Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

Sehemu tulipowezwa ni hapa..

Mtoto wako, anakuja kuishi Tanzania hiii hiii unahangaika awe mzungu..hahaha.. na anafundishwa matatizo ya kizungu, kwa lugha ya kizungu..akitoka huko ameshakuwa mzungu anakuja kwa watanzania mtaani anaanza moja.. 🙂

Na cha kufurahisha ni sisi wazazi ndio tunakuwa tumewanunulia watoto wetu hiyo delay huku mtaani. Elimu tuliyomnunulia ndio imekuwa kikwazo..

Bora kila mwaka ungekuwa unamnunulia mtoto ng'ombe nne.. anasoma shule ya laki tano kwa Temu.. akija kumaliza shule anakuwa na ng'ombe 68, ukiweka kuzaa na kufa hakosi ng'ombe 100 kwenye kipindi cha miaka 16 ya kusomea elimu.

Na elimu yenyewe ndio imekuwa uchuro uchoro mtupu
Urithi pekee wa kuaminika wa kumwachia mwanao ni elimu tu!!

Hizo ngombe anaweza kuamka zimeibiwa zote unless uzikatie insurance..
 
Tunawaachia elimu kichwani,Mali ukiwaachia watanyang,anywa na nduguzo ukifa,ila elimu inabaki kichwani mwao mpaka wafe.

Kwanini wanyang'anywe? Huandiki mirathi? Huna wanasheria?

Watu wananyang'nywa mali sababu mzazi umetengeneza hayo mazingira, ukiweka safeguards in place hakuna atayegusa mali zako.

Kusingekua na kina Mo Dewji au Azam kama wangekua wanarithishana vyeti tu, wao wanarithishana mali huku wanaambia watanganyika walianzia kwenye asiklimu.
 
Urithi pekee wa kuaminika wa kumwachia mwanao ni elimu tu!!

Hizo ngombe anaweza kuamka zimeibiwa zote unless uzikatie insurance..

Hayo maneno wanaambiana maskini tu. Urithi ni mali na basic edu tu ya kuendesha hizo mali.

Hayo makaratasi mtarithishana huku hamna hela wakati wenzenu wanaachia hadi wajuu zao mali. Kusingekua na kina Mo au Azam kama wangekua wanaachiana vyeti tu.
 
Wametoboa mkuu,so ndo hao wako BOT na TRA walitoboa interview. Wako alisoma kata mpaka chuo hawezi hata kujitambulisha, kutwa mpaka Leo anatembea na bahasha ya khaki ya A4 imejaa vyeti anapigwa tu kwenye interview.

NGOs kibao tu hapa nchini walioajiriwa in hawa wakwetu waliopita private,u
Huko hakuna uswahili.

Afu wakuu wa hizo taasisi zote kuanzia TRA, BOT hadi Rais mwenyewe wote wamesoma Kayumba. Ndo utakapojua hujui.
 
Sasa hivi priority ya wazazi wengi ni Chakula, ada afu ndiyo hela ikibakia Mavazi kidogo na ujenzi..

Wazazi wengi wana site miaka 10 hadi 15 nyumba haijapauliwa maisha ni magumu sana kwa kweli.

Ada ya 2.5m kwa mwaka kwa mtoto ni kitanzi kikubwa kwa wazazi..na ukifikiri kumpeleka hizi za umma za bure ni kama mwanao unammaliza kabisa...hazina ubora!!
Umeandika kwa uchungu sana mkuu. I feel you.
 
Afu wakuu wa hizo taasisi zote kuanzia TRA, BOT hadi Rais mwenyewe wote wamesoma Kayumba. Ndo utakapojua hujui.
Mkuu huoni nchi kama nchi ime fail mambo mengi sana hasa kimataifa kwa kuwa na viongozi waliosoma st kayumba hawana uelewa wala exposure.
Angalia mfano hapa
 
Kwanini wanyang'anywe? Huandiki mirathi? Huna wanasheria?

