Kama UKIMWI wa 2005 kurudi nyuma ungekuepo sasa, hali ingekua mbaya sana

Kama UKIMWI wa 2005 kurudi nyuma ungekuepo sasa, hali ingekua mbaya sana

sanalii

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2018
Posts
1,639
Reaction score
5,767
Vijana wadogo wanafanya sana ngono zembe ( kuuza mechi) na wanawake ambao kama vile wameshajikatia tamaa au kujitoa mahuru, hawataki mwanaume atumie condom.

Nikikumbuka vile VVU vya 2005 kurudi nyuma,
1. Nywele zinanyonyoka af zilizobaki zinakua kama za kiarabu.
2. Mabega yanapanda juu na kukonda kusiko kwa kawaida
3. Midomo inababuka na kua na kama unga unga mweupe,
4. Kukohoa pamoja na mkanda wa jeshi mkali sana.

Kipindi kile ilikua haihitaji kuambiwa kujua mtu fulani ana UKIMWI,
Pamoja na lishe na ARV, bado nadhani hivi virusi vimepungua nguvu, vijana wanajiachia sana na hawana woga
 
Bila shaka kulingana na hali hiyo, waathirika walikuwa wachache kwasababu watu wengi walikuwa na hofu kubwa, hivyo walikuwa makini.

Sasa hivi watu hawana hofu na kitu inaitwa UKIMWI, kwasababu hata ukiwa nao unapendeza na kunawili kama kawaida (ukifuata taratibu zake)
 
Vijana wadogo wanafanya sana ngono zembe ( kuuza mechi) na wanawake ambao kama vile wameshajikatia tamaa au kujitoa mahuru, hawataki mwanaume atumie condom.

Nikikumbuka vile VVU vya 2005 kurudi nyuma,
1. Nywele zinanyonyoka af zilizobaki zinakua kama za kiarabu.
2. Mabega yanapanda juu na kukonda kusoko kwa kawaida
3. Midogo inababuka na kua na kama unga unga mweupe,
4. Kukohoa pamoja na mkanda wa jeshi mkali sana.

Kipindi kile ilikua haihitaji kuambiwa kujua mtu fulani ana UKIMWI,
Pamoja na lishe na ARV, bado nadhani hivi virusi vimepungua nguvu, vijana wanajiachia sana na hawana woga
Masidhani HIV haipo, ipo na inaua, isipokua HIV inadanganya kwa sababu inachukua muda mrefu, sifa ulizo sema hiyo ilikua HIV ya miaka ya 1995 huko, na kwa nini ni kama haionekani, ni kwamba watu waliopotea waliambukizwa miaka ya 1985 wakaja kuondoka 1995 -2000, wakaisha wakabaki wengine walioambukizwa ambao nao walichukua miaka kama 15 tena ndo wakaanza kupukutika, ni uogonjwa unao danganya maana toka miaka uliyosema inaelekea kwenye kupukutika tena, inachukua miaka 15 mapaka 20 mtu kuanza kuugua maambukizi na kuisha mwili na kufa, okay swala la madawa limechangamka na vyakula pia, siyo kama zamani na ndo mana vijana hawaiogopi wanaona watu wameng'aa na hawafi ila siku si nyingi wataondoka waliotoka nao miaka ya 2005-2010 Kisha itaachia tena watu watakao pukutika miaka ya 2030-2035

Ni hatari... Sema pia ugonjwa mkubwa na hatari kwa sasa ambao watu wanaugua na hawajijui ni Cancer, ni ugonjwa unajificha unakuja kumuibukia mtu uko stage three ambayo haiponeki tena, hatuna tabia ya kufanya check up Afya zetu Kwa hiyo mtu anakua na Cancer stage one, inakwenda two hastuki, anaanza kuugua wakipima iko stage ya mwisho, Dunia ni ngumu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dawa ya kunguni ni kuchoma nyumba na vilivyomo na dawa ya ukimwi ni kuwageuza kunguni wale wenye ukimwi
 
Nilikuwa mgum kupima ukimwi kwanza nimshuru mungu sana juma ilio pita nilipata ajari mbaya sana ya pipik nikavuja dam nyingi sana nikapeleke polis badae hospital katika arakati za kuokowa maisha yangu niliwapaka baazi ya manesi dam wakati naendelea kushonwaa nilisikia sauti ya nesi akisema ametupAka dam jibu likatoka mpime afya kubwa aka ukimwi asee nilikuwa mpole nimshuru majibu yalikuja akisemA afya yuko salama paka sasa naendelea kuguza madonda ila moyon na amani
 
hebu twambie; unafikiri kama ungekutwa nao ingekuwaje??
 
Back
Top Bottom