mishahara, matokeo yake hii ni 2021 hakuna mradi wowote wa kimkakati na mishahara haijaongezwa 😀😀 (nimechomekea tu watani, kama yeye ambavyo huwa anachomekea)
 
Mleta mada inabidi ujue tofauti kati ya English Medium na International School, International school ni chache sana na zinatumia mitaala ya kimataifa i.e IGCSE, etc ila English medium ni kufundisha kwa kiingereza tu...IST, ISM,Savanna,Canon Andrea Mwaka hizo ndo international schools...
 
Angalia huyu mshamba mwingine huku duniani, watu wanamaanisha maisha ya mtu baadae pamoja na kusoma hizo english school na mtu aliyesoma kayumba,ukweli ni kwamba watu wa kayumba wengi ndo utakuta wanatoboa maisha, hawa wa kwenu ambo unakuta wanasoma wengine mihula ya uingereza huishiaga kwenye ubishoo tu na wanatafuta kwenda kufanya kazi nje, kule ukubwani au uzeeni wanarudi na mikogo tu ya kutembea wametanua mikono na miwani ya jua machoni huku wameacha kizazi chao kikiishi utumwani ugenini na kua wamekimbia aridhi ya uzao wao,endelea kumsifia wa kwako bado yuko darasa la 7, huyo siyo jiwe anakua, akikua utaona kitakacho tokea labda tu awe amezaliwa na utashi wa asili, vinginevyo utajuta tu maana tumewaona wengi kwenye familia na majirani
Hapa kuna harufu ya chuki na wivu hivi hawa wanaokaba mtaani wanobet wanaocheza pooltable mbona ukiwaongelesha kiingereza hawajui ila mtt aliesoma kingereza akifeli mnaitupia lawama elimu yao daa inachekesha...mm hawa watu wa english medium wengi sana wanajitambua usipindishe jambo kw kuangalia m2 mmoja mmoja hapa ishu usimpeleke mtt shule ambayo huwezi kumudu full stop

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Usichanganye kipaji na elimu, uko umeenda mbali kwani Diamond ana hata Diploma? Lakini ni Millionaire anawazidi maisha Maprofesa wote wa Tanzania.

Ana pesa kuliko Maprofesa wote wa Tanzania.
Kuna kina Diamond wangapi Tanzania ambao hawana shule (hata diploma) ukilimganisha na walio tia maji maji wasio na shule , hadi u conclude usipokua na elimu unakua millionaire ila ukiwa na shule unakua kapuku?
 
Back
Top Bottom