Watu wananyang'nywa mali sababu mzazi umetengeneza hayo mazingira, ukiweka safeguards in place hakuna atayegusa mali zako.

Kusingekua na kina Mo Dewji au Azam kama wangekua wanarithishana vyeti tu, wao wanarithishana mali huku wanaambia watanganyika walianzia kwenye asiklimu.
We unafananisha utamaduni Wa waarabu na wahindi,wale wanaoana ndugu kwa ndugu hawawezi nyang,anyana Mali maana wote in wamoja,kwanza wanaishi pamoja ndugu wengi.

Itabidi uanzishe Uzi humu kati ya elimu na Mali kipi bora tuone wadau wengi wako upande wako au wangu.
 
ukisikia ngombe akili unaipeleka kwa mnyama sawa...mooo... hio elimu iliyo bora umeshindwa kuelewa andiko langu....biblia inasema kwa lugha nyepesi fedha na mali mtu huridhi kwa babaye..usikimbie majukumu ya kumiliki mali kwa ajili ya uridhi ukidanganyia elimu ndio urithi... tafuta fedha na mali ya kurithisha wanao...(ndio maana ya ng'ombe)
Hiyo biblia uliyoiquote ni enzi za kina Nuhu wewe,sa hii dunia in nyingine kabisa mkuu.

Acha kabisa SAA hii watu wantafuta kwenda kutalii mwezini na kurudi we unaongelea kitu gani lakini.
By the way nyie ndo mtaji Wa CCM.
 
Mkuu wangu Bufa tafuta hela usomeshe wanao shule za maana wakikuwa watakuheshimu na kukusifu wana Baba mwamba kwerikweri.

Sasa wewe hela unatafutia michepuko afu watoto unamwachia magufuli apambane nao kuwasomesha bure.

Vya bure gharama.
 
TAIFA LINA MAJONZI
KILA MTU APAMBANE NA HALI ZAKE
 
Mkuu wangu Bufa tafuta hela usomeshe wanao shule za maana wakikuwa watakuheshimu na kukusifu wana Baba mwamba kwerikweri.

Sasa wewe hela unatafutia michepuko afu watoto unamwachia magufuli apambane nao kuwasomesha bure.

Vya bure gharama.

Mkuu mimi hoja yangu ni watu wasomeshe watoto wao within their means. Sasa hali ni ngumu unakuta mtu kwa mwezi anainginza lak3 ila bado anataka watoto wasome shule za 3M kwa mwaka, hapo atakopa na kuuza mali zake chache alizonazo zote ili tu watoto waende shule za gharama.

Aidha exposure is natured, ni vile mzazi utavyomkuza mwanao. Kama unataka mwanao awe mpembuzi atakua haijalishi kasoma shule gani.

Nje watu wanafanya home schooling na bado anakuwa sawa au zaidi na wenzake wanaoenda darasani kila siku. Hii inaonyesha elimu sio kwenda shule za gharama tu bali ni malezi kwa ujumla.
 
Mkuu tutabishana sana mi na wewe Leo,unasema exposure ni natured sio kweli.

Nakupa ushauri Wa mwisho ukatae ukubali,kama unaishi mjini una exposure ya kutosha.

Peleka mtoto private,ila kama uko kijijini huko hakuna hizo shule pelwka hata kwa ndugu huko mjini I'll mradi apatiwe elimu bora
 
Sawa mkuu let's agree to disagree.
 
Dah....tusijipe moyo...ili mtoto asome vizuri lazima mwalimu alipwe vizuri...mbona matokeo ya mitihani yanajionyesha wazi tu.....tusidanganyanye...chapa kazi tafuta Ada banaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ukiwa na kipato cha milioni 10 kwa mwaka.. ishi maisha ya milioni 3, wekeza milioni 3, tunza milioni 3 na milioni moja toa sadaka, saidia ndugu nk.

Ukiona unaishi maisha ya milioni 15, na kipato chako ni milioni 10.. kila mwaka unaongeza deni la milioni tano.. hakuna unachotunza.. ujue wewe ni Mtumwa.
 
Back
Top Bottom