Kama Tanzania ingeshindwa vita ya Kagera: Je, Rwanda na Uganda zingefika hapa zilipofika leo?

Thanks for complement but dah, I'm speechless! Nimechelewa sana kuiona hii post ambavyo ina lots of constructive questions na hoja fikirishi! Itabidi haya nayo tuyajadili kwa kina ingawaje nadhani sitakuwa available or active enough in the next 24 hours!! zitakuwa
 
Braza Malcom Lumumba salama?

Mjadala mzurii.Mi nafikiri ingekuwa ngumu au ingechukua muda mrefu kwa PK na M7 kuwa walipo. Amin alijua waasi wa Uganda ipo siku wangemvamia, hawakuwa TZ bure. Ndiyo maana moja ya sababu ya vita ni Idi Amini kushambulia na kufanya mto Kagera kuwa mpaka. Hii ingempa water barrier nzuri dhidi ya uvamizi. Sasa angeshinda vita angepata hii water barrier na ingekuwa ngumu kwa waasi kuivuka huku jeshi la Tz liko hoi kwa kipigo. Wangepita wapi? Rwanda hakupitiki, Zaire kuna Mobutu.

Nakubaliana ile vita ina repercussions ndefu sana, kieneo na kihistoria. Pengine tungepigwa hata mauaji ya kimbari yasingetokea, pengine hata zile Congo wars zisingetokea! lakini hizi ni counterfactual s tu japo zinatusaidia sana kuelewa tulipo.
 
Mkuu mimi nipo salama kabisa. Hapo juu Kaka Chige ametoa uchambuzi mzuri sana, upitie kama utapata nafasi. Lakini sasa leo asubuhi nilikuwa natafakari juu ya Vita ya Kagera, nikagundua kwamba kuna kitu ambacho nilisahau kukiangalia kwa ukaribu ambacho ni: Ongezeko la ushawishi wa mataifa ya nje ambayo ni rafiki wa Idd Amin kama Libya, Palestine na Saud Arabia endapo Uganda ingeshinda ile vita.

Nataka nifukunyue nyaraka kwa undani zaidi ili niweze kufahamu ni kwa kiwango gani haya mataifa ya nje yalikuwa na ushawishi nchini Uganda. Faida zipi za kidiplomasia, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni yalikuwa yanategemea hadi kupelekea yamuunge mkono Iddi Amini.


MENGINEYO MUHIMU KUJUA:


Mahusiano ya kidiplomasia baina ya Rwanda ya Wahutu na Uganda ya Iddi Amin yalikuwaje ???

Mahusiano ya kidiplomasia baina ya Uganda ya Iddi Amini na Zaire ya Mobuthu yalikuwaje ???

Mahusiano ya Kidiplomasia baina ya Rwanda ya Wahutu na Zaire ya Mobuthu yalikuwaje ???

Vita ya Kagera ni uzi moja mrefu sana unaotupeleka kwenye matukio makubwa kwenye huu ukanda: binafsi nataka kuufuatilia huo uzi hadi unapotokea ili kuyaelewa yanayotokea kipindi hiki na kujaribu kutabiri yatakayotokea kipindi kijacho na nini utakuwa mustakabali wa Tanzania ijayo...............

Mkuu panapo majaliwa ya Mungu naahidi kwamba nitarejea na hiyo tafiti........
 
Mkuu ningependa kujua zaidi Nkurunzinza ame deal nao vipi hawa ma covert?
 
Kuna kitu cha muhimu sana tumekisahau kukitaja hapa: Hivi bila Raisi Jakaya Kikwete na Waziri wake Benard Membe unadhani Pierre Nkhurunzinza bado angekuwepo kule Burundi mpaka kufika leo hii ???

Tanzania ingepata madhara gani kimkakati kama Raisi Jakaya Kikwete angeamua kufunga mikono yake ya kijeshi na kidiplomasia kipindi kile Raisi Nkhurunzinza alipofanyiwa jaribio la kimapinduzi na mamluki kutoka nje ???

Matatizo ya Burundi yanaathiri vipi usalama wa Tanzania na kwanini walihangaika sana kutaka kumtoa Pierre miaka michache iliyopita ???

Hebu tujadili zaidi.......
 
Je, Tanzania tulikosea kuwasaidia hawa ndugu zetu, hasahasa baada ya kuona mambo ya ajabu wanayoyafanya kule Congo DRC, na kwingineko?
Walioyafanya na yanayofanyika hapo DRC yana baraka za wakubwa (mabeberu) wao wanatumika tu.
 
Mkuu ningependa kujua zaidi Nkurunzinza ame deal nao vipi hawa ma covert?

Yeye nasikia anawatanguliza mbele ya haki tuuuu. Akigundua cell sijui network zao anawamaliza. Wanaenda kuambiana kwamba nkurunzinza ni noma. Wenyewe wanasema isingekuwa hivyo Burundi ingekuwa very shaghalabaghala mpaka dakika hii. PK hataki kabisa nkurunzinza abaki pale.

Nkuru hacheki na kima. Ukikutwa unafanya espionage na matakataka ya aina hiyo Huna bahati.
 

Burundi nayo ina idadi kubwa ya Tutsi, baada ya Hutu. PK akifanikiwa kumweka MTU wake Burundi (of course Tutsi) atakuwa amejikusanyia nguvu zaidi pamoja na kufanikisha tamaa zao binafsi kama wanavyoitaga superiority etc. Ukija kumchanganya na m7 itakuja kuwa shida kwa nchi jiran kama tz. Nafikiri bongo haihitaji kuzungukwa na nchi zenye ukaribu na maelewano makubwa halafu zilizojaa ukabila halafu zikiwa chini ya viongozi wababe, wapenda vita, wakabila, you name it. Wanaweza kulianzisha muda wowote.

Jiran akiwa na nguvu msuli halafu akawa mkorofi mtapata taabu sana. Of course naona hata ukijumlisha na Burundi bado watakuwa bado sana kwetu, lakini itakuwa si haba.

Kama kweli kuna suala la Hima Empire, Basi mkwamo mmoja ni Burundi kutokuwa chini ya Tutsi.

Weakness moja kubwa ya hao jamaa ni upinzani mkali wa Hutu against them. Mtu yeyote akitaka kuwashinda hao jamaa ni suala la kuungana na au kuwawezesha Hutu.

Nafikiri Nkurunzinza asingeweza toboa bila msaada wa Tz. Hata angetoboa ingemgharimu sana. Chezea hela anayopata PK kutoka Congo.
 
Basi kama ni hivyo Paul Kagame is overrated!
 
Huna habari nyingi wewe, hujui kabla ya vita kins museveni walikuwa wanapambana na Iddi Amin kutokea Tanzania?
 
Ndiyo maana TRUMP anatuponda sana sisi waafrika akili zetu ziko hoi bin taabani kuangalia WANAWAKE tu!
 
Haikuwa vita braza ilikuwa propaganda ya kumzuia Iddy Amini kutanga uislamu Uganda. Alipata Support kubwa toka kwa Gadaffi na walikuwa na mpango wa kujenga Mskiti mkubwa Uganda, ndo kisa kikaanzia hapo.
Ukipata nafasi nenda bukoba waulize Wazee wa kule wakusimulie Malcom Lumumba.
 
We jamaa una akili nyingi sana sijui unafanya kazi wapi. Huu uchambuzi umejaa akili za kipekee
 
Seblen Pub ipo wapi?
 

Nyerere mwenyewe ana tuhumiwa kua ni HIMA.

Which is which?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…